IGP Wambura aagiza askari 19 washtakiwe, 8 wasipewe vyeo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP) Camillus Wambura, ameagiza askari wanane wasipewe vyeo vya kijeshi, huku akiamuru askari wengine 19 walioachishwa mafunzo baada ya kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, washtakiwe na adhabu stahiki zitolewe kwa mujibu wa sheria.

Alitoa maagizo hayo jana katika Kambi ya Kambapori iliyoko West Kilimanjaro, wilaya ya Siha, wakati wa kufunga mafunzo ya uongozi mdogo jeshini, ngazi ya sajini meja na koplo, iliyowajumuisha zaidi ya askari 2,200. Mafunzo hayo ya miezi mitatu yalianza Februari 13, mwaka huu.
IGP Wambura aliwakilishwa na Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu katika Jeshi hilo Kamshna Susan Kaganda.

"Nimepokea ombi hilo la Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania (TPS) na ninawapa fursa ya kurudia mitihani wanafunzi 11 waliokosa kufikia ufaulu masomo ya darasani lakini wana sifa za uongozi.

"Nimeridhia kwamba ndani ya wiki moja, wanafunzi hao 11 wapewe mitihani na ninawakumbusha walimu kwa yeyote ambaye hatafanya vizuri, basi asipewe cheo. "Pia naelekeza kwa wale wanafunzi watatu, ombi la kutowapa cheo wamefeli na hawana sifa za uongozi , Sambamba na wanafunzi watano waliofaulu, lakini hawana sifa za uongozi, naridhia wasipewe cheo na wale wenye vitendo vya utovu wa nidhamu, washtakiwe na adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria zitolewe," alisema.
 
Nidhamu kwanza Asante IGP
 
Jambo afwande timamu...
 
Back
Top Bottom