Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 65 ya watanzania walio masikini wa kutupwa, ni wakulima waishio vijijini. Aidha tafiti zinaonyesha kwamba masikini hao mara kwa mara huwa wakilazimishwa kuchangia miradi ya maendeleo kwa viwango vinavyozidi vyanzo vyao vya mapato. Chukua mfano wa hizi shule za kata, ambazo serikali ya awamu ya nne inajivunia; huku Kagera, kwa viwango vilivyokuwa vimewekwa, familia masikini zililazimishwa kuchangia hadi asilimia 80 ya pato lake la mwaka kifedha. Swali langu ni je kuna chombo chochote katika jamhuri hii kinachowakilisha wakulima? Na kama kipo mbona sauti yake haisikiki? Naomba majibu kutoka kwa wana JF