Hujuma Pantoni za Kigamboni

Sijaelewa dukuduku lako hasa ni lipi? Kutembea dakika 50 au kuiba mafuta? inamaanisha wakiwasha engine zote nne na kutembea dakika 25 ndio mafuta hayaibwi? Watanzania tuache kuongea ongea bila ushahidi,ulijaribu kuwauliza kwanini inatembea engine mbili? Report ya uwekaji mafuta na utumiaji wa mafuta ulionyeshwa na ukajiridhisha kwamba mafuta yanaibiwa?

Ungekuwa unaishi Kigamboni hayo maswali wala usingeuliza lakini watumiaji wameona hali halisi na tumeomba hata Mbunge kama hajui ama haoni nae aingilie kati

Picha tu wanakataa usipige sembuse logistics zao za mafuta . Sisi tunawaona wanavyoyauza wakifika ng'ambo moja kutoka ingine

Kero ni pamoja na kutembea slowly kwani kama una dharula ya mgonjwa una mpeleka hosp inakuwa ni mtihani sanaaa.

Sasa wakishayaiba hayo mafuta maana yake trips zao za ofisi against matumizi ya engine ndio wanafidia kwa kutupeleka slowly
 
Hata kama yanakidhi idadi mkuu yamefungwa na kufuli na funguo zinabaki ofisin na ni chuma tupu unategemea tutatoka ikitokea bahat mbaya

Halafu unakuta mengine yametobolewa na panya, wanashindwa hata kubuni sehemu za kuweka life jacket ambapo panya hawezi kuingia. Mfano kujenga kwa kutumia wavu mkubwa kama ilivyo sasa na kuongezea wavu mdogo au kuweka vioo kwa ndani ya wavu.
 
Yah atleast wangeweka vioo vya plastick vidogo ingekua kama likitokea unabomoa unatoka
 
Halafu kwa ajili ya joto ksli wakati wa msongamano ndni ya banda la kusubiria wameweka feni, mimi nadhani wangeweka 'roof ridges ventilators' ndio zinafanya kazi vizuri kuliko hizo feni.

Pia ndugu zangu hawa wangefikiria juu ya uwezekano wa kuongeza milango ya kutokea kwenye banda kwavile abiria huwa ni wengi sana na husongamana mno wakati wa kutoka ili kwenda kwenye pantoni.
 
Suluhisho ni dogo tu!! Ferry ya kuvuka inahitaji kubinafsisha sector hiyo !! Waje wawekezaji kadri ya kukidhi haja ya wasafiri...
yaani wasafiri 1000 kwa pantoni 5 hadi 10 zichuana hapo !! na kila idadi ikiongezeka pantoni ziongezwe !! Ndo tutaendelea, Kwani mteja (msafiri) ni mfalme, Na ni haki yake kusave time yake " time is money "
The Fixer Barasu KATIBUA The Boss

Umenikumbusha kauli ya profesa mmoja hivi juu ya uwekezaji!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo watataka 10% yao.
Kuna sehemu jamaa amejenga hoteli ya kitalii. Barabara inayokwenda huko ilipo hoteli yake imeharibika sana. Jamaa alikuwa teyari kuijenga kwa gharama zake na kuisimamia. TANROAD walimwambia haruhusiwi kuisimamia yeye bali anatakiwa aipe hiyo pesa TANROAD ili waijenge. Makadirio aliyopewa na TANROAD yalikuwa makubwa sana kuliko aliyopewa na kampuni ya ujenzi. Pia aliambia alipie ada fulani ya ujenzi ambayo nayo ni kubwa. Jamaa aliamua kuachana na ujenzi huo wa kujitolea kwani ingekuwa ni hasara kubwa.
Duuh... nimezimia !! nilipozinduka Nikapigwa na mduaoo!! nashukuru sijafaa!!
Ahante muungwana !!
 
Back
Top Bottom