Huduma duni za afya zinahusiana na mgomo wa madaktari mwaka 2013?

mlekulechoma

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
1,367
1,057
Suala la afya kwa wananchi wa Tanzania hususani wa kipato cha chini limeendelea kuwa na changamoto kila kukicha!ni jambo la kawaida kusikia hospitali zetu zote kuanzia Muhimbili ambayo ndiyo hospitali kuu ya taifa hadi kwenye zahanati zetu huko vijijini kwamba hakuna dawa za kutosha pia vifaa tiba hakuna!

Mgomo wa madaktari ambao ulipelekea kuteswa na kuumizwa vibaya karibu na kifo kwa kiongozi wa jumuiya ya madaktari Dr. Ulimboka ninaamini bado unaendelea ila kwa mtindo tofauti!

Siku hizi wataalam wetu hawa wa afya hawafanyi kazi kwa moyo wa wito kama zamani! Nilibahatika kuongea na daktari mmoja mwandamizi wa hospitali kubwa hapa nchini kuhusiana na suala hili, alisema mgomo wao ulikuwa ni kudai maboresho ya huduma za afya na wafanyakazi katika sekta hiyo kwa ujumla.Majibu ya Rais yaliwakatisha tamaa sana.

Alisema anaetaka kazi afanye na siyetaka aache!Kinachoendelea sasa ndio matokeo ya mgomo huo na majibu ya Rais wa nchi.

Wataalam hawana muda wa kutafuta vifaa tiba/dawa katika hospitali zetu!

Wengi wa wataalam wetu wanavijiwe vyao hawana muda na hospitali zetu!

Baadhi yao wameingia kwenye mashirika binafsi hivyo kupelekea upungufu mkubwa wa wataalam katika sekta ya afya!!

Waliobaki hawana morali ya kazi,wanasubiri mshahara siku ziende!

Je, nini kifanyike kunusuru maisha ya watanzania wenzetu hasa wa kipato cha chini
?
 
Kila mtu kwa nafasi yake ana wajibu wa kufanya jambo katika hili.
Raia : ana wajibu wa kudai kwa nguvu zake zote na kuhakikishiwa huduma bora kutoka serikalini
Daktari: ana wajibu wa kuhakikisha anatoa huduma bora ya kiwango cha juu kwa uelewa wake wote na kumshawishi mwajri wake kumwezesha kufanya hivyo. endapo anaona mazingira ya kazi hayaendani na taaluma ana wajibu wa kuacha kazi hiyo. Ki ukweli si jambo la busara kwetu sisi madaktari kutibu nusunusu huku wagonjwa wanatufia. endapo tungekuwa na umoja wote kwa umoja wetu tukaacha kazi serikali ingetusikiliza. wengine wetu ni wavivu tu na wala si mgomo .....
Serikali: Isitishe kupeleka wanasiasa nje kutibiwa kwa magonjwa yanayotibika hapahapa Tanzania. huo ni wizi .
 
Back
Top Bottom