Ijue Nehushtani, nyoka wa shaba aliyeabudiwa na Israeli

Shemasi acha kupotosha umma!! Musa hakutengeneza nyoka wa shamba.labda kama biblia yako ni tofauti na biblia zingine! hivi ukikutana na mutu ambae hajasoma biblia suataamini Musa ndie aliyetengeneza nyoka wa shamba..

Kama huna elimu ya kutosha kuhusu mambo haya, uliza kwa wanaojua.
Hebu tuambie nani alitengeneza nyoka wa Shaba ili tuondokane na huu upotoshaji wa Shemasi
 
Labda wewe nadhani hujaisoma biblia Vizuri!
Na Sio nyoka wa shamba Ni nyoka wa Shaba

Kasome andiko hili:

Hes 21:8-32 SUV​

Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi..............................
Shemasi acha kupotosha umma!! Musa hakutengeneza nyoka wa shamba.labda kama biblia yako ni tofauti na biblia zingine! hivi ukikutana na mutu ambae hajasoma biblia suataamini Musa ndie aliyetengeneza nyoka wa shamba..

Kama huna elimu ya kutosha kuhusu mambo haya, uliza kwa wanaojua
 
Shemasi acha kupotosha umma!! Musa hakutengeneza nyoka wa shamba.labda kama biblia yako ni tofauti na biblia zingine! hivi ukikutana na mutu ambae hajasoma biblia suataamini Musa ndie aliyetengeneza nyoka wa shamba..

Kama huna elimu ya kutosha kuhusu mambo haya, uliza kwa wanaojua.
vema ungeweka unachokijua.
 
Wafilipi 2 : 10 - 11 " Kwa ajili ya jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu "
Kwanini haipo specific kwamba yesu ni Mungu badala yake inakuwa yesu ni bwana
 
Ukiona mtu anasema Yesu ni Mungu ujue dini kaijulia ukubwani.
Kwa mtu aliyefunzwa Maandiko matakatifu kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka kitabu Cha ufunuo Kwa Biblia ya vitabu 66 hawezi sema Yesu ni Mungu.

Nitaanzisha Uzi ili kuweka mjadala huru ili Kuwafunza watu waliochelewa kujifunza maandiko na bado hawajahitimu Mafunzo lakini wanajadili ishu complicated kama hiyo ya Yesu kuwa ni Mungu.
Yesu anauungu lakini sio MUNGU Mkuu.

Hata wewe unaweza kuwa na uungu ndani yako lakini kamwe huwezi kuwa Mungu
Pepo shindwa kwa jina la YESU.

YESU ni MUNGU na hakika tunaona ukuu wake kwa kila ombi lililohusisha jina lake na hata kwa damu yake.

Kwanini majini/mapepo, wachawi, walozi, wanga, waganga wa kienyeji, mizimu huogopa sana jina la YESU (MUNGU)?

Kwanini kupitia jina la YESU ushindi upatikane dhidi ya jaribu lolote ikiwa si MUNGU?

Kwanini ukiomba kwa majina ya Manabii kama Yakobo, Daudi au Ibrahim hujibiwi isipokuwa kwa jina la YESU pekee?



Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini haipo specific kwamba yesu ni Mungu badala yake inakuwa yesu ni bwana
Unaweza kurejea chapisho langu halo awali? Kama ndio BASI fanya hivyo!

Yn 1:1-14 SUV​

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu
 
Kwanini haipo specific kwamba yesu ni Mungu badala yake inakuwa yesu ni bwana
Yohana 1 : 1 - 4 "

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. "
 
Unaweza kurejea chapisho langu halo awali? Kama ndio BASI fanya hivyo!

Yn 1:1-14 SUV​

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu
Muongezee na Tito 2:13
 
View attachment 2404825View attachment 2404827

IJUE NEHUSHTANI, NYOKA WA SHABA ALIYEABUDIWA NA ISRAELI.

Joka la Shaba alilitengeneza Musa jangwani na kugeuka kuwa mungu wa Israeli.

Na Shemasi Jimmy 0659 611 252

Bwana Yesu apewe sifa wapendwa. Ikiwa ni siku njema Bwana ametupa kibali cha kuiona siku hii ya leo, si kwa sababu sisi ni wema sana au wakamilifu bali ni kwa neema tu, ilikwamba tumrudishie sifa na utukufu kwa kufanya mapenzi yake.

Leo Bwana ameniongoza tujifunze habari ya nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa jangwani na baadae kuabudiwa na waisraeli baada ya kufika katika nchi ya ahadi..

KUMBUKA:Jina la nyoka aliyetengenezwa na Musa jangwani, aliitwa ‘’NYOKA WA SHABA’’.

Baada ya waisraeli kufika kanaani walianza kuitumia sanamu hiyo ya nyoka wa shaba kwa siri kama mungu wao, jina la mungu huyo aliitwa ‘’NEHUSHTANI’’(2Fal 18:4)

Ni katika nyakati zile Mungu alipowaondoa wana wa Israeli kutoka katika nchi ya ugeni kama alivyohaidi mababu zao(taz Mwa 15:13). Wana wa Israeli walianza vitimbi njiani. Baadhi yao walitamani kugeuka na kurudi Misri huku wakitoa lawama za kila aina kwa Mungu na Musa.

Maandiko matakatifu yanasema wakati wana wa Israeli wakiwa jangwani kuelekea katika nchi ya maziwa na asali, walipita mlima Hori kisha bahari ya shamu huku wakiizunguka nchi ya EDOMU, baadhi yao walikosa uvumilivu na wengi wao walikata tamaa ya kuendelea na safari. Walianza kulaumu Musa na Mungu huku wakiuliza kusudi la kuwatoa Misri.

IMEANDIKWA: wakamnung'unikia Mungu na Musa, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!(Hes 21:5). Kitendo hiki kiliamsha ghadhabu ya Mungu, Mungu akatuma nyoka za moto na baadhi yao walikufa.

IMEANDIKIWA: Ndipo BWANA akapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa (Hes 21:6).

Ikiwa baada ya watu kufa kutokana na nyoka hao, Wana wa Israeli wanaamua kutubu na kujinyenyekeza kwa Mungu ili kwamba hilo tatizo liondoke katika jamii yao(taz Hes 21:7).Pamoja na makosa yao hayo, lakini Mungu anawapa nafasi nyingine ya kusahihisha makosa yao na kumrejea tena. Mungu anamwambia Musa atengeneze nyoka ya Shaba kasha aiweke juu ya mti ili kila aliyeumwa apokee uponyaji kwa kuitazama (Hes 21:8)

WAISRAELI WAABUDU NEHUSHTANI BAADA YA KUFIKA KANAANI NA KUMUACHA MUNGU:

Ikiwa baada ya Mungu kutimiza ahadi yake aliyompa Ibrahimu ya kuupa uzao wake nchi ya kanaani (taz Mwa 12:7, 15:13) . Pamoja na maonyo mengi waliyopewa wana wa Israeli na Mungu juu ya kutotengeneza sanamu na kuziabudu, watu hawa waliiacha njia ya Bwana kuenenda kinyume na maagizo yake.

IMEANDIKWA: Msijitengenezee sanamu za miungu ya uongo, msishike sanamu zao za kuchonga wala nguzo wala sanamu za mawe yaliyochongwa nchini mwenu na kuvisujudu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu (walawi 26:1 BHN).

Waliambatana na sanamu ile (kwa siri, asijue mtu) aliyoitengeneza Musa jangwani na baadhi yao walianza kuiabudu hata ulipotimia wakati wa utawala wa mfalme HEZEKEIA.

Maandiko matakatifu yanasema Hezekia alikua moja ya wafalme wema, mtiifu na mwadilifu mbele ya Mungu, alifanya mambo mengi mema na yenye kumpa Mungu utufu. Ni HEZEKIA mwana wa Ahazi aliyevunja vunja sanamu ya nyoka wa shaba ama Nuhushtani iliyotengenezwa na Musa jangwani, amabayo baadhi ya waisraeli waliitumia katika ibada zao zilizokua chukizo kuu mbele ya Mungu.

MEANDIKWA: Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya Shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani.(2 fal 18:4)

TENDO LA MUSA KUINUA NYOKA WA SHABA JANGWANI LA FANANA NA TENDO LA KRISTO KUINULIWA MSALABANI.

Nyoka wa shaba aliyeinuliwa ili kila atakae mtazama apokee uponyaji na yeyote asiyemtazama alikufa(Hes 21:8-9). Ni sawa kabisa na jinsi Bwana wetu Yesu kristo alivyoutoa mwili wake kwa kila kiumbe ili kwamba kila amtazamae na kuamini basi ataokolewa na asiyeamini atahukumiwa(marko 16:16). Niheri sasa ndugu yangu ambaye bado hujampokea kristo na kumfanya awe Bwana na mwokozi wako, fikiria sasa uamizi huu.

YEYE ANASEMA’’Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha’’(Mt 11:28). Wewe uliyepata neema ya kusoma ujumbe huu,geuka na ufikiri sasa kumfuata Yesu. Nitafte shemasi wako kwa namba hii 0659 611 252 popote ulipo tutakufikia na utapokea wokovu kwa njia ya ubatizo wa maji na roho(mdo 2:38)

Mungu akubariki wewe uliyetumia muda wako wa thamani kusoma chapisho hili. Bwana akubariki wewe na familia yako. Akubariki uingiapo na kila utokapo kwa jina la Yesu, amina
Mtume Mussa hakuwahi kutengeneza nyoka la shaka kama biblia inasema hivyo basi itakuwa hiyo biblia ni feki hizo habari za wayahudi wametunga Hizo History ili kumsingizia Nabii Mussa maneno ya uongo. Habari yako sio ya ukweli .
 
Back
Top Bottom