Hussein Bashe afanya ziara ya ghafla katika hospitali ya wilaya ya Nzega

Fandre

JF-Expert Member
Sep 20, 2013
320
225
attachment.php



attachment.php


attachment.php


MBUNGE WA NZEGA MJINI MHE. HUSSEIN BASHE AMEFANYA ZIARA YA GHAFLA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA NZEGA LEO TAREHE 12.12.2015 NA KUBAINI MAPUNGUFU MAKUBWA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA.


Mbunge wa jimbo la Nzega mjini Mhe. Hussein Mohamed Bashe majira ya saa tano na nusu asubuhi leo Jumamosi tarehe 12.12.2015 amefanya ziara ya ghafla katika hospitali ya Nzega mjini na kubaini mapungufu makubwa katika utoaji wa huduma za afya kama ifuatavyo.


1) Upungufu mkubwa wa vifaa tiba hasa vifaa vya kujifungulia kwa wakina mama wajawazito.

2) Ikiwa ni pamoja na uhaba wa vitanda vya wogonjwa hasa wodi ya wototo ambayo haina vitanda mahususi kwa ajili ya watoto. Uhaba wa matandiko kwenye vitanda, uhaba wa neti za mbu na ukosefu wa taa kubwa kwa ajili ya kumulika ndani ya wodi ya watoto, wanawake na wajawazito ili kufanikisha kazi ya kutafuta mishipa ya damu nyakati za usiku.

3) Upungufu wa vifaa vya kujifungulia yaani delivery pack, pia amebaini uchakavu wa vifaa ndani ya chumba cha kuzalisha wajawazito ikiwa ni pamoja na uwepo wa mikasi yenye kutu.

4) Uhaba wa mashine ya oxygen katika wodi ya wazazi na chumba cha kuzalishia wajawazito

5) Uhaba wa damu salama kwa ajili ya matumizi ya kitabibu.

6) Ubovu wa mashine ya kuulia vijidudu kama bakteria kwenye vyombo vyenye asili ya chuma yaani sterilizer inayotumika katika chumba cha kuzalishia wajawazito

7) Malimbikizo makubwa ya madeni ya posho za watumishi wa hospitali kama vile on call allowance, on duty allowance, post-mortem allowance na posho za kujikimu kwa watumishi wapya walioajiriwa hivi karibuni.

8) Karibuni asilimia 85 ya watumishi wote katika hospitali ya wilaya ya Nzega hawajapandishwa vyeo kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi.

9) Hospitali inakabiliwa na uhaba mkubwa wa watumishi yaani madaktari na manesi.

10) Tozo za ushuru wa maegesho ya baiskeli zinatozwa kwa wananchi wanaoenda hospitalini hapo.

11) Uhaba wa majengo kama vile wodi ya wanawake ambayo inapokea wagonjwa wengi kuzidi uwezo wake.

12) Uwezo mdogo wa hospitali kuhudumia jenereta hasa nyakati ambazo umeme unakatika mara kwa mara.

13) Kutokutumika kwa jengo jipya la upasuaji (theatre) ambalo ujenzi wake umekamilika.

14) Kutokufika kwa wakati kwa vifaa na madawa ya kufanikisha zoezi la upasuaji katika chumba cha upasuaji.

15) Madaktari kutopita round kuangalia hali za wagonjwa kwa mfano wakati wa ziara katika wodi ya wazazi mbunge alikuta Daktari hajapita round siku nzima, jambo ambalo linachangiwa na uhaba wa madaktari lakini pia uwajibikaji hafifu wa watumishi.

16) Uzembe wa baadhi ya manesi kutowahudumia wagonjwa ipasavyo na kwa wakati, mfano Mbunge alikuta mgonjwa aliyemaliza dripu tangu siku iliyopita saa mbili usiku na sindano ya dripu hiyo haikuondolewa mkononi mwake na dripu ikining?inia mkononi mpaka baada ya ndugu za mgonjwa huyo kulalamika mbele ya Mbunge, hivyo nesi akalazimika kuichomoa.

17) Malalamiko ya uwepo wa rushwa ili kuharakisha huduma za afya kwa wagonjwa hasa katika huduma za uzazi.

18) Afisa Afya wa Wilaya ambaye yupo likizo ya masomo, amelalamikiwa na madaktari mara kwa mara kutoka likizo na kuja kugawa fedha za OC kisha anarudi masomoni.

HATUA ALIZOZICHUKUA MBUNGE.

1) Mbunge amepiga marufuku hospitali ya Wilaya ya Nzega kutoza ushuru wa shilingi mia mbili kwa wananchi wanaoegesha baiskeli zao pindi wanapoingia ndani ya hospitali hiyo.

2) Mbunge amedhamiria kushughulikia suala la utumishi wa Hospitali ya Nzega kwa kuhakikisha DMO (District Medical Officer-Afisa Afya wa Wilaya) Daktari Mkuu wa wilaya ya Nzega anahamishwa kituo cha kazi kutokana kushindwa kushughulikia kero za watumishi wa hospitali ya Nzega na kutosimamia ipasavyo utolewaji wa huduma za afya hospitalini hapo.

3) Mbunge amemtaka DED asiruhusu DMO arudi kazini ili tufanye uchunguzi wa OC na atafutiwe kazi sehemu nyingine na sio Nzega kwa sababu hawezi kazi.

4) Mbunge atahakikisha madai yote ya madeni ya posho za watumishi wa hospitali ya Nzega mjini yanalipwa na Halmashauri ya mji wa Nzega haraka sana na kuahidi kuwasilisha madai hayo mbele ya kikao cha Halmashauri ya mji wa Nzega inayowajibika kulipa stahiki za watumishi hao.

5) Mbuge atahakikisha ufumbuzi wa haraka unapatikana katika masuala yote ya upungufu wa vifaa tiba ikiwamo vifaa vya maabara, oxygen, vitanda kwenye wodi za watoto , wazazi na wanawake.

6) Mbunge ameadhamiria kuhakikisha wananchi wengi zaidi wa Jimbo la Nzega mjini wanajiunga na mfuko wa afya ya jamii yaani [Community Health Fund] au maarufu kama CHF.

7) Mbunge anakusudia kushughulikia suala la upatikanaji wa damu salama katika hospitali ya wilaya ya Nzega.

8) Mbunge ameahidi kushughulikia upatikanaji wa dawa nyakati zote katika hospitali ya wilaya ya Nzega kwa kuhakikisha kuwa duka la bohari ya dawa yaani MSD linafunguliwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega haraka iwezekanavyo.

9) Aidha Mbunge ameagiza apatiwe taarifa kamili ya kiasi cha malimbikizo ya madeni yanayodaiwa na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Nzega, ali kila mtumishi anayedai apewe stahiki zake haraka iwezekanavyo.

10) Mbunge amewaelekeza wananchi kutoa taarifa za uwepo wa rushwa haraka sana kupita dirisha maalumu la malalamiko lililopo hospitalini hapo. Pia ameagiza uongozi wa hospitali kutoa elimu ya kutosha ya jinsi ya kuwasaidia wananchi kutoa malalamiko.

11) Mbunge ameahidi kuisimamia Halmashauri ya mji wa Nzega ili iweze kumudu kuchangia gharama za kuendesha jenerata ya hosptali ili ikitokea umeme umezimika hospitalini huduma muhimu ziendelee.



Imetolewa na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mbunge wa Nzega Mjini
 

Attachments

  • IMG-20151212-WA0046.jpg
    IMG-20151212-WA0046.jpg
    76.2 KB · Views: 5,890
  • IMG-20151212-WA0050.jpg
    IMG-20151212-WA0050.jpg
    107.2 KB · Views: 5,736
  • IMG-20151212-WA0048.jpg
    IMG-20151212-WA0048.jpg
    80 KB · Views: 5,668
Hongera sana Bashe. Achana na wanafiki, watumikie wana Nzega. Mara ya mwisho kupita Nzega ilikuwa miaka ya 2002. Sijuia sasa papoje ila weweni kiongozi. Mshirikiane na Kigwangalla ili kuhakikisha wananzega wananemeeka
 
Hii ni kazi yake... kuan siku tutaambiwa mtu kafanya ziara ya ghafla chooni kwake

too much drama sasa


Ndugu zangu tusiyaangalie mambo kwa macho ya kawaida tu, ni jambo la kweli kabisa kuwa nchi yetu imekuwa na mapungufu mengi katika maeneo mbalimbali lakini Mtu mmoja pekee hataweza kutembea nchi nzima na kuhimiza maendeleo hasa kwa maeneo yaliyoko mbali kwani watu wengi walioko huko wanahisi hawawezi kufikiwa na mamlaka za serikali hivyo kujifanyia mambo kwa namna waitakayo.

Nadhani tuzipongeze juhudi za watu na viongozi wenye kuonyesha kuwa nao wanaunga mkono jitihada zinazofanywa katikakuhakikisha tunatokomeza uzembe unaorudisha nyuma maendeleo ya taifa hili kuanzia ngazi za chini kabisa.

Mh. Hussein Bashe ni mbunge mpya katika bunge hili la sasa na Jimbo la Nzega Mjini, hivyo kwa alichofanya ni jambo la kutiwa moyo ili aendelee kuhimiza maendeleo jimboni mwake. Sisi tukaao mbali au nje ya Jimbo la Nzega na Nzega kwa ujumla tunaweza tukabeza jitihada hizi ila wananzega watafurahia sana kwani wanajua mahitaji yao.

#UzalendoKwanza
#HongeraMhBashe
 
you are light???? ulitaka kumaanisha nini mkuu...yaani jamaa ni mwanga ama wewe ni kayumba product
 
Hivi hizi hospitali za wilaya huwa Kuna MDs kweli au COs na AMOs tu?
 
CCM ikiwa na mtazamo huu wa kimaendeleo itabidi upinzani ujipange na mawazo mazito zaidi.
 
Hivi bashe alikuwa hayajui hayo? Huu sasa unaitwa uigizaji ushaanza kunikera, kushtukiza ndio imekuwa kufanya kazi?
 
you are light???? ulitaka kumaanisha nini mkuu...yaani jamaa ni mwanga ama wewe ni kayumba product
Halafu kaandika your light siyo you're light kama ulivyoandika wewe. Ndo elimu ya nchi hii ilipofikia halafu serikali ndo kwanza inataka kupenyeza siasa hadi private schools.Huyu lazima ni zao la shule za kata na si ajabu ni mhitimu wa Chuo kikuu.
 
Kila siku ziara za gafla!
Hivi ina maana hao viongozi walikuwa hawajui shida wazipatao wagonjwa hospitalini au kujua majungu fu ktk hospital

Ovaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom