Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,288
- 9,923
Ni kweli mafanikio katika maisha yako mengi. Ahsante kwa kuwa katika hili wewe umekuwa specific na ume focus kwenye utajiri na nahisi ni utajiri wa mali.
Utajiri wa mali ni relative term. Hakuna distinct line ya utajiri na umaskini na wala kipimo cha utajiri wa mali si kimoja. Utajiri wa mali unategemea sana na vision ya mtu katika maisha. Unahitaji uwe na nini ili uone kwamba uko satisfied kiasi kwamba sasa huna hitaji litakalokusumbua kulikidhi.
Mtu mmoja akipata nyumba yenye sakafu ya marumaru na choo cha maji ndani, na gari dogo na tractor la kulimia, huyo mtu hahitaji zaidi na atajulikana hata tabia zake zilizofichika. Wakati huo huo mtu mwingine ana miliki estates za mansions na ana boats, na ndege, bado anahitaji kumiliki visiwa katika kila continent na ikiwezekana hata afuge na viumbe wanaoishi katika sayari zingine.
Wakati hayo yote yanaweza kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na jitihada ama fursa anazobahatika mtu kuzipata, bado zinahitaji kuunganishwa na uwezo wa mazingira yake ili ziweze kuleta satisfaction. Kunahitajika conducive macro na micro environments kama vile political stability, responsive social and economic policies, supportive ecological and geographical conditions.
Ni kweli umri kama miaka inanafasi yake katika uwezo wa mtu ku pursue life visions lakini miaka arobani siyo kigezo. Inahitajika mtu awe na afya njema ya mwili, akili, nafsi na roho kitu ambacho kinamahitaji yake mengine zaidi ya miaka ya kuishi.
Mtu wa miaka sitini akiwa na positive mental, spiritual and physical health anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kufacilitate mafanikio ya malengo yake zaidi ya kijana mwenye miaka 30 ambaye ana ill health. Lakini pia anaweza ku-recover katika umri mkubwa zaidi ya 40 na akafanya zaidi ya muda wake wa utoto.
Kwa hiyo kijana usiogope umri. Fanya mambo yako kwa malengo na speed ndiyo huku ukilinda na kutunza afya yako. Lakini pia, chagua CDM itakayokujengea mazingira sahihi ya kufanikisha malengo yako. Na si ccm inayodumaza kwa huduma mbovu na udanganyifu.
Tuko pamoja.
Like from Kurunzi.