Ifahamu Manyovu mkoa wa Kigoma

zireya ndimkanwa

New Member
Aug 31, 2017
4
6
View attachment 587762
Bwn.S.K.JAPHET (BHUZUZU) alizaliwa Tar.05 Julai, 1974 katika eneo la Manyovu kijiji cha Mwayaya, Wilaya Buhigwe, Mkoa Kigoma. Ni mtoto wa 7 kati ya watoto 9 wa familia ya Mzee ANGELO BUZUZU KAHOBOLA MPENDA. Elimu yake ni Diploma ya Kompyuta na Ufundi ” DIPLOMA IN COMPUTER STUDIES AND MANTAINANCE” aliyopata KATIKA CHUO CHA UTALII MUSOMA-MARA mwaka 2009/010. Kutokana na changamoto nyingi hasa za mambo ya kale , alikusudia kuja kuwa mwandishi wa vitabu. Kwa mara ya kwanza wazo la kuandika kitabu lilimuijia katika miaka ya 1990 baada ya kuona baadhi ya kumbukumbu za mambo ya kale pamoja na mmomonyoko wa maadili na uharibifu wa Mazingira viki shamili miongoni mwa jamii. Pia alibaini Watu wengi wakipuuza na kukimbia hoja zinazochambuliwa na wataalamu/ watu wenye elimu za kawaida zenye lengo la kubainisha asili za watu. kutokuthamini, kutunza nakuendeleza mila zao. Aidha pia aliona Vijana wakiamua kuishi katika mitindo ya kigeni inayoletwa na utandawazi na kupanuka kwa Tekinolojia ambayo imeifanya dunia kuwapo kiganjani. Jamii pia imebainika kupoteza dira hasa pale ambapo utakuta vijana wakisikia muziki masikioni kwa kutumia headphone/ earphone’s music, matumizi ya mitandao ya kijamii mfn. Whatsup, facebook, twitter na nk. kwa matumizi yasiyo na maana. Hali hii imepelekea sehemu kubwa ya jamii na hasa vijana katika maeneo yote ya vijiji na mijini kukweza mila za kigeni huku wakisahau mila zao. Jambo hili limebainishwa katika kitabu chake kiitwacho “ IFAHAMU MANYOVU”. Katika mazungumzo na masimulizi ya Wazee wetu wa zamani jamii haikupaswa kusahau mambo yao ya asili. Kusahau kunapelekea watu kupoteza ndugu, jamaa na koo zao. Pia husababisha mila na Desturi za watu kufutika. Athari yake ni kwamba jamii huishi kama watumwa nyumbani kwao. Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa inayopoteza mila zake kwa kasi kubwa kwa kuiga mila za kigeni kwa mfn. Matumizi mabaya ya lugha; Usiingii badala ya usiingie, unaokopa badala ya unaogopa. Dhana ya eneo la Manyovu kuanzia Nkalizi wakati Manyovu ni Manyovu, Manyovu ni mjumuisho wa maeneo mengi huku Manyovu ina asili yake nk. Hivyo ni vyema mtu kutunza mila zake kwa kuzilinda ili zisiharibiwe, kuchafuliwa na kumezwa na tamaduni za mataifa ya nchi jirani au na tamaduni za makabila mengine yanayoishi katika mkoa na maeneo yetu. Jukumu la ulinzi wa tamaduni za watu ni la watu wenye tamaduni hizo. Haitafaa mtu kutoka sehemu nyingine kudumisha utamaduni wako ili hali wewe mwenyewe hufanyi hivyo. Tujali kilicho chetu.

IFAHAMU MANYOVU.

Kimeandikwa na,

Mr. S.K.Japhet (Bhuzuzu).
Tangu Mwaka 1990 – Agosti, 2017. Manyovu (Mwayaya)

UTANGULIZI

Tunafahamu wazi kwamba kila jina analopewa au linalotolewa kwa mtu au kitu huwa ni la kipekee (unique). Na kwamba linakuwa na maana na asili yake kadri ya mahitaji na malengo ya Yule anayelitoa jina hilo. Unapomkuta mtu akilitumia ama kuliita jina lako vibaya nadhani huwa unaumia sana hata kama jina lako litakuwa na maana nyingine zaidi. Kitabu changu nimekipatia jina IFAHAMU MANYOVU”. Jina hilo linakaribisha wenyeji na wageni wasiofahamu vizuri manyovu wafike na waone vitu vinavyoashiria jina la Manyovu na kumbukumbu za kihistoria zilizopo.

Watu wengi hawaelewi chanzo cha jina na eneo la Manyovu. Wameishia kusimulia ilivyotofauti na matokeo yake jamii ya Manyovu imepokea visivyo hivyo wamebakia kuishia kuifahamu kijuujuu hawajui ukweli wa asili yao. Wageni wanaokuja ndio wanaoanza kutufundisha asili zetu matokeo yake tunakuwa kama watu tusiojua mambo (vichwa maji) . Jambo hili limenipa msukumo wa kuandika kitabu chenye lengo la kutambulisha, kukumbusha na kuelimisha juu ya asili, eneo na chanzo chake.

Idadi ya watu wa Manyovu ki-utawala (Tarafa) ni kubwa na imeenea karibu sehemu zote za mikoa ya Tanzania. Endapo jamii hii ya watu itaachwa na kuishi ughaibuni bila kufahamu asili yao na ya jina lao kwa vyovyote itakuwa vigumu kulitangaza eneo lake vyema.

Katika kitabu hiki nimejaribu kuelezea kwa undani kabisa chanzo na asili ya jina. Pia nimeonesha jinsi ambavyo eneo hili limeendelezwa tangu kipindi cha utawala wa jadi, tawala za Kizungu na wakati wa uhuru. Katika miaka ya 1970 kipindi cha mfumo wa vijiji ndipo kumeonekana mabadiliko yaliyolenga kuhamisha au kuondoa kabisa majina ya sehemu za asili mfn. Manyovu(mwayaya), Buhigwe(Buyenzi), Ikavumu(Rusaba), Nkalinzi(Kalinzi), na Buha(Kigoma)nk. Nimebainisha sababu za zilizopelekea jina hili kufifizwa na athari yake. Harakati na mikakati ya kuendeleza jina hili kutokana na umaarufu wake nimezitaja. Nimetaja pia umuhimu wa kulinda na kuendeleza majina ya asili.

Ni matumaini yangu kwamba baada ya kukisoma kitabu hiki, kila mtu atakifurahia kwani kinatoa ujumbe mzuri kabisa wa kuhifadhi na kutunza mila na kumbukumbu za mambo ya kale kwa kizazi kilichopo na kijacho

ASILI YA JINA: limetokana na mto Manyovu. Mto huu hupatikana katika eneo liitwalo Bugalama (Ibhugalama) na ulikuwa ukItililisha maji yake katika mto Mtunguruzi. Kwa sasa mto huu umebaki kuwa mto wa msimu kwani unategemea mvua za masika kutokana na shughuli za kibinadamu. Jina lingine la Manyovu ni MAHWENYI. jina hili ni la utani (nickname) walililoitwa watu wa Manyovu na jamii ya watu wa Heru. ABHANYAMAHWENYI maana yake watu wa Manyovu. Jina hili halitumiki kwa sasa.
IDADI YA KABILA –MANYOVU;

Kabila la asili ni WAHA. Yapo pia makabila mengine kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliofika kwa shughuli za kikazi kama walimu, maafisa ugani, Mashirika na matabibu nk. Kuna pia idadi ndogo ya kabila la Wahutu kutoka Burundi. Hawa walikimbia kwao vita vya wenyewe kwa wenyewe.

MANYOVU ILIPO:

Manyovu ipo Kaskazini mwa Makao makuu ya Mkoa wa Kigoma umbali wa takribani km76 hivi kutoka Kigoma Mjini kupitia Barabara ya Lami itokayo Mwandiga hadi Munanila yenye umbali wa km 64 na kutoka Munanila kuelekea Kusini umbali wa km12 ndipo MANYOVU. Majina mengingine ya maeneo yaliyoko karibu yake ni Ibhugalama na Inyabhihama. Imepakana na Makao makuu ya Wilaya Buhigwe, kijiji cha Kibwigwa na Nyankoronko upande wa Mashariki. Upande wa Kaskazini kuna Vijiji vya Munanila na Mkatanga, Magharibi kipo kijiji cha Nyakimwe na Kusini kipo Kijiji cha Muhinda.

KUFIKA MANYOVU:

Ili mtu aweze kufika Manyovu akitokea Kigoma mjini atapaswa kwenda katika kituo cha mabasi kilichopo Masanga kwa jina maarufu (Stand Mpya). Pale ataona gari aina ya Noah au Hiace ziendazo Munanila. Atapanda gari mojawapo kwa kiasi cha Tshs.4,000/= hadi Munanila kisha atapanda bodaboda kutoka Munanila kuelekea upande wa Kusini hadi Manyovu kwa nauli ya Tshs.2,000/=. Umbali kutoka Munanila ni km12 ili kufika Manyovu. Pia kuna usafiri mwingine wa tax (michomoko) inayo anzia safari zake njia Panda ya Mwandiga hadi Manyovu kwa nauli ya Tshs.6,000/=. Ipo pia njia ya mchepuko itokayo Kigoma Mjini hadi katika kijiji cha Nyarubanda. Pale mtu atapaswa kukata kona kuelekea upande wa Mashariki kupitia kijiji cha Muhinda penye Misioni ya Kanisa Katoliki. Ni umbali wa km8 hivi kufika Manyovu.

Njia nyingine ni ile inayopitia Kasulo. Kwa kutumia njia hii, mtu atapaswa kupanda gari aina ya Hiace zinazoekwenda Manyovu katika kituo cha Basi Kasulo. Ataelekea upande wa Kaskazini Magharibi akipanda mlima Rusunwe hadi kijiji cha Kibwigwa. Kisha atakatisha upande wa Magharibi umbali wa kama km5 hivi atakuwa amefika Manyovu.

MITO MAARUFU:

Manyovu ipo katikati ya Mto NyaKafumbe unaotiririsha maji yake kutoka upande wa Kaskazini Magharibi, ukitenganisha vijiji vya Nyakimwe na Munanila na hutiririka maji yake kuelekea upande wa Kusini penye kijiji cha Muhinda. Pia upo Mto Mtunguruzi ambao una umaarufu mkubwa. Moja ya umaarufu wake ni kuwepo maporomoko wawili ya maji, kuwepo kituo cha kuzalisha umeme wa nguvu za maji na kuwepo eneo la asili la kuogelea liliokuwa likitumiwa na wenyeji na wasafiri waliotoka sehemu za Myama na Heru wakielekea Ziwa Tanganyika kununua samaki (kwibhenga dyabhahanzo) yaani sehemu ya kuogelea wafanyabiashara. Mto huu hutiririsha maji yake kutoka upande wa Kaskazini kuliko viijiji vya Munanila na Mkatanga kuelekea Mashariki ambako kuna vijiji vya Kibwigwa, Buhigwe na Nyankoronko na kuelekea upande wa Kusini. Mito hii ndiyo imechukua karibu sehemu kubwa ya mipaka inayozunguka eneo la Manyovu licha ya kwamba katika upande wa Kaskazini penye mpaka wa Munanila katika eneo la Nyakitanga ni nchi kavu. Pia kuna mito mingine iliyopo katika eneo hili kama mto Kasarenda, Mto Matandala, Mto Nyamateke na mto Nyasabha. Mito hii ndiyo chanzo kikuu cha maji yanayotumiwa na jamii inayoishi kuzunguka eneo la Manyovu.

MILIMA MAARUFU;

Mlima mkubwa katika eneo hili ni ule uitwao Sindenzwa ulioko Mashariki kuelekea Kijiji cha Nyankoroko. Pia kuna Kavunagule na safu za milima Magoma.

KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA:

Manyovu inazo kumbukumbu nyingi zinazotambulisha eneo. Sifa hizi sio tu kwamba zimeweza kulitambulisha katika Mkoa, bali pia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kulikuwa ndio Makao makuu ya Tawala za Jadi za Wateko na Abhatwale-Bhanini (Kibila). Ipo Shule kongwe na maarufu inayomilikiwa na serikali inayoitwa Manyovu Extended Primary School iliyoanzishwa enzi za utawala wa Kiingereza tangu mwaka 1953. Kuna pia Zahanati Kongwe inayotoa huduma za afya , dawa za Ukoma(reprosy) na TB iitwayo zahanati ya Manyovu. Uwepo wa Nyumba ya kulala wageni wa Kizungu tangu enzi za Ukoloni wa Kiingereza (Manyovu Rest House). Mahakama ya Mwanzo kongwe tangu koloni la Kijerumani ipo ingawa jengo limeterekezwa na kubaki tupu huku mashauri yakifanywa katika chumba cha kupanga. Kunapatikana Josho kongwe la kuogeshea mifugo na Lunch ya kuzalishia ndama Bora (Bull centre) eneo la Nyabututsi. Kituo kilichotumika kupokelea na kuhifadhia vifaa vya kijeshi katika kipindi cha hali ya hatari kati ya Tanzania na Burundi mwaka 1974 kilikuwa hapa. Uwanja maarufu wa mpira wa Miguu na Riadha wa Manyovu. uwepo wa Kasiki ya kutunzia fedha zilizo tokana na ukusanyaji kodi ya kichwa enzi za Ukoloni wa Kijerumani. Ndipo penye Tarafa ya Manyovu.

VIONGOZI WA KITAIFA WALIOWAHI KUTEMBELEA MANYOVU:

1). Hayati Mh. Edward Moringe Sokoine Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 1983

2). Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-1985

MPANGO WA KUFUTA JINA LA MANYOVU:

Kuanzia mwaka 1970 Manyovu ilifanyiwa mabadiliko makubwa. Licha ya kwamba jamii nzima iwe imesoma ama haijasoma inafahamu wazi dhima ya neno” jina” kwamba ni Utambulisho. Kutokana na masimulizi ya wazee wetu wa zamani wanasema majina ya sehemu zao za asili yalibadilishwa badilishwa bila sababu wala maelezo, na kwamba hakukuwa na watu wenye weredi wa kuhoji juu ya hali hiyo. Aidha pia maeneo yaliyokuwa na taasisi za kijamii, taasisi hizo ziliweza kuhamishwa bila kubainisha sabababu yoyote ya msingi na kufanya shughuli zake huko. Ifahamike pia kwamba hata mipaka nayo ya vijiji imeweza kuhamishwa kienyeji pasipo kushirikisha jamii iliyopo. Kwa mfano, mwaka 1970 Shule kongwe ya Manyovu Extended Primary School ilibadilishwa jina na kuitwa “Shule ya Msingi Mwayaya”, Mwaka 1972 Kijiji cha Manyovu kilibadilishwa jina na kuitwa Kijiji cha Mwayaya, licha ya kwamba eneo la Manyovu lilikuwa ndipo yalipo makao makuu ya kijiji na wakati huo huo eneo la Mwayaya lilikuwa mbali ingawa ilikuwa ndani ya kijiji cha Manyovu. Katika miaka ya 1970 Katibu Tarafa aliweza kuhamia kijiji cha Munanila, ingawa jina la Manyovu liliedelezwa na kutumika. Kumeendelea kuonekana huduma za kijamii kuhama hama kwani Mahakama nayo ilihamia Munanila. Jambo la kushangaza ni pale Jina letu Manyovu linapoendelea kutumiwa badala ya kutumia majina yao.

Katika dadisi dadisi zangu niligundua kuwa baadhi ya viongozi waliokuwa wakitoa huduma katika baadhi ya taasisi hizo, ndio waliofanya mikakati ya kuhamishia huduma hizo kwenda kwenye vijiji vyao. Ni wazi kwamba kilichofanyika kilikuwa na shabaha ya kuelekeza huduma kwa jamii zao ili wanufaike nazo kama vile kupata huduma karibu huku jamii iliyo kubwa ikiachwa na kutelekezwa bila huduma yoyote. Kituo cha polisi kilihamia pia Munanila ambacho kinafahamika kwamba ni chombo cha kulinda raia na mali zao. Kilipelekwa kulinda watu kiduchu tena walioko mpakani huku jamii kubwa ya Tarafa ya Manyovu iliyo na vijiji vingi ikiterekezwa nakuachwa bila huduma wala ulinzi wowote wa watu na malizao.

Mwaka 1985 lilitokea tukio lisilo la kawaida pale Serikali kuu ilipotoa Tangazo kwa kila mwananchi katika Tarafa yake kushiriki zoezi la kujenga Sekondari. Tarafa ya Manyovu ilikuwana eneo kubwa kiasi cha kukidhi kupewa wilaya. Mpango uliandaliwa kila raia alishiriki vyema katika zoezi zima la ujenzi. Baada tu ya ujenzi kukamilika bila ya kushirikisha wananchi, inasekana kwamba shule lilipachikwa jina la MUNANILA SEKONDARI. Kila mtu alishangaa tukio hilo la kushangaza kwa kuitwa jina hilo badala ya kupewa jina lenye kuridisha wananchi wote walioshiriki katika ujenzi wake. Aidha pia eneo lenyewe lipo katika kijiji cha Mwayaya na siyo Munanila. Hadi sasa shule hii imeendelea kubakia na jina hilo huku wananchi wa Vijiji vilivyoshiriki katika ujenzi wakibaki kunung’unika kimoyo moyo wasijue la kufanya.

HARAKATI ZA KUTUNZA , KUENDELEZA NA KUTANGAZA JINA MANYOVU.

Jamii ya Manyovu licha ya kwamba wapo walimu uchwala wanaoendelea kufundisha uongo juu ya eneo na asili ya Manyovu, imejipanga vizuri kwa lengo la kuhakikisha kwamba jina lao linatunzwa, kuendelezwa na kutangazwa mahali popote ndani na nje ya nchi. Kwanza imerudisha shule ya msingi iliyobadilishwa kutoka jina lake la awali la Manyovu Extended Primary School kuwa Shule ya Msingi Mwayaya sasa imerudisha jina lake la awali na kuitwa Shule ya Msingi Manyovu. Imeanzishwa Shule ya Sekondari Manyovu. Upo pia mpango wa kuita kitongoji jina Manyovu. Na kwa kuwa pia kata ya Mwayaya imeundwa na kijiji kimoja chenye vitongoji (3) vitatu, ni bayana kwamba mbeleni kutaundwa Halmashauri ya Mji mdogo. Rai kwa viongozi wa Kijiji cha Mwayaya kwamba msikubali wanasiasa kuwatenganisha kwa kuunda vijiji vingine ndani ya kijiji kimoja. Hilo litapelekea kunyimwa Halmashauri ya Mji mdogo. Kwa kuzingatia Idadi kubwa ya watu iliyopo ipatayo 21,000, inafaa kabisa Kupeleka maombi ya kuwa na MJI MDOGO WA MANYOVU katika vikao vya Halmashauri ya Wilaya-Buhigwe.

WATU MAARUFU - MANYOVU:

1. Abhatwale Bhanini- waliotawala Manyovu

Jina Alikotoka

i. Bhikali Kigina------------------------ Manyovu

ii. Lubhele Kigina-----------------------Manyovu

iii. Chureha ----------------- Heru

iv. Agostino Nguge----------------------- Heru

v. Laurent Lugema------------------------Buyenzi

2. Wabunge waliowahi Kuongoza baada ya kufutwa Tawala za Jadi-Manyovu.

Jina Alikotoka

i. Laurent Lugema----------------------------------Buyenzi

ii. Antony Peneza-----------------------------------Msagara

iii. Chobhaliko Bwenda----------------------------Nyakitanga

iv. Midabha Kazuzulu------------------------------Nyakimwe

v. Mh. Mbebagu Kironsi Mpologomyi Mhama;

Manyovu ndipo anapozaliwa Mh. Mbebagu Kironsi Mpologomyi Mhama.Aliyepata kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa huyu ni maarufu sana kutokana na shughuli zake za kisiasa. Aliweza kupambana ili kuchukua ubunge kwa miaka mingi akipambana na wagombea wengine kutoka Kasulo enzi za jimbo moja la Kasulo. Baadaye baada ya jimbo hilo kugawanywa katika majimbo mawili ya Kasulo Mashariki na Manyovu, aliweza kuliongoza jimbo la Manyovu kwa kipindi kirefu.

3. Watu wengine maarufu –Manyovu;

Hayati Komando Dominiko Nshimanyi.

Mtu mwingine maarufu ni Hayati Komando Dominiko Nshimanyi. Huyu umaarufu wake ulikuwa mkubwa sana katika maeneo yote ya Manyovu, Kasulo, Kigoma na Taifa. Aliongoza vikosi vya askari wetu wakati wa mapigano kati ya Tanzania na Uganda mwaka 1978/79. Komando wetu tutamkumbuka sana alale mahali pema peponi.

Mdogo wa Marehemu Mzee Nzungu ;

Yupo mtu mwingine Maarufu sana, ingawa amebaki katika vinywa vya watu pasipo kufahamika wapi alipo. Huyu si mwingine ni Yule Baharia wa Meli ziendazo katika nchi za Ulaya (Uturuki) mdogo wake Marehemu Mzee Nzungu. Inasemekana huyu ni Baharia mtaalamu sana.Tutaendelea kuwakumbuka na kwa wale walio hai ni ombi kwao kwamba tutoe michango yetu kwa jamii ili kwamba hata pindi tutakapolala(kufariki) tuache kumbukumbu zetu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo kwa lengo la kudumisha historia zetu na za familia kwa ujumla.

Mh. Hoka Lubaka; Amewahi kuwa Katibu wa CCM-Mkoa KIGOMA.

PhD Mussa Gidioni Shishi; Mkuu wa chuo Kikuu kimojawapo-ARUSHA.

Bwana Fedrick Dismasi Mapengu Bileha;

Huyu bwana ni maarufu sana kutokana na kipaji chake cha ubunifu wa kiufundi. Elimu yake ni Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Manyovu. Alinunua baiskeli kisha akaiwekea gia aliyoitengeneza mwenyewe. Baiskeli hiyo ilimwezesha kupanda milima iliyoshindikana wakati wa safari zake. Ni fundi wa vitanda na milango shughuli anayoifanya na kumletea faida pasipo kusoma chuo/ shule yoyote ya ufundi. Amejaribu kutengeza umeme unaotokana na maji kutokana na ubunifu wake mwenyewe. Shughuli ambayo ameifanya kwa kutumia ubunifu wa kujitengenezea sampuli za vipuri pasipo kumshirikisha mtaalamu yeyote. Ni bwana anayeingia kwenye karne ya 21 ya Sayansi na Teknolojia pasipo kusukumwa na Elimu wala wakati bali tafiti zake na ubunifu.

UTAWALA-MANYOVU.

Manyovu ni Tarafa. Eneo hili lipo katika Kitongoji cha Mwayaya kinachoongozwa na Mwenyekiti Bwana Jackson Eliasi Kiloloma kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Mwayaya kinachoongozwa na Mwenyekiti Mh. Dangi Ayubu Kiyanga Myella kupitia CHADEMA. Aidha pia Manyovu inapatikana katika Kata Mwayaya, wilaya Buhigwe, Jimbo la Uchaguzi la MANYOVU, MKOA WA KIGOMA.

MANYOVU KI-ELIMU:

SHULE ZA MSINGI. Kuna shule za Msingi 4 ; Manyovu Extended Primary School, Shule ya Msingi Mwayaya, Kibila Shule ya Msingi na Gwimbogo Shule ya Msingi.

WATU MAARUFU WALIMU NA WANAFUNZI WA LIOSOMEA MANYOVU EXTENDED

PRYMARY SCHOOL:

JINA CHEO

i. Mzee Melickiadesi------ Mwl. Mwanzilishi wa shule---1950s

ii. Hayati Dominiko Nshimanyi------------Mkuu Brigedi- Kanda ya Maghribi.

iii. Mh. Mbebhagu Mpologomyi –-------- PhD, Mbunge na Naibu Waziri wa Fedha

iv. Daktari Jackson Bujiji-------------------- Mganga Hospitali Wilaya Kasulo

v. Hayati Eng.Thomasi Chiza Melickiadesi

vi. Mwl. Kalumbilo------------------------------ Mwl. Mkuu

vii. Mwalimu Banzi-------------------------------Mwl. Mkuu

(Naomba majina ya watu maarufu waliosoma katika shule hii na mwaka wa kumaliza)

SHULE ZA SEKONDARI;

Kuna; Manyovu Shule ya Sekondari, Munanila Shule ya Sekondari na Bakanja Shule ya Sekondari inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Misioni Muhinda.

VIVUTIO VYA UTALII-MANYOVU.

A. Kituo cha utafiti mbegu bora za Kahawa TACRI-Manyovu.

Kuna kituo cha utafitiwa wa miche bora ya Kahawa kiitwajcho TACRI. Pamoja na kwamba kituo hiki kina lengo zuri kwa maisha ya jamii ya watu wa Manyovu bado hakijakidhi vigezo vya kumiliki eneo la Mradi kutokana na njia walioitumia katika kupata ardhi hiyo. Kumekuwa na manung’uniko makubwa ya wananchi kwamba hawana uhalali wa kumiliki ardhi hiyo kwani eneo waliloomba ni dogo ukilinganisha na maeneo wanayotaka kumiliki, huku wenzao yaani upande wa walalamikiwa wakidai kupewa maeneo haya na Serikali ya Kjiji iliyokuwepo wakati huo.

B. Maporomoko ya Maji Mto Mtunguruzi-Manyovu.

Ni eneo lenye kivutio kikubwa cha utalii. Hapa ndipo kuna Mradi wa Umeme unaoendeshwa kwa nguvu ya maji( Mtunguruzi falls Hydro Power) unaomilikiwa na Dhehebu la Wasabato. Hapo zamani eneo hili lilikuwa likitembelewa na Wazungu kutokana na Hali ya hewa nzuri inayofanana na hali ya Ulaya. Pia kama tulivyoona katika sehemu hapo juu. Uwekezaji nchini Tanzania unafanyika pasipo elimu ya kutosha kwa raia. Zoezi hili hufanyika kwa siri kubwa baina ya mwekezaji na viongozi. Eneo hili nalo inasemekana kwamba limo katika mgogoro mkubwa baina ya raia na wawekezaji waliomba kupewa ekari 40 mbele ya Mkutano Mkuu wa Serikali ya Kijiji lakini cha kushangaza wao walichukua takribani ekari 120.

C. Mapango ya Nyankwale-Manyovu.

Haya ni mapango yaliyopo km3 hivi kutoka eneo la Manyovu. Jina maarufu la Mapango haya ni MAPANGO YA NYANKWALE. Pamoja na kwamba mapango haya yapo karibu kabisa na jamii, bado hakuna utafiti uliokwisha fanyika ili kubaini ukubwa wake, shughuli zilizofanyika humo na watu wa zamani. Mbali ya kuona vyungu vilivyotumika kupikia chakula, shughuli pia za matambiko zinawezekana kufanyika humo. Kuna pia mapango mengine mengi katka eneo la IMAGOMA.

Ni wazi kwamba Watanzania tumekuwa tukilalamikia ukosefu wa AJIRA huku tukiwa na fursa tele. Tukizitumia fursa hizi tulizonazo tunaweza kupata pesa na kutengeneza ajira nyingi kwa Watanzania. Rai yangu kwenu Wasomi vijana, wazee, Mabibi na Mabwana, Matajiri, wakulima, Viongozi wa Taasisi za Kiserikali na zisizo za Kiserikali (NGOs, CBOs & FBOs mliozaliwa, kuishi, kuhamia na kusoma hapa MANYOVU Tuunganisha nguvu zetu pamoja ili tuweze kujiongezea kipato na kuinua hali uchumi wa ndugu zetu pamoja na Uchumi wa Taifa la Tanzania kwa Ujumla.

