Hujuma zaanza 'Train ya Mwakyembe'

Wanatakiwa wavae sare zinazotambulika rasmi na wawe na vitambulisho wanavyovibandika kifuani.

Wale walioipa hii treni miezi 2 mpaka 3 iwe imekufa huenda dua zao zikajibiwa manake kwa mwendo huu mapato ni zero, watu wanakusanyia mifukoni mwao. Kesho utaambiwa shirika halina pesa ya kufanya ukarabati kwenye treni, au shirika limeshindwa kujiendesha.
 
Pamoja na uthibitisho huu wa wazi utashangaa hakuna hatua itakayochukuliwa. Sana sana itaundwa tume ya kuchunguza, halafu matokeo yake hayatatangazwa.
 
Nilishawahi kupendekeza kwenye post fulani kwamba TIKETI ZISIKATWE KWENYE TRENI utapatikana mwanya wa rushwa kujipenyeza

Ilitakiwa tiketi zikatwe kwenye vituo. Yaani watu wafike mapema. Asiye na tiketi no kusafiri kwasababu ndani ya treni watakuwepo wakaguzi

Ikiwezekana ziuzwe hata zile za tiketi moja inayolipia safari za wiki nzima. Abiria achague kutokana na uwezo wake na pia kama hataki karaha ya kukata kila siku
 
Ndiyo maana hatuendelei!sasa hivi utasikia shirika limeshindwa kujiendesha!

Watanzania uaminifu zero! Najaribu kutafakari daladala za Afrika kusini hazina kondakta. Watu mnachangishana wenyewe kwa wenyewe na kujimegea chenji yako kisha dereva anapewa jumla ya nauli.

Nahisi kibongobongo kila siku dereva angekuwa anasimamisha daladala kutafuta yupi hajalipa! Hahahahaha
 
Nadhani Tanzania kila mtu ana chembechembe za ufisadi isipokuwa ni mianya tu ya kufanya hivyo haijapatikana

Sent from my GT-S5570 using Tapatalk 2
 
Pamoja na uthibitisho huu wa wazi utashangaa hakuna hatua itakayochukuliwa. Sana sana itaundwa tume ya kuchunguza, halafu matokeo yake hayatatangazwa.

Wakuu, ningependa sana watu wa serikali ya TZ waweke watu wao humu ndani ya JF, ili wawe wanafuatilia taarifa muhimu kama hizi na kuzichukulia katua stahiki mara moja.

Huu ni wizi na hujuma ya wazi. Haiingii akilini uongozi mzima wa TRL ushindwe kubashiri wizi na hujuma kama hizi za wazi tangu kitambo kwa kisingizio cha kukosa tiketi?

Hii huduma tangu imeanza kuzungumziwa mpaka ikawa established walikuwa wapi wasijiandae? Au hawakupenda Mhe. Mwakyembe kufanikiwa katika ubunifu wake huo ili daladala zao ziendelee kuvuna?
 
Route moja jamaa ana uhakika wa kukusanya si chini ya 40000/=
 
Haya ndio mambo ya kuanzisha vitu bila ya proper planning. Idea ilikua nzuri lakini ingebidi waboreshe infrastructure ya hizi treni ili kupunguza matatizo wanayopata watu hivi sasa kama huu wizi. Inabidi wachukue hatua haraka kusimamisha huu wizi amasivyo hii treni haiwezi hata ku break-even.
 
Umaskini unahusiana sana na mipango[planning] pamoja na dira[vision]. kwa mfano huyo anayekusanya kwa kuiba waweza mkuta ananunulia rafiki zake mbuzi choma. Watakula na kusaza!! baada ya hapo anaanza kujisifu kuwa aliwalisha rafiki zake mbuzi mzima wakti anajisifu hivo, atakuwa anatembea kwa mkuu kutoka ubungo hadi posta kwa kuwa usafiri ni mgumu na kwamba TRL ilishakufa!!
Watanzania lazima ifike mahali kila mmoja aone ubadhirifu wa mwenzake au jirani unaleta madhara si tu kwa hiyo badhirifu bali hata kwake!!
 
Si wanunue Tickets Validators au Ticket Punching Machines?

Nafikiri wakitembelea nchi zilizoendelea, watapata nyingi tu used kwa bei nafuu ili zitumike kuanzia.

Humo ndani wawepo wakaguzi tu wa ticket na siyo kununua ticket. Kama mtu hana basi anunue na faini kidogo.

3082332422_6630d1a07f.jpg
 
Hivi hata kudhibiti mapato wanasubiri mpaka Mwakyembe aje? by the way watanzania wote ni wezi tu wakiachiwa nafasi
 
Wale ma TT wa zamani wako wapi?walikuwa wanafaidi sana pesa wale akienda Mwanza na kurudi anakuwa zaidi 1mil kwa kweli,maana ana power sana ya kufanya lolote kwa abiria...wanatisha sana
 
Hawa ndio Watanzania waliolaanika...sio ajabu kwa haya yanayo fanyika sasa...mashirika yote ya Umma yaliyobinafsishwa yalikufa kwa mitindo type hiii....sasa kwa hili kama style ndio hii kuna picha kama mbili hivi hapa..inawezekana ikawa ni maagizo rasmi kutoka kwa kundi flani kukwamisha jitihada za Muheshimiwa ionekane kuwa alitaka sifa lakini si mnaona imeshindikana...au ni kwa makusudi linafanyika hili kwa sasa kwasababu ni mwanzo ili iwe ndio mpenyo wa hujuma za mapato kuingia kwenye mifuko ya watu...kwa kutengeneza mazingira from the day one kwamba matapo halisi Train inapojaa au kuwa tupu yasijulikane huu uwe uchochoro mzuri wa kuiba...kwa sababu kwa vyovyote vile huduma hiii haiwezi kuendeshwa kwa hasara..hapa ni faida tupu kwa hali ya usafiri ilivyo Dar es salaaam.

Sasa Muheshimiwa mimi nafahamu wewe ni mtembezi sana mitaaa hii....Kaka usicheke na Kima..kama ukicheka na Kima aibu itakuwa yennu...Fukuza watu hapa kama huna akili sawasawa..usicheke nao hawa Fisi maji kabisa...ni hayo muheshimiwa

Mbona Haya ndio mambo yenyewe!! Kama issue ya Bandari, watu wanadiriki kununua magazeti na kusifia Uozo wa Pale Bandarini!! Mwakyembe songo Mbele baba usilale!! Wewe ndio Nyota yetu Inayong'ara
 
waweke milango ya kuingia na kutoka stesheni pa kupandia na kutoka kama ya Azam Marine

578652_444053832284612_1334242014_n.jpg

http://sphotos-c.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-snc7/578652_444053832284612_1334242014_n.jpg

its good Idea Mkuu, Lakini hili linaweza kufanyika katika vituo vyote, Labda vituo vikubwa vya mwanzo. Nashauri waweke mitambo ya mtu kukata tiketi mwenyewe kabla ya kuingia kwa kadi maalum, TT wawe na kazi ya kukagua kama watu wote waliopanda wanazo ticket. Atakayebainika kukosa ticketi ndani ya tren apigwe faini kubwa na akishindwa afungwe. With time kila kitu kitajiendesha chenyewe. Nchi za wenzetu utaratibu huu umesaidia hata wale wanaokwepa kulipa wanaogopa kubamizwa faini.
 
Back
Top Bottom