Huu uozo unamaanisha nini kwetu? Jerry Silaa na wenzako mnaishi wapi?

MAMC

Senior Member
Jan 3, 2012
139
66
Wanajamvi, naamini kati yetu tunaishi au tumetumia barabara za hapa Dar hivi karibuni.
Vitu vikubwa ambavyo hutoacha kuviona ni!

1. Ujenzi/ukarabati unaondelea maeneo kadhaa barabara kuu na za mitaani (nasikia nyingi ya hizo zimechukuliwa na JP Magufuri na sio manispaa!)

2. Uchafu na uharibifu mkubwa unaofanywa na waosha magari yakiwa katika maegesho.

Mfano. Milambo st- kama unaingia bank kuu, chagga st - maeneo ya Chef Pride! etc na ikumbukwe magari ni yetu, na kwa kuwa yanatumia barabara basi huu uharibifu utatusumbua sie kabla ya hata hao waosha magari.
Na kama kila mahala pameloa as if mvua umenyesha basi tunatembeaje kufika ofisini, etc?

3. Michanga iliyo kidhiri mfano, University Rd, Shekilango, kaijenge, coka cola, mwinyijuma, etc

Hakuna asiejua kama mchanga niko adui namba 1, wa barabara, pia vumbi inachafua magari, inaingia nyumba za Jirani na barabara, husababisha ajali mana breki hazifungi vizuri, barabara unakuwa nyembamba, etc

4. Uchafu toka majumbani kutupwa katikati ya gema za barabara, au pembezoni mfano.Africa sana - karibu na mwenge sokoni - hivi sasa pananuka! msasani - mandazi rd.Samu Nujoma karibu na mwenge kituoni, etc

Haya mambo ni rahisi sana kuyakomesha tukaishi vizuri kama watu wa karne ya 21 na mifano ipo.isipokuwa.

Tujiulize hawa viongozi woote.kuanzia m/kiti wa mtaa, diwani, meya, wako wapi?hii si kazi yao? Hakuna By laws?

Na je wao huwa watumia barabara gani? Hawayaoni haya?

Na sie wanajamvi - japo hatuko madarakani tumetimiza au tuna mpangi kani ku- play part yetu?

Rai yangu! Mwaka 2014 wana mabadiliko wote tugombee kuwa wenyeviti wa mitaa.Mambo mengi yanayotuhusu moja kwa moja yanatakiwa kuwa initiated na hawa watu, ambao hata hatujawahi waona!!! Ubunge baadae!

Naomba kuwakilisha!
 
Nakuunga mkono kwa kuona tatizo na kutoa suluhisho ifikapo 2014, tujitokeze kusafisha yaliyowashinda viongozi wa sasa ambao wako kimaslahi zaidi kuliko kuwasadia wanachi. Pili hivi hao wanaotupa uchafu wakikuta mwingine ametupa au huo uchafua wao na wenyewe wanaona kinyaa? au wanafurahia hizo harufu.
 
Back
Top Bottom