Huyu kijana nitamsaidiaje apate ajira?

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
Kuna kijana mmoja alitokea hapa kwenye kibarua changu akanielezea anahitaji ajira. Akaacha wasifu wake CV nikapitia nikaona ana degree Bachelor of Business Administration kwa mujibu wa CV. Sasa nikazungumza na mkuu wangu wa kuajiri akasema poa mlete tutamfanyia "interview", sasa nimewasiliana na huyu kijana anipe vyeti vyake alivyomalizia chuo na shule zote zlizopita. Bahati mbaya hana cheti cha chuo, yeye ameniambia hajapewa.

Nikaomba anipe japo yale majibu ya mwisho "Transcript" na yenyewe hana. Nikamwambia anipe vyeti vyoote alivyokuwa navyo nione tutafanyaje, sasa hapa akaniletea cheti Form Six ambacho amefaulu vizuri kunishinda hata mimi enzi zangu, pamoja na barua ambayo imeandikwa kama nilivyonukuu hapo chini. Je ungekuwa wewe ungefanyaje? Mind you kwamba nikimpeleka kule mwisho wa siku mimi nakuwa kama referee wake na ninampigia chapuo kama mtu ninayemjua ingawa hata simjui kabisa. Na kwa kifupi anaonesha anaitaka sana kazi.Na sijui alimaliza hicho chuo au aliishia kati. Hapa chini ni kama alivyoandika yeye sijaongeza sijapunguza hakuweka hata nukta moja au mkato na hakusaini.

I (His name) i am pursued batcher of business administrationat univesty of ........... here it is the letter to request to your that I will submit my universty results which is not found in my certificaties and I fail to submit it dut to the problems which I was faced after complete my final examination because my father was die so I was fail to wait for such cerificaties. Please Sir I beg you to accept my application. Im confident I will perform well if my application will be considered.

Yours

.....................

 
hata hicho cha form six inawezekana ni magumashi hebu kichunguze vyema


my father was die so

Duh hapo ni form six gani amemaliza aise Maundumula
 
Last edited by a moderator:
Itabidi umpeleke huko kwa bosi akajieleze mwenyewe kama amefoji hiyo degree itajulikana hukohuko!
 
Mwandikie barua, umpe asign then uipeleke kwa bosi.

Catherine,

Mwisho wa siku watamuweka mtu kati kwenye Interview atakuwa peke yake. Na akizingua wataanza kuulizana imekuaje huyu kaletwa hapa?
 
hata hicho cha form six inawezekana ni magumashi hebu kichunguze vyema


my father was die so

Duh hapo ni form six gani amemaliza aise Maundumula

Mr Rocky,

Hii kitu sijaielewa maana amemaliza katika mojawapo ya shule kongwe ya serikali ambayo hata mzee wangu alisoma.
 
Itabidi umpeleke huko kwa bosi akajieleze mwenyewe kama amefoji hiyo degree itajulikana hukohuko!

Unafikiri mimi nikimpeleka nikamtambulisha kama namfahamu vizuri nikaandika kabisa na reccomendation halafu wakabaini amefoji next time nikiwapelekea mtu mwengine watampokea?
 
Mr Rocky,

Hii kitu sijaielewa maana amemaliza katika mojawapo ya shule kongwe ya serikali ambayo hata mzee wangu alisoma.


Mkuu Maundumula chunguz ahicho cheti vyema
Kumaliza katika shule kongwe sio tija swali ni je alisoma kwenye hiyo shule kweli
Kuna vitu basic unaweza kumuuliza wewe mwenyewe maana umeenda shule ambavyo unaweza kupima uelewa wake wa mambo kabla hujampeleka hata kwenye interview
So chukua muda wako na kaa nae chini mfanyie interview ya kwako kwanza na then ndio ujihakikishie
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Maundumula chunguz ahicho cheti vyema
Kumaliza katika shule kongwe sio tija swali ni je alisoma kwenye hiyo shule kweli
Kuna vitu basic unaweza kumuuliza wewe mwenyewe maana umeenda shule ambavyo unaweza kupima uelewa wake wa mambo kabla hujampeleka hata kwenye interview
So chukua muda wako na kaa nae chini mfanyie interview ya kwako kwanza na then ndio ujihakikishie

Mr Rocky,

Umeongea la maana sana aisee, ngoja nikae nae chini nimsikilize pengine kiingereza cha kuongea anaweza vizuri kuliko kuandika. Au pengine ana vitu extra ambavyo nitaviona tu nikimuuliza maswali mengi mengi. Nitamu interview then nita update.
 
Mkuu ya nini kujitia aibu? huyo anaonekana ni magumashi mwanzo mwisho................ utaonekana mtu mzima ovyo na watu unaoheshimiana nao. Then next time utashindwa kupewa favour kwa sababu watajua 'huyu hana maana, ovyo tu'
 
Duh!! Luck is when opportunity meets quality and qualification. Granted, the young man is lucky to have you as a referee. But I just cant imagine a University graduate writing such a nauseating English!!!
 
Mkuu wangu Maundumula,
Be careful na huyo mtu......am convinced kwamba huyo mtu anafahamu anachokifanya; ole wako ama ole wenu mzani huyo jamaa ni kilaza! Si ajabu hata hapa anafuatilia thread hii!

Let's be honest...kwa mtu mwenye kiingereza kibovu kama hicho anatarajiwa awe hata form IV hajafika. Jiulize, ameitoa wapi confidence ya kujifanya ana degree ya Business Administration! I repeat, anafahamu anachokifanya! Kama huyo jamaa angejinadi kwamba ni Engineer, nisingeshangaa! Let's say alisema ni Mechanical Engineer...so hata kama hana degree ya hiyo fani basi ningehisi labda anajivuna yupo fit practically! c unajua mafundi wetu wa gereji bubu? Unakuta mtu hata FTC hana, lakini yupo fit mbaya! Lakini jamaa anasema ana BA!!! Ujasiri huo ameutoa wapi? Look here, Certificate hana; sawa! Ndo hata transcript?! Be careful broda, msije mkadondokewa na jumba bovu; jamaa yupo kazini huyo!
 
Kiingereza ni janga la taifa, kama kazi yenyewe itahusisha kiingereza hiyo barua tu mushkeli, achilia mbali hivyo vyeti.

Na hapa linaweza likawa suala kubwa zaidi ya Kiingereza.

Maana inaonekana ama hajui kama Kiingereza chake cha kuunga unga, ama anajua lakini kakosa hata akili ya kutafuta mtu (au hata computer) kufanya spellchecking and grammar correction, au anajua lakini ni mlipuaji.

Lakini labda ni kitu cha kawaida bongo mpaka kinazoeleka.Hata wewe mwenyewe mkuu umetaja vyeti tu hujataja hili kama issue (unless kuonyesha barua ilivyoandikwa ndo una solicit input).

Alikuja jioni kisomo mwingine earlier today anatafuta scholarship ya masters degree in Education na madubwana kochokocho.

Nikamwambia kwa kiingereza hiki bora tafuta scholarship ya English course kwanza.
 
Na kazi za siku hizi zinafanywa kwa kuambatana na outlook sijui itakuaje? Official mails ataandikaje maana zinatembea kwa kuweka watu kibao in copy, sasa si ndo kuaibishana huko
 
huyo anafafanana sana na zinduna binti aliyehojiwa na clouds tv anaulizwa kama umemaliza form 4 ulifanyia mtihani masomo mangapi? eti anajibu manne na alazimisha kabisa.mkuu huyo mtu atavuruga heshima yako
 
Mnashangaa nini wakati kuna watu wanaoshikilia nafasi za juu serikalini na kiingereza kinawpa shida.... tena wenginei wanajiita madaktari.................................!
Kama anaonekana ni mchapa kazi, mpe kazi bana achana na majungu........................LOL
 
Back
Top Bottom