Ifahamu dola ya Maya iliyooneshwa kwenye filamu ya Mel Gibson "Apocalypto"

clinician

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
1,661
3,562

Miaka kadhaa tangu kutolewa kwa filamu ya Apocalypto(mwaka 2006),bado nimeguswa kuandika makala yangu ya kwanza kwenye blogu hii kuhusu filamu hiyo.Ninaipenda sana filamu hii.

Mel Gibson na Farhad Safinia ndio walioiandika Apocalpto.Wawili hawa walikutana kwenye matengenezo ya mwisho mwisho ya filamu nyingine nzuri iitwayo The Passion Of Christ,huko walipata muda wa kuzungumzia mapenzi yao kwenye mambo ya filamu.

Mazungumzo hayo ndiyo yalizaa wazo kuu la Apocalypto"mtu akikimbia kuokoa maisha yake,wakati huo huo akikirudia kitu anachokithamini mno"

Shauku ya kuonesha na kupitia utamaduni wa kizamani zaidi katika uhalisia wake kabla ya ujio wa wazungu,iliwafanya Gibson na Safinia kutumia dola ya zamani ya MAYA kwenye filamu ya Apocalpto.

Wasichokijua watu wengi ni kwamba mengi kati ya yaliooneshwa kwenye filamu ya Apocalpto ni mambo halisi kuihusu dola mashuhuri iliyopata kuwepo America ya kati(mexico ya sasa) miaka ya 2000BC,dola hiyo iliitwa MAYA.

Tamaduni nyingi zilizooneshwa kwenye Apocalpto, ni uhalisia wa tamaduni za WAMAYA halisi.Majengo ya piramidi yaliyooneshwa kwenye filamu,kilimo cha mahindi,kutoboa masikio,silaha za kijadi,kuishi katika jamii ndogondogo, lugha, na mfumo wa tarakimu ni miongoni mwa tamaduni halisi za Wamaya zilizooneshwa kwenye Apocalypto.

Kama ilivyooneshwa kwenye filamu,majengo ya piramidi ya WAMAYA ni ndogo kiasi ukilinganisha na zile za Wamisri.Watu wa make-up walifanya kazi nzuri kurefusha masikio ya waigizaji,kuyatoboa(kisanii tu,sio kiuhalisia) na kuyawekea plug ili wafanane na WAMAYA HALISI

Silaha zilizooneshwa kwenye Apocalpto ni za kutengenezwa na msanii wa kiingereza Simon Atherson ambaye kabla alizisoma na kuzifanyia tafiti silaha halisi za WAMAYA.

Kwenye filamu ya Apocalypto,mke wa starring(yule mjamzito) aliigiza kwa jina la Seven,alikuwa na tatuu kwenye mkono wake wa kushoto iliiyoonekana kama kamstari kalikolala na nukta mbili juu yake,hiyo ni alama ya namba saba kwenye mfumo wa tarakimu wa WAMAYA halisi
Lugha iliyotumika kwenye filamu ni KIMAYA cha Yucatec(zipo lugha za Kimaya za aina nyingi) lugha hizi bado zinazungumzwa mexico mpaka sasa.

Lengo la waandaaji wa filamu ya Apocalypto ni kuionesha dola ya MAYA kipindi ambacho ilikuwa inaanguka,dhana hii imebebwa na kukauka kwa mahindi(ukame),ugonjwa wa tauni(rejea kwenye filamu baada ya kuchukua mateka,msafara ulikutana na binti mwenye tauni ambaye alitoa utabiri fulani).

Katika uhalisia wake majanga ya asili na magonwa siyo miongoni mwa vitu vilivyosababisha dola ya MAYA kuanguka
Moja kati ya mafumbo makubwa ya kihistoria ni jinsi gani dola ya MAYA ilipotea,hakuna ushahidi wowote unaoelezea kupotea kwa dola ya MAYA.Hakuna historia ya kushindwa vitani au majanga ya asili(Anaandika Gerald Leinwand kwenye kitabu cha The Pageant Of World History)

Japo ilikwisha potea miaka ya 250 AD (maandishi hutofautiana) mapiramidi ya WAMAYA yanasimama msituni mpaka leo,vizazi vyake bado vinaishi mpaka sasa.

Hata hivyo kafara ya binadamu iliyooneshwa kwenye filamu ya Apocalypto si utamaduni wa kawaida wa WAMAYA halisi bali ni utamaduni wa kawaida sana wa Dola ya Aztec ambayo Gibson na Safinia(watunzi wa filamu) waliwahi kuifikiria kuitumia kwenye filamu ya Apocalypto kabla ya kuamua kutumia MAYAN CIVILIZATION

SALUTE COMRADES

Hii mijengo hapa chini ni mijengo iliyojengwa miaka mingi zaidi kabla ya Kristo, enzi hizo teknolojia ya usafiri ilikua chini!

Swali ni je, nani aliyezunguka bara moja kwenda lingine kusambaza hii teknolojia?

Ikumbukwe mpaka leo hii mzungu hajaweza gundua haya majengo yalijengwa vipi. Yapo bara la Africa, Asia na America.

IMG_20180419_184354.jpg

Pia tujiulize kwanini yote yamejengwa na milango mitatu na mmoja mkubwa wa katikati? Nini maana yake? Nini maana ya namba 3?

Leonardo Da'Vinci katika mchoro/picha yake inayofahamika kama The Last Supper, pia ameweka hiyo milango mitatu!

FB_IMG_1517049322221.jpg
 
Swali la msingi..
Kama mya ilikua Mexico..Mazingira ya muvi ya Apocalypto yanaonyesha Jaguar paw alikua anaishi kwenye misitu iliyopo Amazon. Amazon ipo America Kusini. Je alikimbia kutoka México mpaka brazil au argentina au nchi yoyote ile amabayo kuna msitu wa amazon?

I need Clarification
 
Umeandika vizuri ila hakuna paragraph umebananisha..
Btw Dunia hautakuja kupata Dola imara tena kama zilivyokuwa Roma,Mayan,Greek,Bababeli na Misri...
Ukiangalia Ustaarabu mkubwa duniani tunaiga kutoka kwa hao watu Hasa Misri,Roma na Maya.
Asante mkuu,hii niliandika kwenye blog fulani kipindi cha nyuma,nimefanya ku-copy na ku-paste hapa...imeniwia vigumu kuipangilia tena sababu ya device ninayotumia sasa..
 
Swali la msingi..
Kama mya ilikua Mexico..Mazingira ya muvi ya Apocalypto yanaonyesha Jaguar paw alikua anaishi kwenye misitu iliyopo Amazon. Amazon ipo America Kusini. Je alikimbia kutoka México mpaka brazil au argentina au nchi yoyote ile amabayo kuna msitu wa amazon?

I need Clarification
Kwa uelewa wangu apocalypto imefanyiwa shooting southern mexico,kijiji alichokuwa anaishi jaguar paw kilikuwa kwenye misitu ya mexico na sio amazon.
 
Miaka kadhaa tangu kutolewa kwa filamu ya Apocalypto(mwaka 2006),bado nimeguswa kuandika makala yangu ya kwanza kwenye blogu hii kuhusu filamu hiyo.Ninaipenda sana filamu hii.
...
Wasichokijua watu wengi ni kwamba mengi kati ya yaliooneshwa kwenye filamu ya Apocalpto ni mambo halisi kuihusu dola mashuhuri iliyopata kuwepo America ya kati(mexico ya sasa) miaka ya 2000BC,dola hiyo iliitwa MAYA.

Tamaduni nyingi zilizooneshwa kwenye Apocalpto, ni uhalisia wa tamaduni za WAMAYA halisi.Majengo ya piramidi yaliyooneshwa kwenye filamu,kilimo cha mahindi,kutoboa masikio,silaha za kijadi,kuishi katika jamii ndogondogo, lugha, na mfumo wa tarakimu ni miongoni mwa tamaduni halisi za Wamaya zilizooneshwa kwenye Apocalypto.

Moja kati ya mafumbo makubwa ya kihistoria ni jinsi gani dola ya MAYA ilipotea,hakuna ushahidi wowote unaoelezea kupotea kwa dola ya MAYA.Hakuna historia ya kushindwa vitani au majanga ya asili(Anaandika Gerald Leinwand kwenye kitabu cha The Pageant Of World History) .....
Asante kwa kuleta hapa topic hii ambayo nimependa tangu muda mrefu. Sijaona filamu, wala sijui kitabu cha huyu G. Leinwand.
Ila tu kuhusu Wamaya - hapakuwa na dola moja la Wamaya. Wamaya walikuwa na madola mengi madogo na kila dola liliongozwa na mji fulani na mtawala wake walioshindana kati yao na kupiga vita mara kwa mara. Mwisho wake ulikuwa uvamizi wa Wahispania waliohitaji karibu karne mbili kuwashinda Wamaya.

The Maya civilization developed in an area that encompasses southeastern Mexico, all of Guatemala and Belize, and the western portions of Honduras and El Salvador.
The period c. 2000 BC to 250 AD saw the establishment of the first complex societies in the Maya region, and the cultivation of the staple crops of the Maya diet, including maize, beans, squashes, and chili peppers. The first Maya cities developed around 750 BC, and by 500 BC these cities possessed monumental architecture, including large temples with elaborate stucco façades. Hieroglyphic writing was being used in the Maya region by the 3rd century BC.
In the 9th century AD, there was a widespread political collapse in the central Maya region, resulting in internecine warfare, the abandonment of cities, and a northward shift of population.
In the 16th century, the Spanish Empire colonised the Mesoamerican region, and a lengthy series of campaigns saw the fall of Nojpetén, the last Maya city, in 1697.
(Nimefupisha kutoka Maya civilization - Wikipedia, makala yenye marejeo mengi ya kitaalamu)

Nahisi kile unachorejela kuwa "mwisho wa dola la Maya" ni kipindi kile katika karne ya 9 BK ambako miji mingi katika kanda la kati ya Wamaya iliachwa na wakazi wao . Hata hivyo, utamaduni wa Wamaya uliendelea kwa nguvu kabisa katika maeneo mengine hadi kuja kwa Wahispania.
 
Asante sana mkuu kwa mchango mzuri,nimejifunza kitu.Tafuta filamu uitazame naamini utaipenda.
 
Back
Top Bottom