Rais Magufuli afanya mazungumzo na Bilionea Dangote

Kwahiyo waziri atakuwa nahisika na ile deal maana kila mara alikuwa anakuja na kauli tofauti , au alikuwa hajafanya uchamnuzi yakinifu
 
Dangote angeondoka angeleta damage kubwa sana kwa kuwaogopesha wawekezaji wengine kuja, maana ingeonekana nchi yetu haina mazingira mazuri ya kiuwekezaji, pia ingekuwa hasara kwa Watanzania wote, kiwanda kile ni muhimu kunyanyua uchumi wa kusini na the rest of Tanzania, heko Rais kulimaliza hili swala na kuwa na muafaka kwa mstakabali wa uwekezaji kwa nchi yetu.
 
Mkuu hizo details ni muhimu kuwekwa hadharani lakini jamaa kaamua kuzungumza juu juu tu bila kujali kauli mbali mbali zilizokinzana toka kwa Mawaziri wake na TPDC. Bado hawaheshimu haki ya Watanzania ya kujua nini hasa kilichojiri na nini dangote kaahidiwa toka Serikalini ili kufungua tena mitambo yake.
hhahaha naona umenywea
 
Mkuu hizo details ni muhimu kuwekwa hadharani lakini jamaa kaamua kuzungumza juu juu tu bila kujali kauli mbali mbali zilizokinzana toka kwa Mawaziri wake na TPDC. Bado hawaheshimu haki ya Watanzania ya kujua nini hasa kilichojiri na nini dangote kaahidiwa toka Serikalini ili kufungua tena mitambo yake.
ameahidiwa gesi bure, na wewe fungua kiwanda upewe gesi bure
 
Nadhani mh rais amewamaliza wale jamaa wawili waliokuwa mstari wa mbele kutukana kuwa ati Dangote alitaka gas ya bure. Mpaka yule mmoja kaenda kutafuta watu akiwasema ati ni kutoka viwanda wazalendo wa nchi hii.
Kumbe leo mh rais katufungua macho kuwa ile ilikuwa "Dili". Jamani halaf mnasema ati UKAWA ndio wataumia. Huku Ntwara, UKAWA wamepata lini hilo likiwanja la kumuuzia Dangote kwa mabilioni hayo?? Mnyonge anyongwe mchana lakini haki stahiki apewe tuu jameni.
Ndio alitaka gesi ya bure,
Wapiga dili ambao waliona dili linaruka na ambao ndio wasemaji wa dangote waliona bora tufe wote kwa kutoa habari potofu kwa selikali kuhusu gesi.
Wao waliitaka gesi kwa free kwa kigezo cha uwekezaji na kwenda kumuuzia Dangote.
 
Kuna watu kuanzia tpdc hadi biashara na nishati na madini watakosa kazi.

Maafisa wa wenye dhamana ya kusimamia masuala ya uwekezaji, viwanda na biashara na wizara ya nishati na madini hasa hasa TPDC kundi hilo ndilo linajifanya Miungu wadogo - wanaleta mizengwe mingi wakiwa na lengo la kulipwa chochote, wamekwisha lemaa hawajali hatma ya Taifa letu.

Kinacho takiwa hivi sasa ni JPJM kufanya mabadiriko makubwa katika Wizara ya nishati na madini, Wizara ya biashara na infact katika Wizara ya Biashara asifanye makosa ku appoint tena watu ambao waliwahi kuwa karibu sana na wafanya biashara au kuajiliwa nao, Rais akumbuke kwamba watawatumia hao hao kukwamisha wawekezaji wenye kuleta ushindani kwa marafiki wao ambao ni wafanya biashara wa ndani, narudia kuinsist kwamba JPJM awe makini sana otherwise masuala ya viwanda itabaki ni ndoto tu - wafanya biashara wengi wanataka kuendelea ku-import bidhaa na vyakula sio kujenga viwanda, mfano mzuri ni viwanda vya Sukari, bila Serikali kulivalia njuga suala hili wafanya biashara wa ndani watahakikisha viwanda vya Sukari havijengwi nchini.

Dangote ndiye anaweza kuwa na nia thabiti ya kujenga viwanda vya maana vya Sukari kama Serikali itamkingia kifua asipigwe vita katika kujenga viwanda vingine vya Saruji na viwanda vya Sukari, majamaa wetu wa ndani wengine wanafanya vitu ki ma-mafia mafia kweli kweli, hawataki wawekezaji wakubwa kutoka nje, suala la Dangote is just a tip of an iceberg.
 
Hadi Dangote amelazimika kuja, maana yake kulikuwa na matatizo makubwa kuliko tunachoambiwa...

[HASHTAG]#PombeSiyoChai[/HASHTAG]....Drink Responsibly!
 
Sasa kama hapakuwa na tatizo lolote, Mwijage na Muhongo mbona walifura sana kwenye vyombo vya habari?

Halafu rais anaposema kwamba kuna watu walitaka kujinufaisha binafsi, hao watu wamechukuliwa hatua gani mpaka sasa? I bet my life, hao watu ni wa CCM. Hapa ndipo ninapomwona rais kuwa ni mfanya maigizo kwenye suala la kupambana na rushwa. He ain't serious at all!
 
Back
Top Bottom