Huyu mbunge wa Nkenge mzima kweli?

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Namsikia hapa anatetea msafara wa Pinda kuwa na magari 50, kwani hata yeye akienda kijijini anapokelewa na pikipiki 50 na baiskeli 80. Anaendelea kusisitiza kwamba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi pindi viongozi waendapo mikoani, katika kuonesha kwamba wanawapenda viongozi.
 
Raia waendelee kujitokeza kwenye maandamano.....wasiogope.....na waendelee kuwahoj na kuwazomea viongoz waandamizi wa serikali....ambao wanendesha anasa
Namsikia hapa anatetea msafara wa Pinda kuwa na magari 50, kwani hata yeye akienda kijijini anapokelewa na pikipiki 50 na baiskeli 80. Anaendelea kusisitiza kwamba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi pindi viongozi waendapo mikoani, katika kuonesha kwamba wanawapenda viongozi.
 
Hahaha siasa hizi bana!

Mara wapinzani wanapotezea wananchi muda wa kufanya shughuli za kitaifa lakini huyu anataka wananchi wajitokeze kuwapokea viongozi wanapowatembelea... Tena anaona matumizi ya magari 50 hayana hasara yoyote!

Ahsante Mungu sipo Bungeni... vinginevyo
 
Alivyoanza kuchangia na kuongea maneno hayo mke wangu aka mute TV eti awezi kusikiliza upuuzi.
Nawabunge wengine wakapiga makofi.
kazi ipo inaone mbunge huyu aelewi kabisa
 
Huyo Mama Asumptha hana elimu hata ya Darasa la Nane,Amelelewa kwa kugawa chai kwenye ndege ya Rais (Mwalimu) na baadaye kuwa Mpishi Ikulu na Mlinzi wa first Lady.Hana lolote la maana la kuleta kwa wananchi wa Nkenge zaidi ya kutetea Ujinga uliopitwa na Wakati.Wabunge wa namna hii hawapaswi kurudi ktk Bunge lijalo.
 
Huyu mama si mzalendo wa nchi hii mimi ameniacha hoi pale alipowagusa wanafunzi wa UDOM eti ni watovu wa nidhamu wanastahili adhabu kwa kisingizio eti hata enzi za mwalimu alishafukuza wanafunzi UD.Tatizo huyu mama alikuwa mpishi unategemea nini kwa mtu huyu kama c pumba.
 
Mama kaniharibia jioni yangu huyu. Eti wanafunzi wanaogoma wafukuzwe walete wengine, hiv ccm ivo ndo staili ya kutatua matatizo iyo? Mbona mafisadi hamjawafukuzi? Mnawakumbatia tuu?
 
Huyo Mama Asumptha hana elimu hata ya Darasa la Nane,Amelelewa kwa kugawa chai kwenye ndege ya Rais (Mwalimu) na baadaye kuwa Mpishi Ikulu na Mlinzi wa first Lady.Hana lolote la maana la kuleta kwa wananchi wa Nkenge zaidi ya kutetea Ujinga uliopitwa na Wakati.Wabunge wa namna hii hawapaswi kurudi ktk Bunge lijalo.

Kama kutakuwa na wabunge wa vitu maalumu, hawa wataendelea kuwepo. Kitu muhimu tufanye mabadiliko ya katiba na kuondoa wabunge wa upendeleo kama viti maalumu na wakuteuliwa vinginevyo wataendelea kuwepo kwa gharama ya kodi zetu!
 
Maji marèfu ndo Mbunge ovyo kabisa yaani hajui anachochangia anaropoka tu anafikiria ubunge nikupiga Tunguli.
 
Mama kaniharibia jioni yangu huyu. Eti wanafunzi wanaogoma wafukuzwe walete wengine, hiv ccm ivo ndo staili ya kutatua matatizo iyo? Mbona mafisadi hamjawafukuzi? Mnawakumbatia tuu?
huyu mama anaamini kwamba wanafunzi wanachochewa, hapa anasahau kwamba serikali ndiyo inayofanya uchochezi
 
Namsikia hapa anatetea msafara wa Pinda kuwa na magari 50, kwani hata yeye akienda kijijini anapokelewa na pikipiki 50 na baiskeli 80. Anaendelea kusisitiza kwamba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi pindi viongozi waendapo mikoani, katika kuonesha kwamba wanawapenda viongozi.

Hawa ni wabunge wa chama cha Magamba!
 
Hahaha siasa hizi bana!

Mara wapinzani wanapotezea wananchi muda wa kufanya shughuli za kitaifa lakini huyu anataka wananchi wajitokeze kuwapokea viongozi wanapowatembelea... Tena anaona matumizi ya magari 50 hayana hasara yoyote!

Ahsante Mungu sipo Bungeni... vinginevyo
ungemrukia mtu kwa hasira
 
kuwa mwana-ccm yataka moyo
 
mkuu bunge niliacha kusikiliza tangu zamani. ile tabia ya wabunge wa ccm kumpigia makofi mbunge mwenzao hata kama ameongea utumbo inaniboa sana. ukweli ni kwamba hawa wabunge wa ccm hawana sera zenye mshiko kwahiyo wanapiga makofi hovyohovyo ile presence yao iwepo. la sivyo tutawasahau kama the extinct dynosous
 
Hahaha siasa hizi bana!

Mara wapinzani wanapotezea wananchi muda wa kufanya shughuli za kitaifa lakini huyu anataka wananchi wajitokeze kuwapokea viongozi wanapowatembelea... Tena anaona matumizi ya magari 50 hayana hasara yoyote!

Ahsante Mungu sipo Bungeni... vinginevyo

kumbe na wewe ni mshabiki?aisee!
 
Kama kutakuwa na wabunge wa vitu maalumu, hawa wataendelea kuwepo. Kitu muhimu tufanye mabadiliko ya katiba na kuondoa wabunge wa upendeleo kama viti maalumu na wakuteuliwa vinginevyo wataendelea kuwepo kwa gharama ya kodi zetu!
Rev.huyu mama ni mbunge wa kuchaguliwa ndo alimwangusha Doudurus Kamala aliyekuwa waziri wa EA Tatizo watu wa nkenge nao walikosa mpinzani makini baada ya mgombea wa CDM kuhongwa na kujitoa kwny kinyanganyiro matokeo yake jimbo likaenda kwa huyu *******
 
Kweli kazi ipo,hivi unaweza kutetea kweli haki za wananchi wako kwa mtindo huu? Unajua suala la kuwa mbunge ni suala nyeti sana,inabidi tuwe makini sana na uchaguzi wa wabunge wetu.

Watu kama hawa hawafai kabisa katika taifa letu,tunahitaji wazalendo wa kweli wenye kujua nini wanafanya na sio kufanya kwa matakwa yao.Huu ni ujinga kabisa kwani mbunge lazima umsifie PM ndio uonekane upo bungeni?

Please wabunge wetu amkeni usingizini.Nchi inawahitaji ninyi na michango yenu yenye manufaa kwa taifa na sio vinginevyo.

Mungu ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom