Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 395
George Clason mwandishi wa kitabu cha The Richest Man in Babylon, anasema kwamba watu wengi hawawezi endelea kamwe maana hawajui kabisa umuhimu wa akiba lakini pia huwa wanajifanya wana matumizi makubwa hasa ya vitu ambavyo wao huona ni mahitaji ya lazima.
Lakini ukweli ni kwamba sisi wenyewe huwa tunashindwa kutofautisha kati ya matumizi ya lazima na matamanio.
Clason anaendelea kusema kwamba, matamanio ya mtu huongezeka kadri ambavyo kipato chake huongezeka. Yaani kama huwezi kujizuia nafsi yako dhidi ya vitu ambavyo ni vya matamanio basi fedha zako zitazidi kupukutika bila kujua sababu kuu.
Robert Kiyosaki ndani ya kitabu chake cha 'Rich Dady, poor Dady' aliwahi kusema ujinga wa watu ni kwamba mahitaji yao huongezeka kadri ambavyo fedha anazopata zikiongezeka. Yaani ikiwa mtu ana uwezo wa kula elfu 2 Kwa siku chakula tu na akashiba basi ukianza kumpa elfu 3 badala atumie ile ile elfu 2 na kusave buku basi ataanza kutumia elfu 3 yote yaani ataongeza mahitaji mengine huenda hata akaongeza soda ambayo hapo awali alikuwa hanunui. Jifunze kudhibiti matumizi yako, kamwe usinunue mahitaji mengine ya ziada kisa tu fedha ipo TUNZA.
Kila mtu ana matamanio mengi ambayo hawezi kuyatimiza lakini shauku ya hayo matamanio huwa kubwa kadri ambavyo kiwango cha kipato chake huongezeka.
Sijui kama naeleweka . Ila George Clason anagongelea msumari na kusema kwamba Ili uweze kumudu fedha zako, basi ni lazima ujiwekee kikomo. Kikomo cha vitu unavyoweza kununua, kikomo cha unachoweza kula, kikomo cha safari unazoweza kusafiri, kikomo cha maisha unayoishi na ujitahidi usivuke hapo.
Endapo usipoweka kikomo basi utajikuta unaishi maisha nje ya kiwango cha fedha zako, na hapo neno mafanikio basi lisahau.
Ahsante kwa kunisikiliza, na samahani ikiwa nilikusumbua na hujaelewa chochote. Hayakuwa maneno yangu, yalikuwa ni maneno ya George Clason ndani ya kitabu chake cha The Richest Man in Babylon
Tamati, ikiwa hutajifunza njia ya kupata mafanikio ukiwa angali kijana basi utatumia muda wa uzee wako wote kujuta na kulia ukiwa kwenye wimbi la umaskini. The Richest Man in Babylon, (page 28)
Naitwa Amani Dimile, follow me if you can
Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app