benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Idadi ya wageni wanaoshuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), imeongezeka kutoka 300 hadi kufikia 2000. Ongezeko hilo limechangiwa na Filamu ya The Royal Tour iliyoigizwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha KIA (KADCO).
Christina Mwakatobe, wakati wa hafla ya kuwapokea watalii 54 kutoka nchini Ugiriki waliofika kwa mara ya kwanza.
Alisema idadi ya watali imeendelea kuongezeka kwa kasi kutoka watalii 780.000 mwaka 2019 kabla ya UVIKO 19 hadi 927.000 mwaka wa fedha 2022/2023 ikiwa ni ongezeko la asilimia 42.
Alisema: "Sasa hivi uwanja huu tunashuhudia makundi makubwa va watalii, kwa siku moja hadi watali 2,000 jambo linaloonyesha matokeo chanya ya kutangaza vyema utalii nje kutokana na Filamu ya The Royal Tour"
Aidha alisema kuna mashirika va ndege yameongeza idadi ya miruko sambamba na uwapo wa ndege za watali binafsi wanaokuja kutembelea vivutio.
Wakala wa utalii ambaye ameleta watalii hao kutoka Ugiriki, Manasse Kidman, alisema watalii hao watakaa kwa muda wa siku tatu na wanatarajia kwenda maeneo mbalimbali ikiwamo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mmoja wa watalii hao, Christos Gianakopoloulos, alisema matarajio yake ni kuona wanyama wakuu watano ambao aliambiwa Tanzania ni rahisi kuwaona kuliko nchi nyingine yeyote.