Huyu mwanamke kabadilika ghafla sana mpaka Namuogopa

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,494
99,262
Habari wakuu,
Kuna mwanamke nko nae kwny mahusiano mwaka wa 4 Sasa, amekua ananipasua kichwa balaa, nyuzi zake nyingi nmeleta sana humu nikitamani japo abadilike niweze kumuoa.

Ila kinachonishangaza Sasa,
Tangu mwezi wa 9 amekua na utulivu, adabu na heshima isiyo ya kawaida. Hii imenipa hofu, Kiufupi sijamzoea hivi. Hadi maji ya kunywa skuhizi anapiga magoti.

Jana nmeshangaa sn naenda kwake tukafanye, ananambia hayupo kaenda kanisani. Nikajua masihara, kweli nmemfata alikonielekeza nakumkuta kweli Yuko kanisani KKKT anasali.

Nmemnunulia bia anakunywa analamba lamba kwa hofu,utadhani ndo anajifunza pombe. Nnachojiuliza Hii hofu ya Mungu Sijui kaitolea wapi.

Kuna mda naamua TU kumchokoza nione Kama atabwatuka mbovu Kama alivozoea, ila naona hana mpango kabisa wa kunijibu. katulia na anatabasamu TU na kukiri kakosea nimsamehe wkt najua hamna alichokosea, nmefanya kusudi TU kumvuruga nimpime.

Naomba kuuliza,
wenzangu mshwahi pitia Hali Kama hii Mwanamke anabadilika ghafla bin vuu hivi? Au Ni mtego huo kuna pigo zito naandaliwa?

Wazoefu KE na ME, nambieni imekaaje Hii.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom