Huu upuuzi unachangamkiwa na nani?

Lukwangule

Senior Member
May 25, 2009
157
2
Mimi sina kawaida ya kutukana watu , lakini huwa najiuliza nini maana ya kuwa na wataalamu, viongozi na wanasiasa kama kila kitu kinakwama kinahitaji msimamo wa kiongozi mkuu?
Kuna kitu kinanikera sana kuhusu suala la kuimarisha upatikanaji wa umeme katika mkoa wa dar es salaam.

Wajep wametupatia fedha mabilioni kuimarisha mfumo na ipo kampuni yao inatengeneza njia kwa ajili ya kupeleka umeme katika kituo kidogo pale usalama wa taifa (mkabala) kutoka Ubungo.
Umeme ule unatakiwa kupelekwa Temeke kuimarisha upatikanaji wa umeme na maeneo mengine ya jiji hili. Lakini hawa jamaa waliopewa zabuni ya kusuka nguzo za umeme kupeleka pale huenda wakarejea na fedha zao Japan kama huu ninaouita upuuzi hautaangaliwa na kuondolewa mapema.

Kwanza fedha zenyewe si zetu na kampuni si yetu na sisi ndio wenye shida anatokea mtu mmoja anazuia umeme usipite eneo la tanroad eti kwa dai kuwa watu wake wanaosali wataharibikiwa.
Ule umeme lazima tuupitishe pale, yeye kanisa anaweza kuhamisha, kama alikuwa anajua kwamba yupo katika eneo karibu kabisa na reserve ya Tanroad basi ajue na athari zake. maeneo hayo ndiyo yanayopitisha mabomba na vitu vingine vya jamii, kwanini kaleta karibu namna ile kanisa lake?Pili mbona hizo nguzo zinainamia kwingine wala hazina uhusiano na yeye. mawasiliano gani duniani hapa anadhani yataharibiwa kwa kuwa karibu na nguzo zile?

Kuna nguzo zinasafiri kutoka kidatu zinabeba msongo mkubwa kabisa, wote tunajua umbali wake, wale wapogoro wakatae nini? Tuache hayo!

Mimi najiuliza Ngeleja anafanya nini hasa kuhusiana na suala hili au anaogopa serikali ya CCM haitapata kura kwa kumshauri anayehusika atuache tupitishe nguzo zetu kwani muda unakwenda na Wajapan hawatuelewi? Lakini kwa mitaji hii ya umeme wa kubabaisha si lazima tuwaondoe madarakani tu?

Nina hasira sana kwani kule temeke kunakatikakatika hovyo umeme na huyu kakobe anadai kwamba lile eneo likipitishwa umeme wananchi wake watafadhaika halafu watashindwa kutekeleza majukumu yao ya kijamii. kama kweli apewe neno limuingie.Sawa apewe kiwanja kingine akajenge kama inaonekana anaonewa. Asisahau kuwa umeme ule unataka kusaidia eneo maskini kabisa ambalo zamani aliishi nyakati hizo ambazo sina sababu zozote zile za kuzitaja. Mimi nataka atuachie nafasi tupitishe umeme.

Si suala la kututisha na Mungu. Mungu ni wetu na alituambia tuyatumie vyema majambo haya ya dunia ili kufika kwake. Umeme wa kubahatisha ndio unaomaliza miti kwa kutengeneza mikaa na ndio unaangamiza dunia kwa kuondoa kinasa kaboni.(miti).

Mimi nasema kwa kukasirika sana kwani haya mavitu tunayalealea tu. Huyo aliyechora amekuwa chizi? hana akili? mwendawazimu?Kichaa au punguani? Kama ni mtaalamu huyu mwingine ambaye naye hakusomea utaalamu anasema nini hasa? Anasema anao wataalamu. sawasawa kila dhehebu lina wataalamu. Wale wa kanisa la wakatoliki Msimbazi nao wanahaki ya kupiga kelele basi. Wana kitu kinachoongoza ndege magneti ile au sio . Huyu anayesema vipaza sauti vyake vitazidi anataka kutueleza nini? pale katika kona ya Tazara kuna substation basi Radio Tanzania wangelisema iondolewe inavuruga utaratibu.

Tusidanganyane bwana.

Si sumaku wala si umeme. mainjinia wanaofua umeme huo basi wangelikosa urijali .

Narudia tena Sijui kwanini viongozi inapofika wakati wa uchaguzi huwa hawafanyikazi zao sawasawa, nini woga wa kunyimwa kura? Mimi nadhani hili wala si jambo.Watu wanasema tu kama serikali haipo. Kama uongozi haupo? Nini maana yake hata shauri la kanisa linahitaji miniti za kabineti? ili iweje huu mradi wa kuboresha umeme dar urejee kwa wajep wenyewe nini? sisi kama si wehu tuna kasoro ya kuzaliwa kama vyote havipo tuna shida kubwa kwelikweli.
 
Mzee wa Lukwangule, waziri kijana Ngeleja, ameonyesha udhaifu mkubwa kwenye hili, Tanesco nao wamemuachia wakidhani anaweza, Askofu Mkuu kavimba bichwa anamtaka Mkuu wa Kaya.

Hoja yake ya interfiarance haina mashiko, TCRA hawawezi kumpa kibali cha kuleta mitambo ya analogue ambayo ni obsolate tech wakati tunashift digital kuanzia mwezi 7 mwaka huu.

Eneo linalopita nyanya ni road reserve, sio lake, sasa anachoogopewa hapa ni nini?.

My opinion, jamaa ni kweli ana powers, sasa anataka kupractice ili kuvutia waumini.
Kila nikipita pale na kushuhudia umati wa watu ambao 'he plays their minds away' kwa kisingizio cha kumtumikia Bwana, huwa namkumbuka David Koresh na wale Camp Davidians, na Kibwetere!.

Bwana Asifiwe Sana!.
 
Swala la huo umeme kudhuru waumini ni la kisaikolojia tu. Kuna nyumba nyingi nje ya nchi ambako umeme wa msongo mkubwa hupita juu ya nyumba bila madhara. Kama TANESCO na ukorofi wa waumini hao kuna njia mbadala za kiufundi nzo ni kutumia nyaya ambazo zina emw kidogo kuliko hizo za aluminum wazotumia. Ni ghali lakini zitamaliza huo mgogoro.
Kiubwa kujenga karibu na road reserve chochote chaweza kufanywa katika eneo hilo. Je songas wakitaka nao kupitisha gas hapo Kakobe itapasa alale mwenyewe kuzuia magreda!!!!
 
He inakuwaje vile, mkijadili watu wanakufa basi kwa kuwa mlishamalizana nalo mnaliacha wakati hakuna ufumbuzi bado.ihii! Mhh! Hakuna jipya katika juhudi za kutengeneza maarifa?Labda watu hufikiri kwamba mjadala hufungwa au labda JF anadhani hivyo lakini suala linalozungumzwa hapa ni la manufaa ya umma na watendaji wa umma wamepata kichapo walipoenda kutekeleza kazi zao tena za halali kuliko anavyofikiria umimi wake huyo bwana kanisa.
 
Kwa hiyo kama tushajadili ndo wengine wasijadili tena. Au mjadala kwako ni kama porojo za kwenye kijiwe cha kahawa. Unapiga porojo tu basi.
Huku ndo kudandia gari kwa mbele. Nimesema suala hili tumelijadili nikimaanisha kuna thread nyingi tayari zipo, kama mdau angetaka kuchangia angeenda kutafuta mada husika aweke bandiko lake..amekulia kusiko na ustaarabu?
 
Hii nchi bwana hivi kila mtu afanye anavyotaka kweli tutafika?always mimi huwa ndio maana namkumbuka Nyerere hivi kweli ingekuwa enzi za Nyerere Kakobe angekuwa na hiyo jeuri ya kuivimbia kichwa serikali?hapo ndipo naona udhaifu wa serikali ya Kikwete ,inambembeleza mtu mmoja wakati mamilioni wanapata shida ya umeme,pia nawashangaa waumini wa hilo kanisa mtu na akili yake anaacha familia yake anaamrishwa kuja kupigwa na baridi na kuwakiwa na jua siku nzima kwa ajili tu askofu wa kujipachika kaamuru hivyo,naamini sasa akina vibwetere tunao hapa hapa,pia inabidi serikali ionyeshe kama inajali walio wengi hivi ningekuwa mimi Mfianchi serikali ingenigwaya?au kuna walio so special,pelekeni FFU bana tuone kama tutaona njano pale Mlimani,ile ni aibu hata kwa watu wanaotoka nje kwa kutuona watu tusiofanya kazi kwani siku nzima watu wamekaa tu,sijui hapo kile kifungu cha kosa la uzururaji kinatumika vipi.Nimeudhika kweli sijui tumlete Kagame ndio ainyoshe hii nchi
 
Ama kweli kazi tunayo .Sasa huyo ni mchungaji sasa je wakulima watafanya nini? Pole sana JK na serikari yako . Hili swala halijaanza leo lina siku kwenye vyombo vya habari. Huyo Ngereja anataka kuwambia nini watanzania kuhusu hilo?
 
Mzee wa Lukwangule, waziri kijana Ngeleja, ameonyesha udhaifu mkubwa kwenye hili, Tanesco nao wamemuachia wakidhani anaweza, Askofu Mkuu kavimba bichwa anamtaka Mkuu wa Kaya.

Hoja yake ya interfiarance haina mashiko, TCRA hawawezi kumpa kibali cha kuleta mitambo ya analogue ambayo ni obsolate tech wakati tunashift digital kuanzia mwezi 7 mwaka huu.

Eneo linalopita nyanya ni road reserve, sio lake, sasa anachoogopewa hapa ni nini?.

My opinion, jamaa ni kweli ana powers, sasa anataka kupractice ili kuvutia waumini.
Kila nikipita pale na kushuhudia umati wa watu ambao 'he plays their minds away' kwa kisingizio cha kumtumikia Bwana, huwa namkumbuka David Koresh na wale Camp Davidians, na Kibwetere!.

Bwana Asifiwe Sana!.
Kaka wakati mwingine unafikiri kama kweli viongozi hawa wanajua wanachotakiwa kukifanya kwa taifa hili au ule ujana ni ukosefu wa utaratibu na kukumbatia zaidi mhhhhhh! manake ukisema sana lazima utukane kwani hasira huwa zinapanda kama mashine ya jet inavyosuck hewa ili injini iendelee kufanya kazi ahh
 
Back
Top Bottom