IGUNGA (Siasa, Uhalifu na Kura za huruma.

Aug 21, 2011
26
0
Ninaanza kwa kusimulia Kisa cha kweli kilichowahi kutokea mjini Moshi eneo la Majengo. Majambazi yalivamia Bar yakiwa na silaha za moto, yaliwalaza chini Wateja wote na kuzima taa, jambazi mmoja alitangaza kuwa yeyote atakayejaribu kunyanyuka atakutana na hii (alipiga risasi hewani) Baada ya kukamilisha wizi wao pamoja na kuwapekuwa mifukoni wateja wa bar, jambazi alitangaza tena kuwa bado niko hapa mlangoni, yeyote atakayenyanyuka atakutana na kitu hiki. (Alipiga risasi nyingine hewani.) baada ya tangazo hilo kumbe jambazi aligundisha nyuma ya mlango sigara inayowaka kwa kutumia big gee kisha akaenda zake. Hakuna mtu aliyethubutu kunyanyuka kwani kila aliyejitahidi kuchungulia anaona moto wa sigara hivyo anaamini kuwa jambazi bado yupo. Walikombolewa na Mlevi wa gongo aliyekuja kusukuma mlango na kusema Hamlipi bili mmekatiwa umeme, nipe pombe gizani. Mara nyingi sana Wahalifu wamekuwa wajanja sana, mawazo yao na utekelezaji wa uhalifu wao unakuwa mbele zaidi kuliko mawazo na vitendo vya chombo chetu cha dola (Polisi). Uhalifu unaofanyika sasa Igunga ukiacha tukio la DC unabebeshwa sura ya kisiasa, hata kama yawezekana Wahalifu wanafanya hayo kwa nia ya kulipa kisasi kwa wanayemtenda kwa chuki zao za huko nyuma ama uhalifu kama uhalifu mwingine unaofanyika sehemu mbali mbali hapa nchini. Tofauti kubwa ya Igunga ni moja. Polisi wameaminishwa na CCM kuwa wafuasi wa CHADEMA ndio wahalifu, hivyo Polisi ninaamini hawatafanya uchunguzi stahiki zaidi ya kuzunguka kwenye vilinge na vijiwe vya wafuasi wa Chadema. Kuwasumbua bila ushahidi. Kifupi, UHALIFU IGUNGA UMEGEUZWA MTAJI WA KISIASA. Hata kama uhalifu utafanywa na wana ccm kwa sababu yoyote ile, uwe wa kupanga ili kuwapaka matope Chadema ama uhalifu kama uhalifu mwingine. Ccm wamepata mtaji wa kuomba kura za huruma kwa Wana Igunga hata kama watakuwa hawana uwezo tena wa kuongoza jimbo hilo. Hiki ni kitu kibaya sana kama hayo yanayotokea Igunga yatakuwa na taswira hii. Polisi badilikeni na timizeni wajibu wenu.
 
Back
Top Bottom