Humphrey Polepole afunguka, Maaskofu semeni tu

Umesema Kweli tupu, malumbano ya nini ? Majibu tunayo maaskofu hawendi Taifa liibiwe , hao hao wakishakaba wezi naanzisha maneno nchi haina amani, tuwaeleweje jamani?
 
Kama askofu akiiponda serikali anaambiwa ni chadema, basi na askofu atakayeisifia serikali atakuwa ni ccm, full stop
 
Mh. Polepole niko na wewe na usiogope mtu au Askofu fulani. Enda zaidi usiandikie mate na wino unao maana baadhi yetu hatukuwasikia wakisema na pengine tunayosoma ni ya watu wanavyotaka tuwaelewe Maaskofu wamesema nini. Toa matamko yao makubwa matatu na sema haya ni itikadi ya chama fulani au si itikadi yetu (CCM). I like your neutral and uniting approach and in this way even our opposition will be listening to you more as the Polepole we know than as CCM knowing for sure you have a good history in Tanzania. I do not believe in the literal translation that "Opposition" means opposing CCM or vise versa.
 
Sifieni kama kuna mambo ya kusifia na onyeni kama kuna mambo ya kuonya lakini hekima busara kwa sababu kauli hiyo ni kauli ya moto inaweza ikatujenga inaweza ikatubomoa.Kuna namna nyingi za kurekebisha, tusije tukageuza na kujadiliana na Maaskofu, Askofu anasema tunamjibu, tutakuwa tunamkosea Mungu.

Mimi sitaki kusema Maaskofu wamekosea au hawajakosea lakini nataka kusema haya majadiliano ukiyaangalia yanatokea wapi? Tusije tukaingia kwenye mtego wa Ibilisi tukajikuta tukimtizama askofu fulani tunaona chama fulani. Askofu unaonekana kama chama fulani, mfano mimi ni mwanaccm nina dhambi zangu nataka kuja kuungama kwako, ntaungamaje kwako wakati wewe una itikadi tofauti na mimi?

Chama chetu kinaamini binadamu wote ni sawa, kinaamini katika utu, kinaamini katika kujitegemea, kinaamini katika heshima ya watu, kinaamini katika kusema kweli, kinaamini katika vita dhidi ya rushwa, kinaamini katika umoja kinaamini katika kujitoa, kinaamini katika kazi ni kipimo cha utu.

Sasa nikikutizama wewe unaamini katika ubwanyenye, unamini katika kuhodhi mali, unaamini katika umangimeza, unaamini katika mimi ni mwenyekiti peke yangu na hakuna mwingine. Sasa utaanza kunipoteza.

Huyu ni wa kupuuzwa tu. Kama hutaki kutubu kufa na dhambi zako.
 

Attachments

  • Polepole+ccm+ijiandae+kukabidhi.mp4
    235.8 KB · Views: 18
kwa hyo maaskofu wanawaonea ccm ya magufuli yake.?
waliyoyasema maaskofu NI UONGO?
 
NNimeamini bongo kuna vilaza wengi sana maana watu wengi wameshindwa kugundua hizi kelele na haya maazimio yanatokana na nini?? Bongo lala mnaona kawaida tu Hii ni vita ya kiuchumi nyumbuu nyie angalieni huko mbele. Hivi mnafikiri watu wa nchi jirani na hao watu wa makinikia na madawa ya kulevya wanaitakia hii nchi mema?? Ila kwa vile wabongo wengi vilaza wanafuata mkumbo tu hawajui hata hawa wanaowachochea wanataka nini. Za kuambiwa changanya na za kwako.
Hebu jiongeze bhas?!
Kwani MTU anapokiuka katiba asisemwe?
Anapoenda against asisemwe???
Sasa hapo INA maana nje wanachochea nn????
 
Utoto huo,kwani viongozi wa dini wanapowaombea wanasiasa mbona husemi kuwa watakuwa na uhusiano na chama fulani?Haya mambo yamechangiwa na wanasiasa wenyewe na wadau wao kwakuhubiri ubaguzi na utekelezaji wake.Utakuta mtu anasema mkimchaguwa mpinzani hamtapata maendeleo maana sisi ndiyo tunaoongoza,tunajuwa pesa tuchukuwe wapi.Wakati yanaongelewa hayo maneno walikuwa hawaoni kama wanahubiri chuki.
 
Maaskofu Hawa walishikwa kichwa na mbowe ziro watalipeleka taifa kubaya na matamko ambayo hata hawakubaliani

Pole pole na chama chako cha CCM kama mnahsisi KKT wamekosea wakamateni na mwape kisago kile kile ambacho mmewapa UAMSHO. kama hamtofanya hivyo basi ni wazi kuwa hamtendi haki, na muwaachie UAMSHO bila ya masharti kwa sabbabu mnaonesha double standards. Mumewakamata UAMSHO baada ya kutekeleza wajibu wao wa kikatiba kama watanzania walipotoa maoni juu ya uendeshaji bora wa muungano na kuwa na katiba bora na si bora katiba. Badala yake mmewapa kesi ya ugaidi. Basi na hao KKKT wakamateni na mkawaweke korokoroni. vyenginevyo, masheikh wetu watolewa jela wakaungane na familia zao.

Mchungaji/ padri akiikosoa serikali anaenziwa / anatunzwa kama yai jipya, yai la dhahabu . wakati sheikh akisimama kukiosoa serikali anachukuliwa kama mhalifu, kama gaidi, kama haramia, kama shetani,kama mwizi . hiyo haki iko wapi? Tunataka UAMSHO watolewe jela. wawe huru. Mateso na udhalilishaji mliowafanyia wakti wa mahojiano yanatosha kuwa ni adhabu, vyenginevyo waislamu tunaamini kuwa kuendelea kuwashikilia UAMSHO ni kuendeleza unyanyasaji dhidi ya waislamu na uislamu. ifike wakti dola ione aibu.
 
ni raha ilioje nchi ikiongozwa kwa sheria? kutoa maoni ni haki ya mwananchi kisheria. mahakama zipo, kama matamko, waraka nk vimevunja sheria, wahusika wapelekwe kwa pilato. kinyume chake ni kutaka kuiamisha dunia kuwa watanzania wote ni wajinga, kasoro mtu mmoja.
 
ni raha ilioje nchi ikiongozwa kwa sheria? kutoa maoni ni haki ya mwananchi kisheria. mahakama zipo, kama matamko, waraka nk vimevunja sheria, wahusika wapelekwe kwa pilato. kinyume chake ni kutaka kuiamisha dunia kuwa watanzania wote ni wajinga, kasoro mtu mmoja.
Da komenti kama hizi huwa zinanifariji sana,sasa huwa naamini kuwa kumbe Tanzania bado ina watu wenye akili nyingi.
 
Ovyo kabisa, askofu akiisema serikali anavalishwa uchadema. Watu wakiuawa wanyamaze tu, wahubiri viwanda. ccm mtatuteletea mauaji ya kimbari.
Aisee nimejaribu kulinganisha comment hii na kinacho daiwa majibu ya raisi kwa masskofu wakiluteri (wahubiri viwanda tuu) nimejifunza kitu kikubwa sana .hiko aja ya kuheshimu hisia za kila mtu
 
Back
Top Bottom