D. Majani ya Kuezekea nyumba yanayo dumu zaidi ya miaka 30 (Uruyange);

Hiki ni kivutio pia cha utalii. Sifa ya Majani haya yanayopatikana pekee hapa Manyovu ni kwamba, huweza kudumu kwa zaidi ya miaka 30 yakiezekwa vizuri kwenye nyumba isiyo na tatizo la mchwa bila kuharibika wala kuvuja nyumba.Sifa ya nyasi hizi ni ya kipekee jambo linalopelekea kupendwa na watu hasa wafanyabiashara wa mjini wa ndani na nje ya nchi. Biashara za nyasi huuzwa katika maeneo ya vijiji jirani, Kigoma Mjini na katika nchi jirani ya Burundi. Majani haya yanafaa sana kuezekea nyumba hasa katika maeneo yenye joto kali kwani hayaruhusu joto kupenya.

E. Kituo cha mafunzo ya kulenga shabaha (redge)-Manyovu.

Kituo cha kulenga shabaha kinachotumiwa na Askari wa Jeshi la Mgambo na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni Kivutio muhimu sana. Kipo sehemu moja iitwayo Mkilimo. Ni njia inayokwenda kwenye mapango ya Magoma (Imagoma).

F. Makazi ya Watawala wa Jadi (Abhatwale Bhanini-Manyovu;

Haya ni makumbusho yanayotanabaisha sehemu, kulinda na kuhifadhi historia za watawala wetu wa Jadi. Kwa kuwa jamii zetu hatujui fedha zinakopatikana, tumeingia kuyaharibu kwa kudhani hayana maana kumbe umuhimu wake ni mkubwa. Utunzaji wa maenneo haya si tu kuhifadhi mambo ya kale bali pia hutupatia fedha kutokana na shughuli za utalii na utafiti. Maeneo haya nakumbuka yapo ilipo Manyovu Extended Primary School na pale anapoishi Mzee Mlandamle Ndilaliha(KAZAGANYA) .

G. Majengo ya Zamani-Manyovu

Yapo majengo mengi ya zamani ambayo ni sehemu ya Utalii na kitambulisho cha Manyovu. Mfn. Jengo la Mahakama, Rest House, Ofisi ya Tarafa, majengo ya Shule ya Msingi Manyovu, Majengo ya Zahanati ya Manyovu, Nyumba za zamani za Walimu(staff houses), shamba la ndizi la shule lililotumika kuficha magari na baadhi ya siraha za kivita wakati wa hali ya hatari kati ya Tanzania na Burundi.

H. Mito maarufu ya Mtunguruzi , Kasarenda na Nyansabha-Manyovu

Kuna mito maarufu inayofaa kwa utalii. Mto Mtunguruzi wenye maporomoko mawili ya maji. Mto Nyasabha na Nyamateke iliyo chanzo kikubwa cha maji ya kunywa. Mto Kasarenda uliotumiwa na wanafunzi na walimu kama sehemu ya kuchota maji ya kunywa, maji ya kufyatulia tofari za ujenzi wa shule ya Msingi Manyovu . Hata hivyo mto Kasarenda umekauka kutokana na uharibifu wa sehemu iliyokuwa chanzo cha mto. Mchango wa mto huu ni mkubwa kwani umaarufu wa wanafunzi na walimu wa shule ya Manyovu ulitokana na huduma ya maji walioipata katika mto huu. Sasa mto umekauka, shule bado ipo, wanafunzi wapo, walimu wapo na wanakijiji wapo. Je, huduma ya maji itapatikana wapi tena? Kwanini kusiwepo mpango maalumu wa kutoa elimu kwa lengo la kurudisha upya mazingira na kubaki kama yalivyokuwa tangu huko nyuma?

I. Ngoma na Burudani;

Sindimba na Bhusambele, akarundo na kasimbo (agasimbo)

Manyovu imekuwa na historia ya michezo kwa muda wa miaka mingi.Kilikuwepo kikundi cha ngoma ya Sindimba kilichoongozwa na Bi Jonabia Kanani, na Mpiga Ngoma maarufu Bwana Butati Kabhohe. Watu hawa katika enzi zao wakiwa wanafunzi waliweza kuwakilisha vizuri Manyovu katika sherehe zilizofanyika wilaya Kasulo. Ngoma hii ni ya asili ya Kabila la Wamakonde. Ngoma nyingine ni ya Mapigo saba. Ngoma hii inaongozwa na Bwana Bheha Yotamu Sunko Nyogoto. Ngoma hii ni ya asili ya Kabila la Waha (Ubhusambele). Hutoa burudani safi wakati wakicheza. Ngoma hii bado ipo ingawa hupotea kidogo kipindi Mkuu wake anapokuwa katika safari za utafutaji wa kipato kwa ajili ya familia yake.

Ngoma za Harusi (Idenga).

Hizi ni ngoma zinazochezwa na wanawake wa Kabila la Waha. Mama maarufu katika uchezaji na uimbaji wa ngoma hizi aliitwa Gasabho (mama Kibwa). Huyu Alisha kuwa marehemu, Mungu amweke mahali pema peponi. Huyu alipokwenda mbele kucheza alikuwa anafurahisha sana. Hebu nikupe kipande kidogo cha nyimbo zake:

WIMBO KIITIKIO.

1. Yeeee mutama ndalaye, ee! Eeeeeeeeeeee!!!!!!!× 2

Ntakulima ngwaye, ee! aye ndovyina ngwaye, ee!.

( maana yake: Nakuheshimu sana Bwana na nina furahi kwa mwaliko wako. Siwezi kulima nikiwa mgonjwa, ila naweza kucheze nikiwa mgonjwa).

WIMBO KIITIKIO

2, I ndege ilobhobha×3

Tegeza kokandazi h’igi!!

Nako sukudyoha h’igi

Kadyohela bhana h’igi

Bhakili bhatoyi h’igi

Inde. Inde. Inde.

Nyimbo hizi za asili huburudisha wenyeji na wageni wanaotembelea maeneo yetu. Hivyo ni sehemu inayofaa kuwekeza kwa ajili ya kipato na burudani.

Pombe ya asili ya kayoga;

Kinywaji cha pombe hutumika kama kiburudisho kwa jamii nyingi ya Manyovu. Ni utamaduni wao kutumia pombe. Pombe ya kienyeji iitwayo Kayoga hupendwa sana kunywewa na wenyeji na wageni hasa katika kipidi cha baada ya kazi. Kinywaji hiki huuzwa pia katika nchi jirani ya Burundi. Kuna siku maalumu katika Juma ambapo misafara mirefu ya watu waendao kwa miguu, baiskeli na pikipiki huelekea sokoni nchini Burundi penye soko kubwa la pombe na vitu vingine lililopo kabisa jirani na mpaka wa Tanzania nchini Burundi.

J. KUANDAA MINARA YA KUMBUKUMBU ZA VIONGOZI.

Kwa mfano; Mnala wa kumbukumbu za viongozi wa jadi. Wabunge, orodha ya wenyeviti walio wahi kuongoza kijiji, wanafunzi wa Manyovu Extended Primary School waliofanikiwa kupata elimu/fedha kutambuliwa na kuomba kusapoti maendeleo ya Kijiji na pia kitakuwa kivutio cha uatlii.

SHUGHULI ZA WAKAZI-MANYOVU;

Wakazi wengi wa Manyovu hujishughulisha na kilimo na Ufugaji. Licha ya kwamba ardhi imetumika kwa kipindi kirefu na kubaki bila rutuba jamii kwa kutumia pembejeo bado inaweza kujipatia mazao mengi. Manyovu kunalimwa ndizi, maharage, mahindi, njegere na mhogo. Kuna pia kilimo cha kahawa ambacho ni cha Biashara. Mifugo imeanza kupunguzwa na kuhamishwa kwenda katika sehemu zenye marisho mazuri. Baadhi ya mifugo inayofugwa nyumbani kwa lengo la biashara, chakula na mbolea ni kama; nguruwe, mbuzi, ng’ombe wa maziwa na kuku. Wapo pia wanaofuga sungura na bata. Sehemu zinazotumiwa na wenyeji kwa ajili ya kuchungia ng’ombe baada ya kugundua ukosefu wa malisho hapa Manyovu ni katika mapori ya wilaya za Kasulo na Uvinza.

HUDUMA ZA JAMII

i. HUDUMA ZA AFYA;

Kuna Zahanati iliyojengwa tangu wakati wa enzi za ukoloni. Zahanati hii kutokana na udogo wake, wananchi walilazimika kujenga jengo lingine na kuliacha la zamani. Zahanati mpya iliyopo inakidhi kabisa vigezo vya utoji huduma bora ya afya. Pia wananchi wameweza kujenga kituo cha Afya. Kituo hiki kimekamilika kikiwa na vyumba vya kutolea dawa na kulaza wagonjwa isipokuwa changamoto iliyopo ni uhaba wa nyumba za kulala matabibu,Vitanda na dawa.

ii. KUNA GODAWN 1 LA KUHIFADHIA NAFAKA.

Jamii ya Manyovu imejipanga kimkakati. Imeweza kujenga Godawn kubwa ya kuhifadhi nafaka, ingawa kwa sasa Kahawa ndiyo huhifadhiwa humo. Huhifadhiwa kabla na baada ya mauzo ikisubiri kusafirishwa.

HALI YA KISIASA-MANYOVU.

Jamii ya Manyovu inao uelewa mkubwa wa mambo ya Kisiasa. Inatambua kwamba Serikali ipo na hutawala kwa kuzingatia misingi ya sheria na utawala bora. Na kwamba hutekeleza shughuli zake kwa lengo la kuhakikisha maendeleo yanapatikana miongoni mwa jamii. Siasa za vyama vingi zinafanyika na kwa sasa serikali inayoongoza katika kijijiji hapa Manyovu inatokana na chama cha CHADEMA.

Palipo na mafanikio hapakosi changamoto. Viongozi wanaotokana na CHADEMA mara nyingi hukumbana na kamatakamata za hapa na pale hasa pale wanapo jaribu kusimamia, kurekebisha na kukemea juu ya mambo yaliyotekelezwa kinyume cha sheria na serikali iliyokuwepo madarakani.

DINI-MANYOVU;

Watu wa jamii ya Manyovu zamani walikuwa na imani yao ya asili. Waliamini kuwepo Miungu mingi, ingawa mti wa Mrumba ulikuwa kielelezo cha Mungu wao. Waliamini pia uwepo wa mizimu. Hawa ni watu waliofariki zamani ambao waliaminika kuwa waombezi wa jamii ya watu walio hai kwa Miungu yao.

Kwa sasa, watu wa Manyovu ni waumini wa Kikiristo na Kiislamu. Wakristo ndio dini kubwa ukilinganisha na dini ya Kiislamu.

TARAFA YA Manyovu;

Hii ni moja ya Tarafa za wilaya ya Buhigwe. Tarafa hii imeundwa na vijiji vya ; Mkatanga, Kitambuka, Kibande, Kibwigwa, Buhigwe, Nyankoronko, Bukuba, Janda, Kinazi, Rusaba, Mubanga, Nyaruboza, Muhinda, Nyakimwe, Munanila na Manyovu (Mwayaya). Huko nyuma kabla ya mfumo wa tarafa, eneo hili lilikuwa chini ya utwala wa jadi wa Watwale(Umutwale-Munini) katika eneo la Manyovu (Mwayaya) hivyo kupelekea pia Wazungu wa kikoloni kundelea kulitumia eneo hili la Manyovu kuwa Makao makuu ya Tarafa.

Sababu zilizopelekea eneo hili kukubalika kuwa makao makuu ya Tarafa; kwanza yalikuwa makao makuu ya Abhatwale wa Manyovu, pili ni mbali kutoka kwenye mpaka wa Burundi na Tanzania, tatu eneo lake linaweza kufikika kwa urahis na jamii yote ya Manyovu, nne huduma nyingi za jamii zinapatikana katika eneo hili mfn. Maji(bomba), mahakama, shule, zahanati, josho, kituo cha kuzalishia ng’ombe bora na rest house, ni katikati ya maeneo yote yanayoundwa na Tarafa ya Manyovu. Zote hizi tunaziita huduma za jamii.

IMEANDALIWA NA MWANAHARAKATI WA MAMBO YA KALE-
NDG. S.K. JAPHET (BHUZUZU)
Tangu 1990 - AGOST, 2017- Manyovu(Mwayaya) wilaya Buhigwe Mkoa Kigoma.

NB: KITABU HIKI KIKO KWENYE MCHAKATO WA KUKAMILISHWA, HIVYO NDUGU WASOMAJI KAENI MKAO WA KULA. KITASHUKA SOKONI HIVI PUNDE. AIDHA PIA NAOMBA WADAU WOTE WENYE MOYO WA KUSAPOTI JUHUDI ZANGU WA NDANI NA NJE YA NCHI WAWASILIANE NAMI ILI TUONE NAMNA YAKUFANYA MAKUBALIANO KWA LENGO LA KUCHANGIA FEDHA ZA UCHAPAJI WA KITABU HIKI.

Kwa michango,maoni na ushauri wasiliana nami kwa;
FACEBOOK-Http://www.facebook.com/japhet sanganigwa9.
E-MAIL-Njelo0504nkobwa@gmail.com

http://www.JamiiForums.com/Nimuzese0504@gmail.com
SIMU YA MKONONI-+255763346826/ +255627818314.
 
Safi mkuu. Next week nitafika hapo Kalinzi, itabidi nije nitembee huko Manyovu mpaka Burundi.
 
Kuna tofauti gani kati ya Waha na Wahutu (wa Burundi) katika mila na desturi? Ilikuwaje lugha zao zikaingiliana kama siyo kushabihiana? Mfano: Idenga, gasimbo, uruyange, n.k; vipi kuhusu majina nayo kufanana ya huku na kule? Mf. Nguge, Chiza, Harimenshi, Kijigo, Ntakamurenga, Zireya, Ndimkanwa, Ndayishimiye, Ndikumana, Hajayandi, Ndolimana, nk.
Nimekuwa siku zote nikiona Waha mkitumia nguvu nyingi sana kujitenga na asili ya Burundi LAKINI ukweli unabaki pale pale kwamba eneo la BUHA (Kigoma) kabla ya mwaka 1884 lilikuwa chini ya himaya ya Rwanda-Urundi. Kwa ufupi Kigoma haikuwa sehemu ya Tanganyika!
Nasubiri toleo lijalo, nina uhakika utaonesha koo mbalimbali zinazoishi eneo hilo. Ninachokuhakikishia ni kwamba majina mbalimbali ya koo utakazo taja, tutaona kwamba zinapatikana Burundi pia. I'm waiting to see!
 
Wewe unaanda mtego wa noti unauweka huku hadharani.... Ngoja waomba lift wasiojulikana wakimbie nayo..... Nakushauri toa hii, then Njoo kando nikupe namna.
 
Kuna tofauti gani kati ya Waha na Wahutu (wa Burundi) katika mila na desturi? Ilikuwaje lugha zao zikaingiliana kama siyo kushabihiana? Mfano: Idenga, gasimbo, uruyange, n.k; vipi kuhusu majina nayo kufanana ya huku na kule? Mf. Nguge, Harimenshi, Kijigo, Ntakamurenga, nk.
Nimekuwa siku zote nikiona Waha mkitumia nguvu nyingi sana kujitenga na asili ya Burundi LAKINI ukweli unabaki pale pale kwamba eneo la BUHA (Kigoma) kabla ya mwaka 1884 lilikuwa chini ya himaya ya Rwanda-Urundi. Kwa ufupi Kigoma haikuwa sehemu ya Tanganyika!
Nasubiri toleo lijalo, nina uhakika utaonesha koo mbalimbali zinazoishi eneo hilo. Ninachokuhakikishia ni kwamba majina mbalimbali ya koo utakazo taja, tutaona kwamba zinapatikana Burundi pia. I'm waiting to see!
si kweli sehemu ya tawala iliyokuwa Rwanda -Urundi ilikuwa Bukoba siyo Buha
 
Bila kusahau almost 98% ya wanaotoka manyovu ni warundi...haswa pale nyarubanda...
 
si kweli sehemu ya tawala iliyokuwa Rwanda -Urundi ilikuwa Bukoba siyo Buha
Mkuu usitake kupotosha alichosema jamaa ni kweli maana kigoma ni buha land nafikiri ndo kulikua na mwami nani sijui yule yani waha huwezi tofautisha na warundi ni kaka na dada aisee....
 
Da hii thread imenikumbusha mbali sana nilisoma nyamasovu shule ya msingi Std 2 tukahamia Dar mpaka Leo sijarudi tena almost 15 years ago
 
Hongera sana sana sana umemaliza kika kitu. Congrats
 
Kijana bado hujaijua vizuri
Manyovu unachanganya mambo
 
Da hii thread imenikumbusha mbali sana nilisoma nyamasovu shule ya msingi Std 2 tukahamia Dar mpaka Leo sijarudi tena almost 15 years ago
Utakua umemaliza chuo mwaka jana au mwaka huu mkuu
 
MANYOVU mpaka KIGOMA mjini !
Jionee mazingira ya kijani kitupu na ardhi ya rutuba kwa mazao mbalimbali na wimbo maarufu wa Kiha ukiwasindikiza katika safari hiyo ya kutoka Manyovu

Source: Tegemea Champanda
 
Back
Top Bottom