Huruma: TANESCO inaidai Zanzibar Bil. 121 wakati Mapato yao ni Bil 425. Tutawaua kwa presha

Halaf Lissu akiwapa akili ya kudai uhuru wao eti wanampa kesi za uchochezi!
 
Hilo deni limelimbikizwa si mwaka mmoja
Pia hilo ni pamoja na watu binafsi.walipe tu hakuna jinsi shirika litakufa hata kwa kukopa watakosa
 
Wawakatie tuu umeme coz Zanzibar ni moja ya nchi jirani inayotuzunguka na hatuna maslahi nayo ya kiuchumi zaidi ya kisiasa
 
Ni aibu kwa mwanaume kulilia amkane jirani yake au nduguye ili akalelewe na misaada ya wanaume wenzie. Sio sifa kutegemea misaada iwe ya makafiri au ya OIC. Kwanza Mungu anataka tufanye kazi tujitegemee.
Kama na hao wanaotowa misaada ya OIC wangekuwa wavivu na rushwa imewatala eanategemea kuishi kwa misaada nani angemsaidia mwenzie. Je dunia ingekuwa ya watu wa aina gani?
Mahiga anajibu hoja za kutegemea misaada, pia analalamika kwa kutopewa misaada.


Je hili la umeme limekuja, kuzima "Ubashite" au "Fanta Zero"?

 
Lakini hili tatizo ni kubwa zaidi kuliko linavyosemwa. Ukisikiliza upande wa pili(ZECO) ndio utajua vizuri masuala hasa yanayozunguka kadhia hii. Sio suala jepesi la on/off!
Na Melisa J
Taarifa kutoka Z’bar zinaeleza kuwa kuchelewa kulipwa kwa deni la umeme hadi kufilia Bilioni 121 kunatokana na Shirika la Umeme la huko (ZECO) kutokubaliaa na gharama za umeme wanazotozwa na TANESCO.

Imeelezwa kwamba sio kweli kwamba ZECO hawataki kulipa deni, isipokua hawataki kulipa kwa viwango vilivyowekwa na TANESCO. Kwa mujibu wa viwango vya gharama za umeme vya TANESCO, ZECO wananunua umeme kwa gharama zilezile ambazo TANESCO wanauza kwa wateja wengine wa bara.

Hoja ya ZECO ni kwamba haiwezekani TANESCO wawauzie umeme kwa viwango wanavyouziwa wateja wengine kwa sababu TANESCO haihusiki na gharama za kuweka miundombinu ya umeme Zbar wala matengenezo yake.

Afisa mmoja wa ZECO niliyezungumza nae kwa simu na hakutaka jina lake liwekwe wazi amesema “Tanesco kutucharge gharama sawa na wateja wengine ni unyonyaji. Kama miundombinu yote tunaweka wenyewe (nguzo, transforma, nyaya, etc), bado mishahara ya wafanyakazi tunalipa wenyewe na gharama za uendeshaji, pia tunafanya maintanance wenyewe, kwanini Tanesco watuuzie umeme sawa na wanavyowauzia wateja wengine?”

Mvutano huo kuhusu bei za umeme ambazo ZECO wanapaswa kulipa TANESCO ndio umesababisha deni hilo kufikia Bilioni 121 kwa sasa.

Juzi akiwa mkoani Mtwara Rais Magufuli aliagiza TANESCO kuwakatia umeme Zanzibar kutokana na kushindwa kulipa deni hilo. Akizungumza alipokwenda kuweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha Tanesco mkoani Mtwara, Rais Magufuli alikaririwa akisema;

“Msiogope mnapaswa kukata huduma hii kwa taasisi yoyote ambayo hailipi bili zake. Nataka kumwambia waziri Muhongo kwamba umeme unapaswa kukatwa hata Ikulu. Nikilala gizani, maafisa wa Ikulu ambao hawajalipa watawajibika na sio wewe. Una hakikisho langu kwa hili. Ninaambiwa SMZ haijalipa Sh121 billion. Ninyi (Tanesco) sio wanasiasa. Mnapaswa kuzingatia majukumu yenu ya kitaaluma… kata huduma ya umeme. Nimesema kata..”
Kama ni kweli ZECO Wana hoja ya Msingi. Lakini kwanini hawakupinga hili EWURA wakati wa kupitisha tarrifs?
Dongate alilamikia kuuziwa Gesi kwa bei sawa na ya Dar. Kwenye Link iliyopo hapa inayosomeka Si deni, ni Tanesco kuikomoa ZECO Link Huruma: TANESCO inaidai Zanzibar Bil. 121 wakati Mapato yao ni Bil 425. Tutawaua kwa presha

ZECO (shirika la umeme Zanzibar) linalalamikia kitu kinachofanana na malalamiko ya Dongate. Magu amefikia uamuzi wa kumpa Dongate mgodi wa makaa ya mawe na pia kuagiza apewe bei ya gesi (gas tarrifs) za Dar, Mtwara.
Link Hongera Rais Magufuli kwa kumruhusu Dangote achimbe Makaa ya Mawe, bado Reli na Gesi...

Leo akiwa katika sherehe ya uzinduzi wa magari 580 ya Dangote, rais Magufuli amemruhusu Dangote kuchimba mwenyewe Makaa ya Mawe na kuyasafirisha kwa matumizi yake na akiweza kuchimba ya ziada auzie wengine. Kwa hatua hii, Rais Magufuli anastahili pongezi za dhati sana.
Sasa bado aruhusiwe kujenga reli yake, aruhusiwe kujenga bandari yake Mtwara, aruhusiwe kuchimba gesi yake.
Kuhusu gesi wengi humu tulimtetea Dangote kwa nini auziwe gesi kwa bei ya Dar es Salaam. Ameamrisha ndani ya siku saba apewe bei elekezi kwa mkoa wa Mtwara.

Paskali
Ukisoma kwa kutulia malalamiko ya ZECO wana hoja ya msingi ambayo inapaswa kushughulikiwa.

Muungano wa magumashi. Kuchakachua chaguzi. Ni kuwagawia umasikini wadanganyika.
 
Kweli hawawezi kukata umeme hawa,wacha wajaribu kukata nusu dakika tu waone kama tanganyika haitorudi fasta,hatutaki maneno kateni.
Hahahaha Nyumba ndogo ni lazima tumtunze..


Mlizoea kukaa kwenye mikeka na kula urojo bila kufanya kazi tukiwalipia umeme, Awamu hii ya magu mtajibeba hahahahaha


Hako ka mkoa kenu hakatupi pressure kwanza mnatutia hasara tu
 
Ndo safi wapate akili
Mimi naona tatizo liko ZECO,kama huduma ya umeme inalipwa na mtumiaji wa mwisho kwa Tanzania bara na kama ilivyo Tanzania visiwani ni kwanini serikali ya mapinduzi ya zanziba idaiwe?,hapa ina maana hao ZECO wanakusanya na wanatumia kwa matumizi mengine badala ya kurejesha mapato hayo TANESCO,Kama vipi ifanyike uthamini(valuation) ya ZECO na kama thamani yake itakuwa sawa na deni inayodaiwa na TANESCO iwe tu ni branchi ya TANESCO,ili basi TANESCO wakusanye moja kwa moja kwa watumiaji wote wa Jamhuri ya Muungano Tz,
 
Mahiga anajibu hoja za kutegemea misaada, pia analalamika kwa kutopewa misaada.


Je hili la umeme limekuja, kuzima "Ubashite" au "Fanta Zero"?


Sijui mada ya vyeti feki inahusiana vipi na mambo ya misaada kama nilivyo andika ktk post zangu hizo ulizoninukuu?
Kuhusu misaada lets think like Great thinkers, Narudia tena ni aibu mwanaume kujitenga na nduguyo kisa ukayegemee kuishi kwa misaada ya mwanaume mwenzio. Ni hivi iwe Tanganyika au Zanzibar au Tanzania yote au UK, USA, UAE ni aibu kuishi kwa kutegemea misaada. Mbaya zaidi kumtenga mwenzio kisa misaada hiyo tunarudia enzi za utumwa mababu anawakamata jirani au ndugu anaenda kuwapeleka kwa mwarabu ili apate misaada ya shanga, kanzu na viungo vya pilau, au anawapeleka kwa mzungu apate biatu suruali na bunduki.
 
↑↑↑ Lazima ufahamu Kuwa Suala la Zanzibar Kudaiwa Deni La Umeme Si Kosa la Wazanzibari.... Bali Ni Kosa la Hiyo Serikali Iliyowekwa Madarakani Kwa Nguvu Na Huyo Mdaiji Baada Ya Kufuta Uchaguzi Halali....

Wazanzibari Wanalipia Umeme Kila Mwezi Kwenye Shirika La Umeme la Zanzibar (ZECO).... Na uchelewe Kulipa Wiki Mbili tu unakatiwa Umeme!!! Sasa Hapa Tuiulize Serikali Je Pesa Wanazozikusanya Kwa Wazanzibari Wanaonunua Umeme Zinakwenda Wapi??? Kwanini Wadaiwe???
Ni Ukweli Usiofichika Kuwa Taasisi na Mawizara ya Serikali Pamoja Na Majengo/Matawi Ya CCM hayalipii Umeme Wanaotumia au Wanalipa Kwa Mfumo Wanaotaka Wenyewe Na Wala Hakuna Mtu Anaeweza Kuhoji Hili jambo ambalo linaongeza Mzigo Kwa Shirika la Umeme la Zanzibar...

Hapa Usiseme Wazanzibari Wamegeuka Kupe! Bali Vibaraka Wa Tanganyika Waliopo Madarakani Ndio Wamegeuka Kupe kwa Kukusanya Malipo Yetu Ya Umeme na Kutoyapeleka Kwa Anaetuuzia umeme..

Sisi Tutaendelea Kulalamika Kuwa Muungano Haututendei Haki, Na hili deni isiwe sababu YabKuhalalisha Unyonyaji, Bali Nindalili moja Ya Ubovu wa Muungano....
Mkuu kumbe ni wanymbani? Dah poa mtani
 
Back
Top Bottom