Ifahamu Meguro Meguro Parasitological Museum: Makumbusho ya Vimelea.

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Habarini Wakuu!

Pole kwa wagonjwa wote Mungu aendelee kuwapambania na mkapate afya njema! Kwa wale ambao wapo wazma basi Kazi iendelee.
caption.jpg
Japani ni mojawapo ya nchi zenye ustaarabu wa kale wa pekee sana na ina historia nzuri na tofauti na nchi zingine duniani. Mandhari ya kustaajabisha na tofauti yenye milima na mazingira ya kuvutia, ambayo yanathaminiwa sana na Wajapani, ila pia kuna vitu vya kushangaza sana ndani ya Japani, moja ya kitu hicho ningependa kukileta kwenu wanajukwaa.
20180522-120338-largejpg.jpg

Makumbusho kwa muda mrefu zimekuwa ni sehemu ya msingi ya maarifa na elimu duniani, zimebeba mamlaka na kufunua ukweli. Lakini mara kadhaa historia, mara nyingi zimetuonesha ukweli nusu, simulizi, au tafsiri potofu kabisa. Makumbusho zinaweza kufanya vizuri zaidi, Makumbusho zina fursa ya kusema ukweli kamili kuhusu uhalisia wa maisha yetu.

The National Science Museum, makumbusho iliyopo huko Korea Kusini ni Makumbusho ya Kisayansi ambayo inajihusisha na kuonesha uhodari na mchango mkubwa wa wanasayansi katika historia ya Korea Kusini. ukienda Marekani kuna The Exploratorium pamoja na California Science Center. Ukienda Afrika Kusini kuna Stellenbosch University Botanical Garden.

Kutoka Tokyo mpaka Meguro ni dakika 38 kwa usafiri wa gari na kwa treni ni dakika 49 tu ukitumia station ya Eifukuchō ambapo utatumia gharama ya shilingi za kitanzania 5,161 sawa na yen 300 ila kama utatumia station ya Honancho basi utalipa yen 350 sawa na shilingi 6021.25 ila ukiamua kuprint basi utatumia lisaa limoja na dakika39 kitaalamu. Ni kilomita tisa kutoka Jiji la Tokyo mpaka Meguro, jiji ambalo ndani yake kuna makumbusho ambayo ni ya kipekee sana makumbuko ambayo ukingia ndani ukiwa umekula zako makande basi utarudisha chenji kabsa.

Jumba la kumbukumbu la Meguro Parasitological Museum huko Meguro, Tokyo linatosha kulipatia hadhi ya kuwa jumba la makumbusho pekee la aina yake duniani, jumba la makumbusho linalojitolea kuonesha duniani kwa ukaribu wadudu, vimelea na viumbe wengine wanaoishi kwa kutegemea au ndani ya viumbe vingine, ikiwa ni pamoja na sisi binadamu.

Kuchunguza na kushangaa ndani ya Jumba la Makumbusho la Meguro kutakuacha ukiwa na karaha kiukweli na kuchukizwa kwa wakati mmoja. Utakutana na wanyama walioambukizwa na vimelea, yote haya yanatosha kukuvurugia siku kabsa.
47683627002_14c6dfccb5_k.jpg
Umewahi kujiuliza je ukiingia kwenye maabara ya wanasayansi wenye wazimu tena yenye hifadhi ya vitu vya ajabu itakuwaje? Meguro kuna kila aina ya mnyama ambaye amekutana na kadhia hii ya kuwa na milelea ndani yake, kuanzia panya wenye matumbo yaliyojaa, samaki walioambukizwa, na minyoo warefu na wakubwa uliowahi kuwaona. Wale wenzangu waoga usipeleke fito zako huko, nenda Meguro Sky Garden ukashangae mimea na miti tu, au uende ukatazame hekalu la Gohyaku Rakanji.
Kaihukuji_temple.jpg

Hii ni makumbusho dogo na kituo cha utafiti kilianzishwa mnamo 1953 na daktari Satoru Kamegai. Makumbusho hii ipo katika jengo ghorofa mbili, yaani kuna sehemu mbili ya makumbusho, kwanza kabsa ni chini ambapo ghorofa hii ni mahususi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wat una kuwapatia taarifa muhimu kabla hata hawajafika juu, wakiwa sehemu ya kwanza kabsa watu hupata taarifa muhimu kuhusiana na vimelea na sehemu ambazo vimelea vinaishi n ani ngumu kuvion kwa macho yetu haya. Sehemu hii huwa na vimelea vya Wanyama kwa ujumla na hutoa maelezo ya jumla.
0_xdYlW82GHRhsBL0Y.jpg
Ghorofa ya pili ndo shughuli nzima ipo huko kwani huko kunaonesha kitu ama madhara ambayo hutoea endapo vimelea wanapoingia ndani ya viumbe vya binadamu na wanyama. Ukifika ghorofa ya pili kuna Mchoro wa bot-fly ambao huu unaeleza kwa kina jinsi mdudu huyo huweka mayai yake kwenye mbu, ambao kisha huhamisha mayai hayo kwa wanadamu wanapowauma au kuwang’ata. Mabuu ya botfly hukua chini ya ngozi, yakicheza na kujikunja hadi yanakua. Pia ghorofa ya pili ni mahususi kwa ajili ya vimelea vinavyohusiana na binadamu moja kwa moja.

Jambo la ajabu na la kikatili zaidi ni mnyoo yenye urefu wa mita 8.8 (urefu wa takriban futi 29) ambayo ulitolewa kutoka kwa mwanaume mmoja baada ya kula samaki mbichi walioambukizwa miezi mitatu iliyopita. Dkt Kamegai alifanya utaratibu wa kumuondoa mnyoo huyo baada ya mwanaume huyo kugundua kitu kikining'inia kwenye puru wakati akiwa anakata gogo, ni kama vile kuna kitu kilikuwa kikichungulia nje na kurudi ndani.
tapeworm.jpg

Ili kukupa wazo bora la ukubwa na urefu wa mnyoo huyu, jumba la makumbusho la Meguro lina kipande kirefu cha kitambaa chembamba chenye urefu sawa wa minyoo inayoonyeshwa, ni Kamba ndefu kiukweli sawa na urefu wa mnyoo huyo. Sasa ebu piga hesabu kuwa mwamba anaishi ndani yako kwa muda wa miezi mitatu!

Ingawa maelezo mengi ndani ya Meguro yapo katika lugha ya Kijapani, luninga pamoja na mbao za matangazo nyingi zina msimbo wa QR ambao utaonyesha maelezo ya Kiingereza ikiwa utaamua ku-scan kwa kamera yako.
curiosita-v1-671716.jpg

Dk. Kamegai alianza kufanya mazoezi ya udaktari punde tu baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Wakati huo mifumo ya maji na mifereji ya maji taka nchini Japani ilikuwa imeharibika na watu wengi kote nchini Japani waliugua magonjwa ya vimelea, magonjwa kama vile, amebiasis, cryptosporidiosis pamoja na giardiasis na mengine mengi, huku ugonjwa wa schistosomiasis ukiwapatia wakati mgumu sana wananchi wa Japani.

Magonjwa haya yanaweza kusababisha upungufu wa damu na upofu kwa watu wengi, pia unachangia kwa ukaribu kudumaza ukuaji wa watoto, mfano kwa ugonjwa wa toxoplasmosis ambao huu unasababisha matatizo ya kiakili, pamoja na kuharibika kwa mimba, na kusababisha maelfu ya vifo kila mwaka. Na sio kawaida kwa watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri kuteseka zaidi ya moja ya magonjwa haya kwa wakati mmoja, na kuathiri uwezo wao wa kwenda shule au kutafuta riziki ama kipato.
FATA50_Japan.jpg

Dkt. Kamegai alivutiwa na ulimwengu wa ajabu wa vimelea na kuanza kuwakusanya vimelea mbalimbali kutoka kwa wagonjwa wake. Mnamo 1953, alifungua jumba la kumbukumbu ndogo ili kuonyesha matokeo yake na kuongeza ufahamu wa viumbe hawa na kulipatia jina la Meguro Parasitological Museum. Dkt. Kamegai aliaga dunia mwaka wa 2002, lakini jumba hilo la makumbusho limeendelea kufanya kazi kama kituo cha kibinafsi cha utafiti na elimu ya vimelea.
curiosita-v1-671716.jpg

Leo, jumba hili la makumbusho lina mkusanyiko wa vimelea zaidi ya 60,000 tofauti, karibu 300 ambavyo vinaonyeshwa kwenye mkusanyiko wa maonyesho ndani ya makumbusho katika safu ya mwanzo kabsa. Kuingia ndani ya jumba la makumbusho ni bure huku kukiwa na duka la zawadi na fulana zenye mada ya vimelea, kalamu na vito vya thamani. Makumbusho hii inaendeshwa kwa michango ya hiari kutoka kwa wadau wa masuala ya afya na vituo vingine vya kiutafiti chini ya usimamizi wa MtaalamuToshiaki Kuramochi.
Karibuni sana Meguro Parasitological Museum.
 

Attachments

  • 公式サイト用パンフレット.pdf
    1.1 MB · Views: 1
  • 46820751355_3746414240_k.jpg
    46820751355_3746414240_k.jpg
    304.9 KB · Views: 3
Haya yalikuwa mambo yakina Dr.Zul Premji, sijui kama bado yuko hai. Kazi nzuri sana hizi kwa wenye mapenzi ya Parasitology and Entomologist. Ila ni ajabu kwamba ni mtu binafsi kaweza kufanya haya, huku kwetu hata,serikali inashindwa.
 
Haya yalikuwa mambo yakina Dr.Zul Premji, sijui kama bado yuko hai. Kazi nzuri sana hizi kwa wenye mapenzi ya Parasitology and Entomologist. Ila ni ajabu kwamba ni mtu binafsi kaweza kufanya haya, huku kwetu hata,serikali inashindwa.
Serikali inashindwa na haiwezi! Pia mleta uzi ninaomba picha za hao panya wenye vitambi.
 
Haya yalikuwa mambo yakina Dr.Zul Premji, sijui kama bado yuko hai.
Kazi nzuri sana hizi kwa wenye mapenzi ya Parasitology and Entomologist.
Ila ni ajabu kwamba ni mtu binafsi kaweza kufanya haya, huku kwetu hata,serikali inashindwa.
Wenzetu wakiamua kufanya jambo wanaanza kwa kufanya sio maneno mengi kama huku nyumbani.
 
Serikali inashindwa na haiwezi! Pia mleta uzi ninaomba picha za hao panya wenye vitambi
Serikali hii y nyumbani hapana hawawezi kufanya maendeleo haya. Ila serikali kubwa zenye kujua umuhimu wa sayansi na teknolojia wanaweza kufanya yote haya.
Serikali za Uchina, Korea na kadhalika.
1702533473708.png

Kwa kawaida panya wengi wanakutana na mtiti wa vimelea kwenye utumbo haswa miamba kama vile, Tapeworms pamoja na pinworms. Hapa Panya 1000 amekutana na kitu kizito sana mpaka ngozi inakosa ushirikiano.

1702533741309.png

Tapeworms

1702533807442.png

pinworms
 
Serikali hii y nyumbani hapana hawawezi kufanya maendeleo haya. Ila serikali kubwa zenye kujua umuhimu wa sayansi na teknolojia wanaweza kufanya yote haya.
Serikali za Uchina, Korea na kadhalika.
View attachment 2842002
Kwa kawaida panya wengi wanakutana na mtiti wa vimelea kwenye utumbo haswa miamba kama vile, Tapeworms pamoja na pinworms. Hapa Panya 1000 amekutana na kitu kizito sana mpaka ngozi inakosa ushirikiano.

View attachment 2842006
Tapeworms

View attachment 2842007
pinworms
Wanakula vitu vya hovyo ndo mana wanakutana na maminyoo ya hatari
 
Back
Top Bottom