Huyu ndio baba aliemzika mwanae hai -Mbeya

SAKATA LA BABA ALIYEMUUA MWANAE JIJINI MBEYA KWA KUMZIKA AKIWA HAI




30032013935.jpg

Marehemu Debora Riziki miaka 3 enzi za uhai wake
img_0793.jpg

Riziki Mwangoka kulia anaetuhumiwa kumzika mtoto wake akiwa hai
img_0776.jpg


img_0767.jpg

Hapa maiti ya mtoto Debora ikiwa imetolewa nnje mara baada ya kufukuliwa ndani ya nyumba ya baba yake mzazi
img_0787.jpg

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI TUNAZOZIONYESHA
img_0786.jpg


img_0788.jpg

Mwili wa marehemu Debora ukionyeshwa kwa mzazi na kudhibitisha kuwa ndiye mwenyewe aliyemfukia
img_0791.jpg

Mwili wa mtoto Debora ukiandaliwa kwa kuzikwa kwa heshima zote
img_0795.jpg
img_0796%25231.jpg

Mwili wa Debora tayari kwa kuzikwa
dscf2009.jpg

Hatimae sasa Debora anazikwa
dscf2010.jpg
img_0802.jpg

Mara tu baada ya mazishi baba mzazi wa Debora anapelewa kituo cha polisi Tukuyu
img_0803.jpg
img_0804%25231.jpg


DSC00023.JPG

Mama mzazi wa marehemu Debora asimulia kisa chote
DSC00027.JPG

Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili
DSC00029.JPG

Bibi wa marehemu Debora
DSC00030.JPG
DSC00060.JPG

Tukiwa na baadhi ya waandishi wenzangu tukiendelea kupata historia fupi ya marehemu Debora toka kwa mama yake mzazi
DSC00035.JPG

Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.
DSC00042.JPG

Dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) kulia ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa anakumbuka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni.


“Nilitaka kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa masikitiko Neema.
DSC00051.JPG



MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .


Akizungumza kwa hisia kali, katika mahojiano maalumu na Mbeya yetu kijijini kwake Ibula, katika kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili.


Alisema tukio la mzazi mwenza huyo kumwiba mtoto na kwenda kumfanyia ukatili huo wa kinyama lilikuwa la pili, baada ya awali kumuiba akiwa na miaka miwili na miezi mine na alimrudisha kwa maandishi ya serikali ya kijiji.


Alisema katika tukio la kwanza la mtalaka wake huyo kumuiba mtoto wao huyo, lilitokea Septemba mwaka 2012, baada ya wiki chache za kumfukuza katika nyumba waliyokuwa wakiishi katika kitongoji cha Iponjola, kijiji cha Asenga, nyumba iliyotumika kuzikwa mtoto huyo.


Alitaja sababu za yeye kufukuzwa ni ugomvi uliotokana na yeye kuhoji sababu za kuficha fedha kiasi cha sh. 120,000 zilizotokana na wao kwa pamoja kufanya kazi ya kibarua katika mashamba kijijini hapo na baada ya malipo kutolewa mtalaka wake huyo alionesha kiasi kidogo cha sh.80,000.


Alisema ugomvi huo ndio ulisababisha yeye arudishwe kwa wazazi wake, lakini baada ya muda mfupi mwanaume huyo alimfuata na kumbembeleza ili warudiane na alipogoma aling’ang’ania aondoke na mtoto .


“Nakumbuka ilikuwa Novemba mwaka jana baada ya mimi kuondoka nyumbani kwake na kurudi kuishi hapa nyumbani, siku hiyo tukiwa shambani huyo bwana alikuja hapa nyumbani na kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema Steven ) niliyezaa na mwanaume mwingine” alisema Mwambenja.


Alisema baada ya kufika eneo hilo majira ya saa mbili asubuhi alitumia ujanja na kufanikiwa kumuiba mtoto na kisha kutokomea naye kijijini kwao Asenga, hali ambayo ilisababisha kutoa taarifa kituo cha polisi Kiwira.


