Huyu ndio Mzee Kingunge

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
232
653
Pichani ni Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mke wake Peras Kingunge Enzi za Ujana wao.

Duru za historia zinasema Kingunge alikuwa muumini mzuri sana wa dini ya kikristu na wakati anasoma alisoma seminari, baadae alikuja kuhitilafiana na dini kutokana na misimamo yake ya kukinzana na misingi ya dini na hii ilitokea baada ya kurudi nchini akitokea Urusi alipokwenda masomoni. Hivyo rasmi akatangaza kuwa mpagani ( mtu asiyekuwa na dini ) wakati alipokuwa akiapishwa kushika wadhfa wowote serikalini yeye hakuwa anashika kitabu chochote cha dini wakati wa kula kiapo bali katiba ya nchi pekee kwa sababu alikuwa mpagani.

Kwa sasa Mzee Kingunge pamoja na Mke wake wote ni Marehemu na walifariki mwaka 2018 baada ya kushambuliwa na Mbwa. Vifo vyao viliibua hisia za watu wengi sana kwani walipishana mwezi mmoja tu, mke wake alitangulia kufariki Januari na Mzee Kingunge alifuatia February.

Mbwa waliofanya tukio walikua wa kwake mwenyewe anawafuga nyumbani. Walikua wanamfahamu mlinzi tu kwani ndio alikua akiwahudumia. Hawakumfahamu au kumzoea mtu mwingine hapo nyumbani. Asubuhi na mapema mlinzi anawarudisha tena kwenye banda lao ndio watu waweze kutoka. Mzee Kingunge alikua na utaratibu wa kwenda mazoezi asubuhi baada ya kuwasiliana na mlinzi wake kwamba tayari kashafunga/rudisha mbwa bandani.

Sasa siku ya siku Mzee alitoka kama kawaida alfajiri kwenda mazoezini kumbe hajawasiliana na mlinzi wake na mbwa hawajafungwa.

Walipomuona tu kwa mbali wakamkimbia mlinzi na kuanza kumshambulia, mlinzi alijaribu kumnusuru mzee ila mbwa walimzidi nguvu kutokana na ukubwa wao.

Mpaka watu wengine wanafika kutoa msaada tayari mzee alikua amejeruhiwa sana hususani tumboni Wakati Mke wake anafariki Kingunge alikuwa yupo Mahututi kitandani akiwa ametoka kufanyiwa Upasuaji.

Mtoto wa Kingunge aliwaambia wanahabari " Mama yetu ameshafariki lakini bado hatujamwambia Baba kwa sababu ndiyo ametoka tu kwenye Chumba cha Upasuaji, tunategemea akiamka Usingizini tumwambie kwamba mke wake amefariki".

Msiomfahamu Kingunge alikuwa ni mwanasiasa mkongwe ambaye alikuwa na kadi namba 4 ya CCM. Mwaka 2015 alitangaza kukiunga mkono Chama cha CHADEMA wakati Lowasa anagombea urais.

Wakati wa pumzi yake ya mwisho, mzee Kingunge aliomba msamaha na kurudi kwenye dini yake ya awali ya Kikristu (ukatoliki)

Nawakaribisha ambao hamjanifollow kunifollow ili tujifunze.

Even Nassary
 
Hakuna boss yeyote duniani asiyependa kufaham mbwa wake, kiufupi tu ni kwamba alibadilishiwa mbwa
Sio kweli wale mbwa wana kijana ndie alikuwa anawapa chakula na kuwafungua na kuwafunga hivyo kijana alichelewa kufunga asbh akifanya usafi mabandani
 
Ila na nyie ukisasa wenu umewafanya muwe wajinga na wapuuzi wa kutupwa. Ukisasa, mikogo, na kuiga-iga maisha ya mbele (ughaibuni) kunazidi kutufanya sisi Waafrika mazezeta wa kutupwa. Mbona zamani watu walikuwa hawauawi na mbwa wao wenyewe?

Mwezi uliopita, nilimdrop mwanakamati ya harusi mwenzangu nyumbani kwake usiku tukitoka harusini. Kumbe jamaa ana mimbwa hatari sana, mikubwa kama ndama na ni mikali hakuna mfano. Basi bwana, tulipofunguliwa geti ikaja mbio na vi-puppies vyao, mwenyeji wangu akanionya nisithubutu kushuka kwenye gari la sivyo yatanikuta ya Kingunge Ngombare. Kusema kweli hata bila ya yeye kunipa tahadhari nisingeshuka. Wale mbwa walionekana kunitamani sana wanijeruhi.
 
Ndo maana nikienda nyumba za WABOPA mkono unakaa sambamba na mguu wa kuku akijanganya mbwa na mwenye mbwa wote nawamwagia mwaniiii
 
Pichani ni Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mke wake Peras Kingunge Enzi za Ujana wao.

Duru za historia zinasema Kingunge alikuwa muumini mzuri sana wa dini ya kikristu na wakati anasoma alisoma seminari, baadae alikuja kuhitilafiana na dini kutokana na misimamo yake ya kukinzana na misingi ya dini na hii ilitokea baada ya kurudi nchini akitokea Urusi alipokwenda masomoni. Hivyo rasmi akatangaza kuwa mpagani ( mtu asiyekuwa na dini ) wakati alipokuwa akiapishwa kushika wadhfa wowote serikalini yeye hakuwa anashika kitabu chochote cha dini wakati wa kula kiapo bali katiba ya nchi pekee kwa sababu alikuwa mpagani.

Kwa sasa Mzee Kingunge pamoja na Mke wake wote ni Marehemu na walifariki mwaka 2018 baada ya kushambuliwa na Mbwa. Vifo vyao viliibua hisia za watu wengi sana kwani walipishana mwezi mmoja tu, mke wake alitangulia kufariki Januari na Mzee Kingunge alifuatia February.

Mbwa waliofanya tukio walikua wa kwake mwenyewe anawafuga nyumbani. Walikua wanamfahamu mlinzi tu kwani ndio alikua akiwahudumia. Hawakumfahamu au kumzoea mtu mwingine hapo nyumbani. Asubuhi na mapema mlinzi anawarudisha tena kwenye banda lao ndio watu waweze kutoka. Mzee Kingunge alikua na utaratibu wa kwenda mazoezi asubuhi baada ya kuwasiliana na mlinzi wake kwamba tayari kashafunga/rudisha mbwa bandani.

Sasa siku ya siku Mzee alitoka kama kawaida alfajiri kwenda mazoezini kumbe hajawasiliana na mlinzi wake na mbwa hawajafungwa.

Walipomuona tu kwa mbali wakamkimbia mlinzi na kuanza kumshambulia, mlinzi alijaribu kumnusuru mzee ila mbwa walimzidi nguvu kutokana na ukubwa wao.

Mpaka watu wengine wanafika kutoa msaada tayari mzee alikua amejeruhiwa sana hususani tumboni Wakati Mke wake anafariki Kingunge alikuwa yupo Mahututi kitandani akiwa ametoka kufanyiwa Upasuaji.

Mtoto wa Kingunge aliwaambia wanahabari " Mama yetu ameshafariki lakini bado hatujamwambia Baba kwa sababu ndiyo ametoka tu kwenye Chumba cha Upasuaji, tunategemea akiamka Usingizini tumwambie kwamba mke wake amefariki".

Msiomfahamu Kingunge alikuwa ni mwanasiasa mkongwe ambaye alikuwa na kadi namba 4 ya CCM. Mwaka 2015 alitangaza kukiunga mkono Chama cha CHADEMA wakati Lowasa anagombea urais.

Wakati wa pumzi yake ya mwisho, mzee Kingunge aliomba msamaha na kurudi kwenye dini yake ya awali ya Kikristu (ukatoliki)

Nawakaribisha ambao hamjanifollow kunifollow ili tujifunze.

Even Nassary
Kingunge hakuwahi kurudi kwenye ukristo.

Hayo madai ya kusema kingunge alirudi kwenye ukristo yalitokea baada ya yeye kufariki hivyo walikuwa wanatafuta namna ya kumzika na kumzika kipagani waliona haiwezekani ndipo waliposingizia hilo suala.
 
Back
Top Bottom