huyu binti ana tatizo gani?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
habari yenu wana jf.huyu binti anaumia tumbo chini ya kitovu kila baada ya ku-do.nini tatizo na tiba yake?
 
Kwa maelezo mafupi hivyo...labda mpiga ramli ndio anaweza kujua tatizo na tiba! Elezea kwa kirefu ni lini ameanza kuona hali hiyo? Je ni kwa mwanaume mmoja tu inakuwa hivyo, her past boyfriends ilikuwaje? kuna seasonality ya hayo maumivu...yanatokea after every sex au kuna baadhi ya siku za mzunguko?

Kama hayo maumivu yapo tu wakati na baada ya kila tendo la ndoa hata akiandaliwa vizuri, na katika wakati wote wa mzunguko...inaweza ikawa hali tunaita 'retroverted uterus' ambapo kizazi (uterus) ambacho kwa kawaida huelekea kwa mbele (anterverted) kinakuwa kinaelekea kwa nyume (retroverted)..kwa hiyo inakuwa rahisi sana wakati wa tendo la ndoa uume kukifikia na kukisukuma wakati wa nje ndani, hata kama uume ni mfupi. Hali hiyo husababisha maumivu kwa mwanamke huyo wakati na baada ya tendo. Ukifanya Ultrasound inaonesha kama hilo ni tatizo.

Hali hiyo ni inakuwa mwanamke amezaliwa hivyo kimaumbile, kwa hiyo anakuwa na maumivu tangu anapoanza kujihusisha na tendo la ngono.

Matibamu mara nyingi kama maumivu si makali sana ni kutumia pain killers, lakini matibabu thabiti kama maumivu ni makali na hayavumiliki ni operation kukiinamisha kizazi kwa mbele na hivyo maumivu hayatokei tena.
 
maumivu yameanza juzi.anasikia maumivu makali.ni kwa mala ya kwanza.anaumia hata wakati wa kutembea.akilala haliumi labda alalie tumbo.jana alimeza diocipro jana akapata nafuu kidogo.
 
Back
Top Bottom