IGP: Sababu halisi za tatizo sugu la Foleni Dar es Salaam hizi hapa. Chukua hatua!

namtumbo

Member
Aug 30, 2011
78
102

Kama kuna jambo moja linalowasononesha wananachi wa Dar es salam kila siku, ni muda mwingi wanaoupoteza barabarani kutokana na foleni zisizoisha. Foleni zina athari kubwa kwa uchumi wa Dar es salaam kwani watu wanapoteza muda wa uzalishaji barabarani na kuchoma mafuta ambayo yangetumika kwenye shughuli nyingine za kuleta tija.

Jambo muhimu la kuzingatia ni kwamba huko nyuma tatizo la foleni lilikuwepo nyakati za asubuhi na jioni- muda ambao watu wengi wanaingia na kutoka jijini. Lakini Siku hizi foleni ni kubwa muda wote, bila kujali ni asubuhi, mchana au jioni.

Lipo jambo lingine muhimu kulizingatia. Zipo siku foleni inakuwa kubwa, na zipo siku foleni ni ya kawaida. Swali ni je inakuwaje- idadi ile ile ya magari, siku ngingine isababishe foleni kubwa na siku nyingine hakuna?

Tatizo
Nimefanya utafiti kidogo kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Kwenye barabara ile, foleni inakuwa kubwa: saa 12 na dakika 20, saa moja kasorobo; Saa moja na nusu; na saa 2 kasorobo hadi saa 3 kasoro. Patern hii inakuwa influenced na muda wa kuanza shughuli kwenye ofisi za serikali ambao ni saa moja na nusu; muda wa kufungua mabenki na muda wa kufungua maduka kati ya saa mbili asubuhi hadi saa 3 asubuhi.

Patern hiyo ndio ina determine muda upi foleni inaongezeka na muda upi inapungua.

Hata hivyo zipo factors nyingine ambazo zinaweza ku affect foleni kwenye baranara ile ya Ali Hassan Mwinyi
E kama vile:
1) Misafara ya viongozi wakuu wa kitaifa wanaotumia barabara ile asubuhi wakiwepo Dar es Salaam-Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Marais wastaafu wa awamu ya pili na tatu

2) Movement za magari ya kubebea wagonjwa

Hizi factors mbili nazo zimekuwepo muda mrefu na hazijawahi kuwa tatizo sana kwasababu sio kila siku kuna ambulance kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi, na vilevile viongozi wa kitaifa mara nyingi wanakuwa nje ya Dar es Salaam na hata wanapokuwepo Dar...wanaoratibu movement zao, wanajitahidi sana ku avoid zisifanyike wakati wa rush hour (vipindi vyenye magari mengi barabarani) ili kuepuka usumbufu kwa wananchi na sababu za kiusalama pia.

Kwanini sasa foleni imeongezeka?
Wapo wanaosema kwamba ongezeko la foleni limetokana na wingi wa magari mjini. Wakati sababu hii ina ukweli, lakini bado zipo sababu nyinginezo zinazoongeza tatizo juu ya tatizo.

Sababu kubwa No 1 utaratibu wa kuongoza magari kwa kutumia TRAFIKI badala ya taa za barabarani. Wiki hii kwa mfano, kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Morocco hadi junction ya St Peters hakuna foleni kabisa kwasababu taa ndizo zinaongoza magari. Kipande cha kuanzia DSTV na kuendelea ndio foleni imekuwa sugu kwasababu ya matrafiki kuongoza magari kwenye makutano ya sallender.

Kitendo cha kuamua kuacha kutumia traffic lights na kutumia matrafiki....ni sawa na Mkulima aliyeamua kuacha kulima kwa kutumia trekta na kurejea kwenye jembe la mkono. Kwa vyovyote vile ile human element katika kucontrol traffic itakuwa na mapungufu na inakuwa influenced na so many other factors kama vile trafiki yule ameamkaje, ana mood gani? Afya yake ikoje siku hiyo etc Yapo maneno yanayozungumzwa kwamba siku hizi kuna baadhi ya watu wana utaratibu wa kuwapa fedha matrafiki ili wakiwa kwenye foleni wanawapigia simu ili wafanye movement ya magari kwenye barabara waliopo iongezeke ili wawahi wanapokwenda. Nasikia ni shilingi 100,000 tu kwa mwezi, waweza kupata huduma hiyo. Je unadhani traffic lights zingetumika, tatizo la aina hiyo lingekuwepo?

Trafiki wana hoja kwamba taa za barabarani zinachelewesha flow of traffic...ndio maana wao wana intervene. Lakini nijuavyo mimi, zipo taa za barabarani ambazo unaweza kuziprogramme muda gani unataka ziruhusu flow of traffic....

Sababu no 2: Ongezeko la misafara inayoongozwa na matrafiki (nje ya ile misafara ya viongozi wa kitaifa). Hapa kuna makundi manne hivi.

Kundi la kwanza
Kuna wakuu wa taasisi ambao zamani hawakuwa na privillege ya kusafishiwa njia, lakini siku hizi utaona nao wanapewa service hiyo. Mfano IGP, Spika, Mkuu wa Majeshi, Jaji Mkuu n.k) Ni muhimu ikajulikana ni viongozi gani wapo entitled kupata huduma hiyo na kwa wakati gani. Pia ni muhimu kujfunza kutoka kwa nchi za wenzetu......ni akina nani wanapewa huduma hiyo. Zipo nchi, hata Rais wa nchi nyingine akienda kwao,hawampi huduma hiyo.

Kundi la pili: umekuwepo utaratibu wa waheshimiwa wabunge wanapokwenda kwenye majukumu ya kutembelea maeneo mbalimbali nao kupewa huduma hiyo.
Katika kundi hili wapo pia baadhi ya Mawaziri ambao kutokana na kutokuwa na mpagilio mzuri wa muda katika ratiba zao, huchelewa kwenda wanapotakiwa na mwishowe wanaomba kusindikizwa na police rider.

Kundi la tatu: wageni kutoka nje ya nchi. Hili kundi nalo zamani tulizoea kuona wageni wanaopewa huduma hiyo ni viongozi wakuu wa nchi husika au wawakilishi wao wanapokuja Tanzania. Lakini siku hizi, hata Mkurugenzi Serikalini ilimradi ametoka ugenini unaweza kukuta anademand na kupewa huduma hiyo. Tumefika mahala hata viongozi wa makampuni binafsi wanapokuja nchini wanademand na kupewa police escort...(ridder). Mara nyingi tabia hii imejengeka sana kwa wageni kutoka China.

Kundi la nne: siku hizi pia, haukawii kukuta kuna msafara wa kusindikiza msiba. Ilimradi mfiwa ni mtu anayejulikana, anaweza kuomba huduma hiyo, akapewa.

Hii yote ni confussion ambayo kwa ujumla wake ndio inayosababisha foleni zisizoelezeka na kueleweka kuongezeka mjini Dar es salaam. Hivyo, hatua hazinabudi kuchukuliwa kupata solution ya tatizo hilo.

Hatua za kuchukua ni pamoja na:

1) Kusitisha matrafiki kuelekeza magari.....badala yake Taa za barabarani zitumike

2) Ziwekwe taa za kisasa za kuongozea magari katika zile junction kubwakama salender, Ubungo, Tazara, Chang'ombe, Kamata, Serena, Morocco, Mwenge. Taa hizo ziwe na uwezo wa kuwa programmed kuruhusu flow of traffic kwa kuzingatia muda wa magari mengi na magari machache

3) Sheria/taratibu kuhusu wanaostahili kupewa huduma ya msafara ifuatwe. Huduma ya kusafishiwa njia iishie kwa viongozi wakuu wa kitaifa yaani Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Makamu wa kwanza na wa pili wa Rais wa Zanzibar. Pia kwa wageni wanaotoka nje ya nchi, huduma hiyo itolewe kwa Wakuu wa Nchi au wawakilishi wao pekee.

4) Barabara za pembezoni zitengenezwe ili kupunguza idadi ya watumiaji wa njia kuu

5) Trafiki wafanye kazi yao ipasavyo ya kuwakamata na kuwachukulia hatua kali wale wote wasiofuata sheria za barabarani ambao kwa kiasi kikubwa nao wanachangia tatizo la msongamano usio wa lazima.

Kwa kuchukua hatua hizi ninaamini tutapunguza msongmano usio wa lazima wa magari jijini hata kabla ya kuingia kwenye mipango ya kujenga flyovers (barabara za juu).

Moja ya mambo yanayowakera wakazi wa Dar kupita kiasi, ni foleni za magari kwenye jiji hilo.

Siyo ajabu kabisa kwenye jiji hilo, kwa wakazi wake kutumia hadi masaa mawili au matatu wakati wanapokwenda kwenye shughuli zao katikati ya jiji, na kutumia muda huo huo wakati wa kurudi jioni.

Kwenye jiji ambalo inakadiriwa ndilo linalobeba asilimia 80 ya uchumi wa nhi hii, tafsiri yake ni kuwa, kila siku Taifa linapata hasara ya mabilioni ya shilingi kutokana na foleni hizo.

Hata huu uporomokaji wa kasi wa shilingi yetu ya Tanzania, unaweza kabisa kuhusishwa na kuporomoka kwa uchumi wa jiji hilo, kutokana na foleni hizo za kutisha za magari.

Wanasiasa wetu wamekuwa wakitoa ahadi za mara kwa mara kuondoa tatizo hilo, lakini hawaonekani kama wamedhamiria na wana nia ya dhati ya kuondoa tatizo hilo.

Nimetangulia kusema kuwa wanasiasa wetu hawaelekei kuwa na dhamira na nia ya dhati ya kuondoa tatizo hilo kwa kuwa niaminivyo mimi, utatuzi wa tatizo hilo ni wa kisera zaidi kuliko kufikiria misaada ya mabilioni ya dola kutoka kwa nchi wafadhili.

Ukiangalia undani wa tatizo la foleni jijini Dar, unatokana zaidi na ongezeko la magari yanayotembea kwenye jiji hilo ambalo hayaendani sambamba na upanuzi wa miundombinu ya Jiji hilo.

Kutokana na hali hiyo kama watawala wetu wanalijua hilo, ni kwa nini basi wanashindwa kutengeneza sera ya kuimarisha usafiri wa uma, ambapo ukiimarishwa usafiri huo wa uma, wakazi wengi wa Jiji hilo wataacha kutumia magari yao binafsi na watatumia usafiri huo wa Public?

Hebu tujiulize swali moja tu la msingi, hivi inakuwaje wananchi wengi kwenye miji mikubwa ya nchi zinazotufadhili, kwa mfano nchi za Scandinavia wanatumia usafiri wa uma, wakati sisi wananchi masikini tunaopewa misaada hiyo tunaamua kujitanua kwa anasa ya kila mtu kutaka kuliingiza gari lake barabarani?

Kulithibitisha hilo la magari binafsi kuwa ndiyo yanayosababisha foleni ya 'kufa mtu' hapa jijini, ilionekana wakati wa mgomo wa daladala ambapo wakazi wa jiji hilo, walitumia hadi masaa 6 kufika makwao, kama vile Tegeta, Mbezi ya Kimara, Gongo la Mboto au Mbagala, wakiwa wanatoka kwenye shughuli zao katikati ya Jiji!

Nimesema suala la kumaliza foleni ya magari jijini Dar limekaa kisera zaidi kuliko kudhani kwamba kwa kutumia mabilioni ya shilingi kama kwenye miradi ya BRT ndiko kunakoweza kumaliza tatizo hilo sugu.

Hebu tuwaulize watawala wetu ambao ndiyo watunga sera, hivi wanashindwa nini ku-introduce mfumo wa usafiri wa uma, ambao utacategorize usafiri wetu kwa classes?

Kwa mfano class moja iwe na mabasi ya kawaida kama yaliyopo sasa, ambayo yataendelea kujaza abiria wanavyotaka na kuendelea kutoza nauli za hivi sasa, na class nyingine iwe introduced, ambayo itakuwa na 'LUXURY BUSES' ambayo mabasi hayo yatapewa vigezo vya kuwa katika class hiyo ni lazima yawe na AC na yapakie abiria kwenye level seats, na class hiyo ya mabasi ya Luxury ipangiwe viwango tofauti vya nauli zake. Kwa mfano kutoka Mbezi ya Kimara ikawa shilingi 1,500 badala ya 600 inayotozwa na mabasi ya kawaida kwenye route hiyo.

