Ikulu imetumia sh bilioni 53 toka mwaka 2003

Wana JF acheni kulumbana. Toeni michango badala ya kulumbana!!!Mada imeeleweka hata kama hakuedit post yake.

Hivi ofisi za serikali zinakarabatiwa kila mwaka? Hizo hela zingesomesha wa Tanzania wangapi, zingesaidia wajawazito wangapi, zingejenga barabara ngapi, zingenunua dawa kiasi gani kwa hospitali zetu, madaktari na manesi wangeweza kuboreshewa mishahara ili wasitunyanyapae tukienda hospitali!!! Mbona siielewi nchi yetu!! Priority iko wapi??? Wafanyakazi wangeweza kuongezewa mishahara wanayodai na mengine mengi tu!!
Nawewe kupika rangi ndio nini au wanatengeneza mikeka..
 
Jf nisaidieni kwa hili. Kwani ghalama za kujenga ikulu mpya ni kama sh ngapi?

My friend, if you want to know signs of corruption in any organization have a look at the recurrent costs in their annual budgets, nazo ni... maintenance repair and operations (MRO), refershments, other consumables..... you know why?? hakuna justification kwa macho ya ku-quantify kazi zaidi ya makaratasi

sasa twende kwenye MROs... kama trend ni 7billion, 10 billion.. then yawezekana kabisa kuanzia 2005 JK alipochukua madaraka hii budget kufukia zaidi ya billioni ishirini. sasa nenda kaombe uone kazi iliyofanywa... huwa ni rangi, koki, vitasa, tiles, uzio nk. you cant separate rangi ya 2009 na ya 2010 na ya 2011 etc

THINK ABOUT IT, AND TELL ME WHY ONE LOVES TO BE THERE... YAWEZEKANA KABISA JK HANA CHAKE HAPO, BUT WALIOMZUNGUKA NI WATAALAM WA PROCUREMENT
 
kila mwaka hutengwa pesa nyingi za ukarabati wa ikulu,kwa mwaka huu ni tzs bilioni kumi,wanachokarabati ni nini?youk
 
Naomba yeyote mwenye taarifa sahihi atuwekee fedha ambazo zimekuwa zikitengwa kwaajili ya ukarabati wa ikulu katika miaka mitano iliyopita
 
wanakarabati wapi wanazitumia tu kwenye miradi ya riz1 kununua malori makubwa.Eti maisha kimjinimjini.Like father like son
 
Suzan Lymo amesema kuwa matengenezo ya ikulu yamegharimu shilingi bilioni 53, na mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 10. Je matengenezo hayo ni yepi?
 
kwani hujaona matengenezo?ikulu imepakwa rangi kwa aliyepita maeneo ya ikulu anaweza kushudia hili.Labda aulize Value for Money.
 
Jamani dodoma kuna nini??katikati ya nchi, kama tulivyofundishwa tangu tupo skuli kwamba ndiyo makao makuu ya nji hii njema. Tuliambiwa na kuaminishwa kuwa hii ndiyo makao makuu ya nchi na wizara kibao zitajengwa huko badala ya Daslam. Ndiyo tangu kitambo hicho mpaka sasa nchi yetu imegubikwa na matatizo lukuki na tunajitadi kupambana nayo na kwa mafaniko yanayoenda kama kobe, lakini ni nani aliyetuaminisha kwamba wizara nyingi zitahamishiwa huko?mchawi ni nani hapa??

Tunaaminishwa kila siku kwamba taifa hili ni changa na maskini, kumbe kuna watu wamejilimbikizia mimali/mipesa mingi ya kuweza kuilisha nchi ya burundi kwa zaidi ya miaka 8, can u imagine this?? sasa hii ya dodoma ni kweli au changa la macho?? Wabunge sasa hivi wapo mjengoni, hakuna hata anayethubutu kuuliza kuhusu dodoma, why??

Ngoja ni-hit point!! Hivi inaingia akilini mawaziri, wabunge na viongozi wengine kuhamisha familia zao toka daslam kwenda kuishi dodoma?? Agenda ya kuhamisha wizara kwenda dodoma ipo miaka na miaka lakini hakuna kinachofanyika..ni siasa tu!! Ardhi ipo, climate nzuri, infrastructure bora, lakini kwanini hii kitu ni sumu hata kwa viongozi wetu kuona kwamba dodoma inakuwa replacement daslam??nani anajua siri ya hii kitu kugonga mwamba??naamini kuna wabunge/mawaziri wengine tangu wapo kindegaten walisoma hii kitu, lakini wapi, siasa bana!! Sijui kwanini kuhamia dodoma kwa viongozi wetu imekuwa 'inshu ngumu' hivyo! Miaka nenda rudi sasa imekuwa kama alfu-lela-ulela, ni mambo ya kufikirika tu!!

Hivi inawezekana ugumu wa kuhamisha makao kwenda dodoma ni kwasababu ya starehe za daslam??inawezekana!! maraha yote ya daslamu nani aende dodoma??ndio kusema ile lunch ya Movenpick, New Africa Hotel, Kempisky na kwingineko ndiyo kusema is over??aagh hapana bana hatuwezi kuhamisha makao dodoma asilani!! Can u imagine, mbunge siku zote utamwona bungeni lakini malazi yake yapo daslam daily!! Kunani dodoma jamani??Twende kule ndio kusema ni mwisho wa kupigwa na kipupwe cha bahari nzuri ya Hindi hapa daslam?? Nikapigwe vumbi jekundu dodoma??Nikipata mafua nikatibiwe dodoma hospital??niende huko niwafate akina Matonya?? Big No.

