Huyu mwanamke muuaji

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,704
Ndugu wana jf, kuna mkasa umempata jirani yangu nataka ni share na nyie.
Kuna jirani yangu kaoa na ana watoto wawili. Pia ana mdogo wake wa kiume ambae naye pia kaoa. Siku za nyuma huyo mdogo wake wa kiume alikuwa akiishi peke yake pamoja na mkewe, ila maisha ya kawa magumu kiasi kwamba akashindwa hata lipia ela ya pango la nyumba maana jamaa anapenda sana starehe hadi anashindwa mtunza mkewe.
Mke wa jirani yangu akamuomba mumewe wamchukue mke wa mdogo wake waishi naye ili wampe muda jamaa kujipanga upya akiwa tayari ndo aje amchukue mkewe na kweli akaanza ishi pale.
Sasa tatizo ndipo likaanza, huyu mwanamke akaanza visa. Mke wa jirani yeye ni mfanya biashara uwa anaondoka asubuhi, akawa anategemea huku nyuma wifi yake atapika na kuwahudumia watoto wakitoka shule, lakini mambo yakawa sivyo yeye akiachiwa ela ya mboga ananunua bia na vocha watoto wanashinda njaa. Mama akiuliza jibu analopewa kwani mimi house girl wako.
Mambo yakaendelea na hali ikazidi kuwa mbaya visa kila siku mgeni kageuka simba, ikabidi mke wa jirani amweleze mumewe mumewe akasema mimi siwezi mfukuza mke wa mdogo wangu.
Sasa ya juzi ndiyo funga kazi, mama katoka katika mihangaiko kakuta ela aliyo acha kwa ajili ya chakula wifi yake kanunulia bia na na nyama choma amekaa kibarazani anaburudika. Mama kuona wanae wanalia njaa, chakula hakuna hasira ikampanda akamwaga bia ya wifi yake, kumbe shemeji yake naye alikuwa ndani (mme wake mwanamke mwenye bia) akatoka wakamchangia wakampiga na mbaya zaidi jirani akawa anashangilia mkewe anavyopewa kipigo toka kwa mdogo wake na mke wake.
Jambo hilo lilimuuma sana mke wa jiran yani kapigwa mbele ya mumewe basi akawa anasema yeye ndiye mama mwenye nyumba hataki tena kumuona mdogo wake mmewe na mkewe waondoke. Wakawa wanasema hawaondoki huku wakisimamiwa na jirani.
Ugomvi ukawa mkubwa baina ya jirani na mkewe, jana usiku wakawa wanapigana katika kurushiana vitu mke akawa anamrushia frame ya picha mumewe bahat mbaya ikampiga mtoto kichwani ikapasuka na vioo vikamchanachana mtoto vibaya na sasa hivi yuko muhimbili.
Ndugu wa upande wa mume wanasema mwanamke aondoke yani balaa tupu.
 
hapo inaonekana wote wanamatatizo ila hao walevi ndio yamezidi poleni kwa sinema zisizokuwa na malipo..
 
Kaa mbali na ndugu zako wasio na elimu na wanapenda starehe.
OTIS
 
OMG!!If any punk dares to lay his/her hand on my lady i'll surely crucify someone.
Hakuna wanaume hapo.Tena hapo kwenye suala la watoto ndio kabisa anaondoka siku hiyohiyo hata jua halitui.
 
Duuh hayo ni matatizo ya kuishi na ndugu...mimi nasema huyo mama mwenye nyumba hizo biasha ameanza lini kabla au baadaya ya kukaribisha hao ndugu kuishi nao. Kama ni kabla, watoto wake alikuwa anawaachia nani na mambo ya nyumbani kama upishi alikuwa akifanya nani kama baada naona hata huyo mke wa ndugu atakuwa na haki kusema kuwa kaletwa hapo kuwa housegal.

Ninachotaka kusema ni kuwa unaposaidia mtu isitegemee shukurani in return, kuna watu hawajui utu, huyo mama mwenye nyumba angepanga mambo ya nyumbani kwake regardless wale wapo au hawapo. Hii ingeondoa mzizi wa fitna.!
 
Huyu Mume ndio wale waume suruali,yani unashwindwa hata kufanya mamuzi,vyovyote itakavyo kua lazima mume usimame na mkeo kama kugombana ndani loooh asara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom