Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,789
- 218,428
Nitasema Kweli Daima Fitina kwangu Mwiko .
Mkutano ulioandaliwa na TCD , ambayo inadaiwa kuwa Kituo cha kusimamia Demokrasia nchini Tanzania , ambao umepanga kujadili masuala ya Demokrasia , ikiwemo Katiba Mpya , Tume Huru ya Uchaguzi na Sheria za Uchaguzi , leo umeingia siku ya pili , Mkutano huu umefadhiliwa na Ubalozi wa Marekani .
Sina tatizo na mkutano huu muhimu , Tatizo langu kwenye mkutano huu ni Uwepo wa Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi na kupewa heshima ya kuwa Mgeni Rasmi .
Hussein Mwinyi aliingia madarakani 2020 kwenye uchaguzi ambao ulivunja rekodi ya mauaji ya chaguzi zote zilizowahi kufanyika Zanzibar , wapinzani walidhibitiwa vilivyo , huko Pemba walipigwa mabomu hadi vikongwe , ulikuwa uchaguzi wa hovyo kuliko wowote niliowahi kuushudia tangu nipate akili , Zipo tetesi kwamba kulikuwa na majeshi kutoka Burundi ama Rwanda yaliyokodiwa na Serikali ili kudhibiti Wapinzani kikatili zaidi .
Hussein Mwinyi hakuwahi kuomba radhi kwa unyama ule , Kiongozi wa namna hii hakupaswa kuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa Kidemokrasia kama huu wenye lengo la kuboresha Mazingira ya Uchaguzi na demokrasia .
Ni vema waandaji wa Mikutano kama hii wakajaribu kutuheshimu (hata kwa heshima ya uongo) sisi Wananchi tulioona hali ile na ambao bado hatujasahau , waheshimiwe wafiwa na Yatima waliopoteza ndugu zao kutokana na uchaguzi ule