buhange
JF-Expert Member
- Oct 23, 2011
- 505
- 110
Habari zenu wana JF.
Nimevutiwa kuanzisha thread hii baada ya swala hili kuletwa kama maada katika gazeti la THE CITIZEN la tar. 28 june 2014. Baadhi ya wasomi katika taaluma ya fedha wameilalamikia BOT kwa kuweka kiwango kidogo cha Tsh. 12 bilioni kama kiwango kwa taasisi ya fedha kupata banking lisence kama Commercial bank na Tsh. 2 bilioni kuwa Community bank, wengine wakisema hakuna haja ya kuwa na utitili wa benki 53 wakati asilimia kubwa ya watanzania wakiishi chini ya dola 2 kwa siku.
Lakini pia wengne wakaenda mbali kwa kutolea mifano nchi kama Nigeria ambayo miaka kumi iliyopita ilikuwa na jumla ya benki 83 huku uchumi wake ukiwa mbovu, huku kwa sasa ikibaki na benki 22 licha ya kiwango kizuri ilichonacho cha uchumi.
Mtanzania mwenzangu, unasemaje juu ya hili, benki zikipungua idadi ushindani utakuwaje!, vipi kuhusu hali ya mikopo kwa watanzania maskini?
Karibu kwa maoni wadau.