Mbona hata kwenye mabasi ya mikoani, kuna tofauti hiyo ya madaraja, inawezaje kushindikana kwenye jiji la Dar?

Hivi mbona watu wanaokwernda Serena Hotel au Kilimanjaro Hyatt Hotel, wanaweza kunywa bia hiyo hiyo inayotengenezwa pale TBL Ilala kwa shilingi 5,000 ambapo 'uswazi' bia hiyo hiyo inanywewa kwa 2,300, na hakuna mtu yeyote anayekwenda Serena ambaye analalamikia tofauti hiyo ya bei kubwa kwa kiasi hicho?

Manufaa makubwa sana yatakayopatikana kwa kuintroduce Classes mbalimbali za usafiri wa hapa jijini ni kuwa utawadiscourage watu wengi kuingiza private cars zao barabarani na wata-opt kutumia Public Transport ili waepuke gharama, kwa kuwa pia watakuwa assured, hata kama watakuwa 'wamezitinga' suti zao, watashuka kwenye mabasi hayo wakiwa bado wasafi kabisa na hata viatu walivyovipolisha vizuri, polish hiyo ikiwa intact!

Na baada ya hatua hizo za kuimarisha Public Transport, zichukuliwe hatua za makusudi za kuwadiscourage watu wasiyaingize magari yao City centre kama hakuna ulazima sana.

Mathalani zinaweza kuwekwa check points, kwa mfano Mwenge,Ubungo,Tazara na Uhasibu ili iwatoze wale wote watakaopenda 'anasa' ya kuyaingiza magari hayo mjini.

Ninaamini watawala wetu wakiamua kisera kufanya maamuzi magumu, matatizo ya foleni Dar hata kama hayatakwisha kabisa, basi yatapungua sana, lakini kwanza itabidi mindsets za watawala wetu zibadilike na waondokane na fikra za kuwa matatizo ya foleni yatatatuliwa na wafadhili toka nje, wakiendelea kuamini hivyo, tatizo hilo litaendelea kudumu hadi mwisho wa dunia!
 
Ninakubaliana na uchambuzi wako Namtumbo,
ulichonifurahisha zaidi sio tu umeorodhesha matatizo yaliyopo, bali umemalizia kwa kutoa mapendekezo.

IGP Mwema ni mtu msikivu na mwenye kufanya mambo yake kisayansi, am sure akiupata ujumbe huu hatoupuuzia, ataufanyia kazi.

Nchi yetu ingepiga hatua kubwa kama kila mtu angeamua kufanya utafiti na kutoa solutions namna hii.

Unadhani kuwa taa za barabarani zitasaidia kupunguza foleni Dar? Think again. Tungeanza na kujibu swali la msingi kabisa, foleni hutokea namna gani? Hapa ni kutaka kujua kitendo ama jambo linalopelekea magari kukutana hata kufanya msongamano.

Tuone sababu ulizo ainisha:

1. Traffic kuongoza magari - Ingawa ni rahisi kudhani kuwa traffic police wanaleta msongamano, lakini ukweli ni tofauti kabisa. Uwepo wa traffic police unasaidia sana kupunguza machungu ya msongamano kwa vile huruhusu magari kwa kuzingatia umuhimu wa barabara wakati ule. Mfano wakati wa asubuhi magari mengi sana hupita njiapanda ya TAZARA kuekea mjini kupitia barabara ya Nyenyere. Hivyo traffic police hutumia muda mwingi zaidi kwa magari yaendayo mjini kuliko yatokayo huko. Jioni ni kinyume chake. Taa haziwezi kuamua haya. Nimeshuhudia mara nyingi tu pale traffic wasipofika wakati wa msongamano, watumiaji hukosa uvumilivu na hivyo kuendelea kupita hata kama taa zimewazuia. Matokeo yake magari hukutana kati na kufunga barabara.

2. Misafara ya VIP - Ingawa kwa kiasi fulani yaweza kuchangia msongamano, si kweli kwamba sehemu zote zilizo na msongamano zina pitiwa na misafara hiyo. Mfano tuchukulie leo misafara yote ifanywee kwa helikopta, je kutakuwpo na unafuu katika msongamano (kuokoa muda)? Si rahisi kuona tofauti yoyote.

Mpaka hapo bado hatuwezi kukwepa tatizo la ufinyu wa barabara. Halafu tatizo kubwa zaidi ni taa za barabarani. Kila baada ya umbali mfupi unalazimika kusimama na hapo magari kurundikana. Ndio maana fly overs hazikwepeki.Hebu fikiri kwa mfano, unatoka Gongolamboto unafika TAZARA husimami, unafika Ngozi husimami, unafika KAMATA husimami. Huoni kama foleni zingepungua sana?

Ni mawazo tu.
 
Mkuu thinking capacity yako ipo vizuri ume advanced sio kama vile mwanzo ulivyo kuja hapa jamvini
 
Tatizo juu ni barabara, haya mengine ni ziada. Kama limorogoro road si ubwabwa mtupu ule? Kwanini wasingejenga flyovers, wameacha kabarabara ambako hata gari mbili haziendi sambamba. Kesho tutabomoa tujenge flyovers Kama tunavyohangaika kutengneza biashara ya uda kwa kuwajengea Barbara. Kama umefikisha nairobi hebu icheki ile thika road na jinsi ilivyosaidia, njoooooooo na matatu,daladala, corrola,vx wote ni speed 120. Bongo tunashindwa nini?
 
Hamna kitu. Huna cha maana chochote ulichofanyia utafiti au kutoa ushauri mwafaka. Kama mtihani makisi zako hata 0% hustahili labda hasi100%.
 
Hamna kitu. Huna cha maana chochote ulichofanyia utafiti au kutoa ushauri mwafaka. Kama mtihani makisi zako hata 0% hustahili labda hasi100%.

Ambagae mimi ninadhani amepata asilimia 80 maana marking yako ndio ya mtu wa sifuri.....umetoa hukumu bila kuonyesha mapungufu ya hoja zake, au hoja mbadala ni zipi....u just jumped to crush the author bila vigezo.
i suspect wewe ni mmoja wa wale matrafiki wachache wasio waaminifu mnaotusababishia foleni mjini. Jibu hoja kaka tukusome kama mwenzio alivyojaribu kujenga hoja ambazo baadhi ninaziafiki na nyingine siziafiki pia
 
namtumbo

Nyerere alilitambua hili mapema Ndio Maana alitaka serikari ihamie Dodoma mapema lakini Wamegoma kuhamia Dodoma sasa tunabanana hapa hapa Dsm Gari za Umma ni Utitiri Gari za makampuni ni Utitri Gari za Ofisi za Barozi na mashirika ya kimataifa ni utitiri huku gari Binafsi za watumish wa Umma na wa Dini nazo zimefurika jijjini bila kusahau daladala maroli na Gari za Vimada na masharobaro tena wengi hawana Reseni nazo zipo jijini kwenye Miundombinu ile ile ya zamani ! Unategemea nini ?

Foleni haitakwisha Dsm hata ujenge barabara 200 mpya njia pekee ya kuliepusha jiji na kuwaelimisha watu waache Ubishoo wapende Public transport Kama ulaya au Wahamie Dodoma haraka iwezekanavyo hakika Gari za serikari zikihama jiji na gari Binafsi zikahama pamoja na gari za vimada ziikahama Nina uhakika jiji litapumia na foleni itapungua sana.Malawi,Nigeria,south Africa ,India wao walihamia miji Mipya baada ya kugundua miji ya Zamani ni majanga Kama ilivyo jijini Dsm sasa
 
Last edited by a moderator:
Pia huyo IGP awaambie na wakubwa wenzie wapunguze malori yao mjini kero tuuuupuuuu....mikontena..milori yamafuta...halafu yanakufa njiani mno na kusababisha foleni..mabovu..sehemu ya speed 80 yenyewe yanajikokota na 30...km vipi yatembee usiku
 
Nashauri miradi ya ujenzi mpya ihamishiwe miji mipya kando ya jiji mfano kibamba, kongowe, nk. Pia ofisi muhimu za Serikali mfano wizara, tra, na taasis zingine zihamishiwe nje ya jiji.
 
Back
Top Bottom