Ndibalema
JF-Expert Member
- Apr 26, 2008
- 10,956
- 4,648
Hilo ni pembeni ya suala la sera. Watanzania mnapenda kupewa maneno matamu ya kuwaambia "tutaanzisha mchakato" au "serikali iko mbioni". kwa upande wangu nadokeza tu kuwa kama watu ninaowaunga mkkono wataingia madarakani kuna vitu vya kwanza ambavyo vitatakiwa kufanya. Na kubwa ni kuwatia pingu na kuwafungulia mashtaka baadhi ya viongozi na wengine wenye kuenjoy sijui immunity watavuliwa. HIli lisiwe na utata. Sasa linaweza lisiwe zuri kujulikana lakini litawekwa kwenye sera mapema na kwenye ilani ya uchaguzi. Watanzania watatakiwa kuwachagua wagombea wetu kwa misingi hiyo.
Sasa kama mnataka kuendelea na kamati za uchunguzi na tume za Rais.. endeleeni na CCM.. au chama kingine cha upinzani. Tunajua kwanini wanaogopa kukipa CCJ usajili wa kudumu but the train has already left the station..
Hivi ni nani mwenye mamlaka ya kuwavua imunity?
CCJ ikishaingia madarakani haiwezi kuwavua immunity? na kama inawezekana ningependekeza na hilo liwekwe kwenye sera mapema.
Mwanakijiji hukiamini chama kingine chochote cha upinzani zaidi ya CCJ? kwa nini?