Hivi vitu vyote,ugumu wote hapa daslam, msongamano, ajali nyigi, joto kupanda kwa sana, mvua haba, polution, population na mengineyo ni matokeo/zao ya serikali yetu kukaa zaidi kisiasa badala ya kihalisia/kifikra/kiutendaji!! Huko mikoani hakuna kinachofanyika. Hii ni nchi gani bana??Hivi kuna ugumu gani kwa mfano balozi za Malawi, Mozambique, South Afrika,Shelisheli n.k zisiwe Mtwara na Lindi?? Balozi za Kenya, Ethipoia, Rwanda nk zisiwe Mwanza??Balozi za Congo , Zambia nk zisiwe Mbeya n.k? Kwanini??

Hembu angalia barua za mkopo kwa wanafunzi lazima uje daslam, ukitaka visa lazima uje daslam, malipo ya wazee EAU daslam, kusafiri nje ya nchi lazima uje daslam,bidhaa flani-daslam, saloon za nywele-daslam,maombi ya chuo-daslam, maombi ya kazi daslam...jamani dodoma patakalika kweli?? Jamani Daslam sasahivi ndio Tanzania..hahaaaa!!nani anapenda kukaa bush bana??? Sasa ukiwauliza wanasiasa/viongozi hembu angalia majibu yao mepesi...''tunasubiria zijengwe ofisi kwanza''..hivi tatizo ni ardhi au fedha??cha kushangaza hata hapa Daslam kuna wizara na ofisi nyingi tu ni za kupanga.
Serikali haijajenga ofisi zote hapa daslam. Viongozi wanamiss kweli raha za jiji.

Ushauri wangu ni kwamba ujenzi wa kumbi za starehe uanze mara moja kabla hawajafikiria kuanzisha ujenzi wa wizara mbalimbali-zijengwe kumbi nyingi za starehe., club nyingi za usiku, migahawa ya 3, 4 na 5 star, madanguro na vinginevyo vingi, baada ya hapo nadhani wabunge wote watakuwa radhi kuhamia dodoma!! na kama hili halitekelezi basi hii kauli kwamba wizara zitahamishiwa dodoma ifutwe mara moja!!

Tuchangie hoja...Jioni njema!!
 
Kivyangu hizo hela naona ni kidogo sana, inawezekana wanachimba mahandaki ya kupitia chini ya baharini ili kujiepusha na gharika linalowangojea.
 
Suzan Lymo amesema kuwa matengenezo ya ikulu yamegharimu shilingi bilioni 53, na mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 10. Je matengenezo hayo ni yepi?

Kwa maoni yangu huu ni ufisadi mwingine wa hali ya juu ambao CAG inabidi aukague na kuuanika hadharani.
 
kwani hujaona matengenezo?ikulu imepakwa rangi kwa aliyepita maeneo ya ikulu anaweza kushudia hili.Labda aulize Value for Money.
Rangi yA ukuta ya bilioni 10 NI RANGI GANI?...Labda mnambia hiyo rangi ni ANTI-BALLISTIC MISSILLE!
 
Suzan Lymo amesema kuwa matengenezo ya ikulu yamegharimu shilingi bilioni 53, na mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 10. Je matengenezo hayo ni yepi?

Hapo ukifanya tathimini ya kisayansi utagundua zimetumika bil 1.3 kihalali lakini hizo zingine zimeishia kwa wajanja wanafikiri kwa kutumia tumbo
 
Kwa kweli huu ni ufisadi mwingine yaani kila mwaka mabilion kila mwaka kwa ukarabati!!!! Umeona wapi hiyo ingekuwa ujenzi tungeelewa lkn rangi?? Tunaomba CAG akakague au lkulu CAG haingiiii??? Na hilo bunge kwa nini linakubali kupiticsha fedha hizi?????
 
Kwa kweli huu ni ufisadi mwingine yaani kila mwaka mabilion kila mwaka kwa ukarabati!!!! Umeona wapi hiyo ingekuwa ujenzi tungeelewa lkn rangi?? Tunaomba CAG akakague au lkulu CAG haingiiii??? Na hilo bunge kwa nini linakubali kupiticsha fedha hizi?????
Wabunge wote wa ccm wanafuata maagizo ya mwenyekiti wao,au humuoni Makinda anavyowafanyia wapinzani bungeni?Bado miaka minne uvumilivu inatakiwa
 
Imekuwa ni kawaida ya ikulu kukarabatiwa kila mwaka kwa mabilioni ya shilingi, wandugu hebu tuambieni huo ukarabati wa mabilioni, wanajenga ukuta au vipi?
shule na nyumba za askari hazikarabatiwi.

kama tukisave matumizi ya ukarabati wa ikulu tunaweza kuongeza fedha hizo katika uzalishaji wa umeme kwa kuwekeza katika uhifadhi wa mazingira na ukarabati wa miundo mbinu chakavu, kuongeza kina cha bwawa la mtera.

Je CAG ameshawasilisha matumizi ya hizo fedha za ikulu? Mheshimiwa zito wa kamati ya fedha ripoti ya ukaguzi wa fedha za ukarabati wa ikulu iko wapi?

Je gharama ya kujenga ikulu nyingine itakuwa bei gani??hasa Pale Dodoma ambapo mkulu anatakiwa ahamie.
 
Ndugu zangu neno 'ukarabati' kwa wanaojua kiswahili lina maana nyingi!Naanza na labda wanaupdated mitambo ya kiusalama wa kisayansi au labda wanaupdate mitambo ya kisayansi ya giza!Au labda kale ka ugonjwa ketu kakubadili fenicha each year?Labda ni projeck ya watu flani?Labda kanasaidia ule mle mradi wa WaMa usiupata fungu kutoka selikari kuu?Hizi zote ni labda tu ndugu zangu wala hazina ukweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom