Humphrey Polepole azibwa mdomo na fikra

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,281
2,423
Kwa wafuatiliaji wa siasa za kiharakati nchini Tanzania hamtakuwa wageni kwa jina ili la Humphrey Polepole.Ni mmoja wa vijana waliopata umaarufu kupitia vyombo vya habari asa wakati wa mchakato wa katiba mpya na uchaguzi.

Wakati wa mchakato huo Polepole alionyesha msimamo wake kuhusu Demokrasia, Umuhimu wa katiba mpya na kupinga kuwepo nafasi za uteuzi kama wakuu wa mikoa na wilaya mpaka akadiriki kusema kua ata nae akipewa hiyo nafasi ataikataa.

Lakini pia Polepole huyu huyu alisema kuwa Uchaguzi wa 2015 ukiwa wa huru na haki basi CCM ijiandae kukabidhi Ikulu lkn ni leo hii ndiye msemaji wa chama ambacho alikisema kuwa kukabizi Ikulu kama Uchaguzi utakua huru na haki.Hii ina maanisha kua uchaguzi haukua huru na haki ndiyo maana ccm bado ipo Ikulu.

Lakini pia tukumbuke msimamo wake kuhusu nafasi za uteuzi hizi ambazo alisema akiteuliwa hawezi kukubali. Je, leo nani mkuu wa wilaya ya Ubungo kama sio yeye.

PolePole alipinga sana kelele kuhusu katiba mpya sasa anaongonzwa na mwenyekiti ambae haitaki katiba mpya maana amenukuliwa mara nyingi kuwa hakuwai kutaja katiba mpya kwenye kampeni ili hali kwenye Ilani ya CCM ukurasa wa 183 imetajwa kabisa.

Sasa tumtegemee kukiona Humphrey Polepole aliyezibwa mdomo baada ya kushiba na kuishinda njaa iliyokuwa inamtafuna kama maneno ya Mwenyekiti wetu CCM aliposema Mayala atakuwa na njaa maana ata jina linamanisha njaa huku usukumani.

Vijana wa kitanzania tumieni njaa zenu kuzitafuta na kuzisaka nafasi na sio kutumia akili na elimu zenu kutatua matatizo ya jamii au kuokosoa serikali.

Bravo Polepole
 
Kuwa mwanangu uyaone .....tulifikiri kuyaona magorofa....NO...' ni kuona maisha yalivyo na yanavyombadilisha mtu ....anabadilika mithili ya kinyonga anavyobadilisha rangi kulingana na mazingira....
 
NI HIVI KWA DATA CHACHE SANA NILIZONAZO WATU WENGI WALIOWAHI KUFANYA KAZI KTK NGOs NI WACHUMIA TUMBO HAWANA USTAMILIVU WA KUTOSHA MAANA WAMEZOEA KUISHI KWA POSHO NA MALUPULUPU!
 
Niliwahi kuiona na kuisikia clip yake ya video akisema "kama uchaguzi ukiwa huru na haki CCM itashindwa"
 
Lowasa alisema hawezi hama ccm, ile wale wasiomtaka ndi9 waondoke. Leo yuko CDM.

Chadema walimuita Lowasa Baba wa Mafisadi na fisadi number 1. Na leo n kiongozi wa chadema na mpeperusha bendera.

Mbowe mara ngapi kala matapishi yake na kubadilisha gear kwenye gari ya mkokoteni??????
 
Niliwahi kuiona na kuisikia clip yake ya video akisema "kama uchaguzi ukiwa huru na haki CCM itashindwa"

Ni propaganda za gazeti (Mwananchi ) ndizo zilirusha kipande kifupi badala ya habari nzima, nnazo clip zote mbili (iliyopotoshwa na iliyo sahihi)

Iliyo sahihi inaeleza maonyo kwa Kauli za Chadema na CCM!!!!! iliyopotoshwa inachukua maneno aliyonukuu Pole pole toka Chadema na kufanya kuwa hayo ndo maneno yake
 
Kuwa mwanangu uyaone .....tulifikiri kuyaona magorofa....NO...' ni kuona maisha yalivyo na yanavyombadilisha mtu ....anabadilika mithili ya kinyonga anavyobadilisha rangi kulingana na mazingira....
Kwahiyo tuendelee kusomana tena sisi vijana kua ukinyonga ndio mtindo kama Pole Pole alivyofanya
 
Ni propaganda za gazeti (Mwananchi ) ndizo zilirusha kipande kifupi badala ya habari nzima, nnazo clip zote mbili (iliyopotoshwa na iliyo sahihi)

Iliyo sahihi inaeleza maonyo kwa Kauli za Chadema na CCM!!!!! iliyopotoshwa inachukua maneno aliyonukuu Pole pole toka Chadema na kufanya kuwa hayo ndo maneno yake
Sasa wewe unasema clip wakati watu tulushudia kwa macho na maskio alitamka mwenye kwenye mdahalo UDSM wewe unatuambia clip....Au ni wale wale
 
Kama bado haujausoma mchezowa Ngooshaa basi unaweza kuumizwa kichwa kabisa...Kuna tatu za kuziba watu midomo na kufunga fikra zao...Sasa hii ya Pole Pole inatumika sana ila mwisho wake ni mbaya...Unatupwa kama chupa la maji dampo
 
pole pole is a brave young man, km uncle magu kamuona anatafaa kuvaa viatu vya Nape basi apo ajakosea! manake ni bora kuliko wa jana..huyu hanaga magoli ya mkono,nimchapa kazi,ana busara kuliko umri wake na anathubutu kuliko vijana wengi pia knowledge na utashi wa uongozi anao.. niliwai kukutana nae( kwnye seminar tanga) miaka zaidi ya kumi iliyopita immediately nikasema huyu atakuja kua kiongozi mahiri sana wa nchi hii..kuliko hata yule bwana usafi..
 
Back
Top Bottom