“Unajua kuwa baada ya kwenda kutoa taarifa polisi walitusaidia kufika kijijini kwao ambapo serikali ya kijiji ilikubali nimchukue mwanangu kwa kuwekeana mkataba wa kisheria kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa chini ya miaka saba”.


Aliongeza kuwa Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.

Tukio la pili la kuiba mtoto.


Alisema tukio hilo lilitokea Novemba 29 mwaka jana 2012, ambapo alifika nyumbani kwao majira ya saa 12 :00 na kumkuta dada wa marehemu kumchukua mtoto akimdanga kuwa anaenda kusenya kuni eneo la jirani.


Aliongeza kuwa baada ya kuona dada wa marehemu anang’ang’ania kwenda wote alimuamuru arudi nyumbani kuchochea moto kwa kuwa kulikuwa kumeinjikwa mboga na kukubali kurudi.


“kwa mujibu wa maelezo ya mwanangu huyu wa kwanza alisema baada kurudi toka ndani, alikuta baba yake huyo ameondoka na mtoto na tuliporudi na kupokea taarifa hizo tulichanganyikiwa na kuanza kuhangaika hovyo” alisema mama wa marehemu.


Mwambenja alisema kuwa baada ya kucha siku ya pili asubuhi yake walienda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kiwira ili waweze kupata msaada wa kumtafuta, huku wakionesha barua ya makubaliano ya awali ya yeye kuwa na haki ya kisheria ya kusimamia malezi ya mwanao hadi afikishe miaka saba.


Alisema baada ya kutoa taarifa hizo kituoni hapo, askari aliyekuwa zamu siku hiyo alimtaka kutoa kiasi cha shilingi 50,000 ili fedha hizo wapewe askari mgambo wa kwenda kijijini kwa mzazi mwenzake huyo, kwani tayari walikuwa na taarifa kuwa alikuwa amekimbilia huko.


“Kutokana na hali ngumu ya maisha tulikosa kiasi hicho cha fedha hivyo suala hilo kubaki bila msaada wa polisi na pia hatukuweza kwenda kwa kijijini kwao”.


Aliongeza “sababu ya mimi kuwa mzito kuendelea kumfuatilia kijijini kwao kwa mara ya pili ili kujua kama yupo huko na mtoto ilitokana na hofu niliyoijenga, kwani awali tukiwa kwenye ugomvi alitamka maneno ya vitisho kuwa endapo nitaendelea kung’ang’ania kumchukua mtoto pale anapomchukua atakuja kumuua ili tukose wote”.


Hata hivyo mama huyo mzazi wa Debora, alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo, aliendelea kuwasiliana na wifi yake , Bupe Mwangoka,ambaye ni dada mkubwa wa mume wake anayeishi eneo la Isanga Jijini mbeya, ambaye ndiye alisaidia kwa kiasi kikubwa kubainika kwa unyama aliofanya.

Maisha kabla ya tukio.


Akielezea maisha yao kabla ya kutengana na baadae kuamua kufanya ukatili huo, alisema aliwahi kumtamkia maneno makali wakati akiwa na ujauzito wa miezi nane .


Alisema baada ya kuibuka ugomvi katika kipindi hicho, mwanaume huyo alimtaka kwenda kuiuza mimba ile kwa mwanaume mwingine yeyote atakayempenda ili asije akazaa mtoto ambaye atachanganya damu ya koo hizo mbili.


“Maneno yale katika kipindi hicho sikuyatilia maanani kwani nilifikiri zilikuwa ni hasira, lakini leo hii ndio najua maana ya ile kauli ” alisisitiza Mwambenja.


Hata hivyo alisema inashangaza kwani kuna wakati tukiwa katika maisha ya kawaida kabla ya yeye kufanya tukio hilo, mara kadhaa alijutia na kuonya juu ya matukio machafu yaliyojitokeza na kusikika ya watu kuuawa au kuondolewa baadhi ya viungo vya miili yao.


Aidha, alieleza mkasa mwingine wa mume wake huyo ni ule wa wao kufukuzwa katika mji wa Kiwira walikokuwa wakiishi awali kwa kufanya shughuli za umachinga.


Alisema walitimuliwa na serikali ya mtaa katika mji huo kutokana na mumewe huyo kutuhumiwa kuiba simu ya mkononi ambapo alipokea kipigo kikali na baadae kufukuzwa.


Kutokana na hali hiyo, mama wa marehemu Debora alisema yote yaliyotokea amemwachia mungu na kwamba kama ingekuwa uwezo wake angeamuru naye anyongwe, hivyo mamlaka husika zitajua cha kufanya.


Kwa upande wake dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa anakumbaka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni.


“Nilitaka kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa masikitiko Neema.


Hata hivyo uchunguzi wa Mbeya yetu umebaini kuwa marehemu Debora alifariki dunia siku hiyo ya Novemba 29 mwaka jana, majira ya saa nne usiku baada ya baba yake kufanikiwa kumuiba kutoka nyumbani kwa mama yake.


Inadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kumtorosha baba huyo wa marehemu alitembea kwa mguu umbali wa kilomita 50 kutoka kijiji cha Ibula alikomuiba hadi nyumbani kwake kijiji cha Isange katika kata ya Isange.


Imeelezwa kuwa baada ya kufika nyumbani kwake, baba huyo mzazi wa marehemu alichimba shimo katikati ya sebule na kumchukua mtoto wake huyo akiwa usingizini na kisha kumfukia akiwa hai.


“Mwanaume Yule alikuwa katili sana, kwani baada ya kumfukia alichukua meza ya chakula na kuiweka juu yake huku akiipamba kwa magazeti jambo ambalo lilifanya ndugu zake wasigundue kirahisi” alisema mpasha habari.


Chanzo hicho kilisema baada ya kufanya hivyo aliishi kwa wiki moja na baadae kukimbilia Jijini Mbeya ili watu wasibaini juu kitendo alichofanya na kwamba kila alipohojiwa na ndugu zake alisema mwanae huyo alimuweka kwa rafiki yake Jijini Mbeya.


Hata hivyo baada ya danadana za muda mrefu ndipo dada wa mtuhumiwa huyo aliamua kutoa taarifa jeshi la polisi na kufanikiwa kumkamata akiwa katika harakati za kutorokea wilayani Chunya na alipobanwa alifichua siri ya alipo mwanae kwa kueleza kuwa alimuua na kumfukia ndani kwake.




Joseph Mwaisango
Ezekiel Kamanga
na
Venance Matinya
http://freebongo.blogspot.com/2013/04/sakata-la-baba-aliyemuua-mwanae-jijini.html
 
Now you're making some sense best...
Maana hukuweka sosi mwanzoni ndio maana nikawa na hamu ya kukuchimba...
Ndio maana nakupendaga tuuu!!!

tatizo lako umepata taarifa hapa hapa tu kuwa curious to know more about ,mimi sijaipata hii taarifa hapa tu nimepita zaizi ta blog 3 ndio sababu nsema hivyo
nenda mbeya yetu blog-anaitwa
BABA WA MAREHEMU:
RIZIKI MWANGOKA
MAMA YAKE ANAITWA
, Esther Mwambenja,
MWENYEKITI WA KIJIJI:
Lutengano Mwakyoma

sasa utakkuwa umenielewa vizuri
 
mhhhhhhhhh jamani haya mambo hata cha kusema sina! huko SIngida nako kuna mama kamcharanga mwanae mapanga - sijui ni akili mbovu au ni nini!!!?!??!
 
Inasikitisha sana. Huyu jamaa akapimwe kama ana matatizo ya akili. Kama sio hivyo, atakuwa ni mshirikina. R. I. P Debora.
Hivi kwa nini tukimbilie kupima... Ashitakiwe... Nashauri, kama tulivyo na magereza ya watoto watukutu, au kama tulivyo na hospitali ya mirembe... TUWE NA MAGEREZA YA WASIO NA AKILI
 
Nivea, I am shocked,,what the hell!! Whats wrong with that little one? These people now....I am tired of them. Is not the same region where the innocent Anet was stubbed? and all these were baby girls. This man deserves to be treated like the way he didi to "his daughter".

nilimuonya sana mdogo wangu kuhusu mchumba wake wa huko mbeya mnyakyusa .akija uwawa sijui itakuwaje watu wa mbeya sio watu ,kulingana na huu msururu wa mauaji yakinyama ntamtimua yule bwana akileta mahari lol sitaki kuamini binadamu wa hivyo bora ukutane na simba mla watu akule na sio binadam kiumbe kibaya sanahiki. Thanda co me this way mbeya its not a good place to stay!!!
 
Last edited by a moderator:
nilimuonya sana mdogo wangu kuhusu mchumba wake wa huko mbeya mnyakyusa .akija uwawa sijui itakuwaje watu wa mbeya sio watu ,kulingana na huu msururu wa mauaji yakinyama ntamtimua yule bwana akileta mahari lol sitaki kuamini binadamu wa hivyo bora ukutane na simba mla watu akule na sio binadam kiumbe kibaya sanahiki. Thanda co me this way mbeya its not a good place to stay!!!

Usihukumu usijehukumiwa, watu wa mbeya sio watu ila ni mawe? iyo ni akili ya mtu iliyoshindwa kutanuka na si kabila wala rangi ya mtu. Haya nimatatizo ya kisaikolojia huwapata watu wengi tu wanapokosa msaada wa kiakili na mawazo katika maswala wanayofikiria bila kupata majibu. Usimkoseshe mwenzio penzi lake, wanaoua wachungaji na mapadri nao ni wa mbeya? Wanaofisadi nchi wote ni mbeya? Usiigawe nchi kwa mtazamo wako huyo ni mtanzania na sio mmbeya kama wewe unavyosema. Binadamu yeyote hata wewe waweza kugeuka na kuwa na hali hiyo kulingana na mwenendo wa kimwili, kwani hilo swala si la mtu mwenye akili timamu, hicho ni aina ya kichaa.
 
Last edited by a moderator:
Unyama mkubwa Huyu bwanaanastahili adhabu kubwa sana ili iwe fundisho kwa mababa wenye Tabia Kama yake!
 
nilimuonya sana mdogo wangu kuhusu mchumba wake wa huko mbeya mnyakyusa .akija uwawa sijui itakuwaje watu wa mbeya sio watu ,kulingana na huu msururu wa mauaji yakinyama ntamtimua yule bwana akileta mahari lol sitaki kuamini binadamu wa hivyo bora ukutane na simba mla watu akule na sio binadam kiumbe kibaya sanahiki. Thanda co me this way mbeya its not a good place to stay!!!

Baada ya kumkataza asiolewe na watu wa Mbeya ulimpelekea mwanaume uliyetaka aolewe naye? Unaweza kutupa idadi ya wanaume ulio waacha baada ya kuona kusikia matendo yaliyofanywa na watu wa makabila yao?
Mdogo wako ana akili sana, alishakupima na kuona mawazo yako yanapoishia. Yaani badala ya kujishughulisha kumfahamu mtu anayetaka kumuoa mdogo wako ili umsaidie wewe unaenda na story za kuambiwa ambazo hazimhusu mchumba wake huyo bali watu wengine?

Unadhani kabila utokalo wewe ni salama sana lisilo na matope?

Kwa taarifa yako ni kuwa huyo jamaa yupo driven na psycological disorders ambazo humpata mtu yoyote bila mipaka ya kikabila bali kwa hisia tofauti zitokanazo na masuala ya kiuchumi, kisiasa, mapenzi, kiroho n.k
Pi ni kuwa huna ulijualo kuhusu watu wa Mbeya.

Kuendelea kuwa mjinga ni uamuzi wako.

Soma hapa chini.

Je ni kweli alimuua Mkewe Mja mzito wa Miezi 8?
 
Baada ya kumkataza asiolewe na watu wa Mbeya ulimpelekea mwanaume uliyetaka aolewe naye? Unaweza kutupa idadi ya wanaume ulio waacha baada ya kuona kusikia matendo yaliyofanywa na watu wa makabila yao?
Mdogo wako ana akili sana, alishakupima na kuona mawazo yako yanapoishia. Yaani badala ya kujishughulisha kumfahamu mtu anayetaka kumuoa mdogo wako ili umsaidie wewe unaenda na story za kuambiwa ambazo hazimhusu mchumba wake huyo bali watu wengine?

Unadhani kabila utokalo wewe ni salama sana lisilo na matope?

Kwa taarifa yako ni kuwa huyo jamaa yupo driven na psycological disorders ambazo humpata mtu yoyote bila mipaka ya kikabila bali kwa hisia tofauti zitokanazo na masuala ya kiuchumi, kisiasa, mapenzi, kiroho n.k
Pi ni kuwa huna ulijualo kuhusu watu wa Mbeya.

Kuendelea kuwa mjinga ni uamuzi wako.

Soma hapa chini.

Je ni kweli alimuua Mkewe Mja mzito wa Miezi 8?
blabalabalabalablabaa nyingi ujumbe ushaupata ndugu yangu hata msichana wa kazi wa mbeya ni hatari sana nimekaa nao nimeona
 
Usihukumu usijehukumiwa, watu wa mbeya sio watu ila ni mawe? iyo ni akili ya mtu iliyoshindwa kutanuka na si kabila wala rangi ya mtu. Haya nimatatizo ya kisaikolojia huwapata watu wengi tu wanapokosa msaada wa kiakili na mawazo katika maswala wanayofikiria bila kupata majibu. Usimkoseshe mwenzio penzi lake, wanaoua wachungaji na mapadri nao ni wa mbeya? Wanaofisadi nchi wote ni mbeya? Usiigawe nchi kwa mtazamo wako huyo ni mtanzania na sio mmbeya kama wewe unavyosema. Binadamu yeyote hata wewe waweza kugeuka na kuwa na hali hiyo kulingana na mwenendo wa kimwili, kwani hilo swala si la mtu mwenye akili timamu, hicho ni aina ya kichaa.
:blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah: habari ndio hiyi!!!!
 
blabalabalabalablabaa nyingi ujumbe ushaupata ndugu yangu hata msichana wa kazi wa mbeya ni hatari sana nimekaa nao nimeona

Sawa nimeongea blah blah, unaweza ku highlight anya of what you call blah blah katika niliyoyaongea?mbona umekwepa kujibu hata moja ya maswali niliyokuuliza. Au ndiyo hata mdogo wako ulivyomjibu ulipompelekea story zako za vijiweni?
Huna unalolijua ni bahati si tu kuhusu watu wa Mbeya, bali maisha kwa ujumla, yaani unamkataza mdogo wako kuolewa kwa sababu ya story za salon? Halafu unamkataza jambo bila hata ya kumpa options ili apate way forwards....by the way huwa sina tabia ya kurefusha mada pale ninapoona hoja zinakwepwa.

What Matters is not what you have or what you hate and love, but what you do with what you got.

Maadam unaishi na kuchangamana na watu, kujifunza ni kati ya majukumu yako, lakini kuendelea kuwa mjinga ni uamuzi wako.
Enjoy your time.
 
Allah Akbar!

Yaani mtoto wake mwenyewe kamfanyia hivyo je mtu baki?

Huyu kwa hakika hastahili kuishi ni vema uhai wake na yeye uondolewe mara moja baada ya uchunguzi kukamilika na akitiwa hatiani kwa kosa hili. Si vyema kukaa rumande kusubiri adhabu ya Kifo huyu akishaonekana na hatia mheshimiwa atie saini tu.
 
huyo hana roho ya binadamu ana roho ya nguruwe

Nguruwe is far way. better compared to Uamsho, BokoHaram, Al Qaeda, wale wasomali sijui wanaitwaje, n the likes which are all Muslims. Pole yako with ur low thinkin capacity:thumbdown:
 
Back
Top Bottom