huu ni ubepari wa aina gani na utaisha lini????

Carla

JF-Expert Member
Aug 4, 2012
398
331
wana jf wenzangu hebu tujuzane labda mimi nina kaujinga kanastaili kuondolewa ntauliza kutumia mfano il mnielewe'mf,mimi nafanya kazi kwenye kampuni nikapewa target kwamba kwa mwezi niingizie kampun milion 3 afu wenyewe watanilipa laki 4 nikafaulu kufanya hivyo wakanipa mshahara wangu alafu wakaniongezea target had mil10 nikafikisha lakini wakanipa ile ile laki 4 je huu sio unyonyaji? hiki kitu ni haki na kama sio nikashtaki wapi??naombeni mawazo na msaada wenu
 
hiyo ni kampun gani,ukiona wanakufanyia hivo we iingizie hiyo kampun ela hiyo hiyo million 3,kampun nyingine zina tamaa na siyo waaminifu
 
Inategemea na agreement yenu. lakini na wewe una wajibu wa kuwauliza, unaweza kukuta wanakutaim kama utauliza au. Ndio tabia za mabepari hizo, kukunyonya mpk utoe povu.
 
soma upya mkataba wako wa ajira kabla ya kushitaki, halafu kaa na mwajiri wako mpange terms upya utakua safe
 
ni kampuni ya tigo na ndo wanavyowafanyia sales man wa tigo rusha yani wananikwaza: atleast wangekua wanatoa hata ten percent ya kiasi unacho waingizia jamani!
 
Yaani wewe unaonesha unaweza kujiajiri na kuanzisha kitu ya kwako...

Hapo sepa haraka sana...You can be an investor soon
 
Jamani kwani mfanyakazi ni ww pekee hujui wapo wengine kuna kulipia kodi ya ofisi,matengenezo,vat,kulipia umeme etc usilalame wakati unajua kuwa hayo yapo

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
nisipo sema nani atasema tz kuna freedom of speech lakini watu niwaoga coz kuna vitisho vya chinichini,na uzuri jf tunaruhusiwa kujimwaga na tunapendana ndo mana ukitoa hoja lazma utapata msaada wa namna moja au nyingine na hata ikiwa ni tatizo la mahusiano jf wana jibu la tatizo 'kidole kimoja hakivunji chawa' asanten wadau mlio nielewa na kunipa mawazo yenu naendelea kukusanya kama kuna mengine
 
Yeah ni unyonyaji huo. Atleast ni kamfano

nilitumia mfano ili nieleweke lakin ni ukweli mtupu na mbaya zaidi mimi wa mil kumi nalipwa laki nne na yupo wa mil ishrin analipwa hiyohiyo laki nne na wapo wa mil tano, sita wanalipwa hiyo hiyo laki nne, wakuu kama mpo badilikeni kwa upande wangu naweza nikatoka mda wowote: je hao wengine tuwe waungwana,
 
wewe usisikitike
iba ujuzi hapo,isome vyeema kampuni,
jifunze kazi zoote
itakuja kukulipa mno baadae....jifanye mjinga now
 
nilitumia mfano ili nieleweke lakin ni ukweli mtupu na mbaya zaidi mimi wa mil kumi nalipwa laki nne na yupo wa mil ishrin analipwa hiyohiyo laki nne na wapo wa mil tano, sita wanalipwa hiyo hiyo laki nne, wakuu kama mpo badilikeni kwa upande wangu naweza nikatoka mda wowote: je hao wengine tuwe waungwana,

dah? Pole sana Mjumbe, naamin ushaur wa The Bos ndo mpango mzma... Ila pole sana Jo
 
Back
Top Bottom