Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Salamu zangu kwenye Kongamano la Katiba Day
01/07/2021.
Ndugu Mgeni Rasmi Mh Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa.
Mheshimiwa John Mnyika Katibu Mkuu Chadema Taifa
Watoa Mada wakuu Prof Rwaitama na Askofu Emmanuel Mwamakula.
Wageni waalikwa wote na vijana wenzangu, itifaki imezingatiwa!
Walionitangulia wamezungumza mengi mazuri kwa mstakabali wa mchakato wetu wa Katiba Mpya.
Mimi ninaomba nizungumze jambo moja muhimu ambalo linaukabili mchakato huu tangu ulipoanza Mwaka 2011. Na jambo hilo ni Mitazamo tenge juu ya Katiba Mpya.
Lakini kabla sijaanza kueleza mitazamo hiyo naomba niwaeleze vijana wenzangu, Sisi Vijana tuliopo hapa hatujawahi kuandika Katiba ya Tanzania, Wazazi wetu na pia viongozi wetu mliopo hapa hamjawahi kuandika katiba ya Tanzania, Mababu zetu pia hawakuandika katiba ya Tanganyika wala katiba ya Zanzibar.
Katiba ya mkoloni iliandikwa na watu wachache (6) tu ndani ya ofisi ya Ukoloni Mjini London Uingereza 1919. Ifahamike kuwa huko nyuma kabla ya vita vya kwanza vya dunia alivyoshinda Muingereza, alikuwepo Mjerumani ambae aliitawala Tanganyika kama Kampuni na kuiongoza kama Kampuni la faida kwakutumia MoU badala ya katiba. Ingawa kwa mwaka mmoja wa 1919 nchi yetu iliitwa majina 9. Ambapo, Kwanza iliitwa Smutsland, Pili ikaitwa Eburnea, Tatu ikaitwa Azania, Nne ikaitwa New Maryland, Tano ikaitwa Windsorland, Sita ikaitwa Victoria, Saba ikaitwa Kilimanjaro , Nane ikaitwa Tabora na hatimaye jina la Tisa ikaitwa Tanganyika January 1920.
Katiba ya Tanganyika huru licha ya kuirithi Katiba ile katiba ya kikolini lakini kwa sehemu kubwa ilitokana na msingi wa katiba ya TANU, ambayo nayo msingi wake ni katiba ya chama cha AA iliyoandikwa na raia wa Gold Coast Dr James Emman Kwegyir Aggrey 1927. Chama cha AA rais wake Mwasusu akiwa Mwalimu Cecil Matola.
Lakini pia Mwalimu Julius Nyerere wakati wakiunda chama cha TANU 1954 walilazimika kuazima sehemu ya katiba ya chama cha CCP cha Ghana chini ya Dr Kwame Nkurumah.
Hadi hapo mtaona Katiba ya Tanganyika wala Tanzania haikuwahi kuandikwa na Wananchi bali watu wachache waliandika kwa niaba ya wengi, huu ulikuwa mfumo wa kale ambako dunia leo haiko huko, Leo dunia ni shirikishi na ya kidemokrasia.
Kwa mara ya kwanza 2013 Watanzania tulishiriki kuanza kuandika katiba mpya, na kwa sehemu tu hatua tulishaivuka kwakutoa maoni yakwamba tunataka katiba ya aina gani kupitia Tume ya Jaji Warioba. Maoni yale ndio ushiriki wetu kamili na thabiti kwaajili ya Katiba Mpya.
Dhana tata juu ya Katiba Mpya
Baada ya Maoni na mchakato kuanza wa Katiba Mpya, Ziliibuka dhana tata nyingi sana, zikianzia kwenye kutunga sheria ya mchakato wa Katiba Mpya, Kwenye Kanuni za Bunge la Katiba na mitazamo mingine imeendelea kuwepo hadi leo. Nitaorodhesha kwa uchache kama mifano hai.
1. Katiba Mpya itaiondoa ccm madarakani
2. Katiba Mpya itaisaidia Chadema kwenda Ikulu
3. Katiba Mpya itamuondolea rais Madaraka
Dhana hizi zote tunao wajibu wa kuzifafanua na kuwaelimisha wenzetu wanaojenga dhana hizi potofu.
Dhana kwamba Katiba Mpya itaiondoa ccm Madarakani ni dhana potofu kwakuwa Katiba mpya ni mstakabali wa kitaifa kati ya watawala na watawaliwa, ni mstakabali juu ya wakulima, Ni mstakabali juu ya wafanyakazi, Ni mstakabali juu ya wavuvi nk. Mstakabali huu hauhusu kundi la SIASA tu bali nchi nzima.
Dhana kwamba Katiba Mpya itaisadia Chadema kwenda ikulu, ni dhana mfu, na kama kuna yeyote miongoni mwetu hapa anafikiri hivyo namuombeni afute mawazo hayo, Tukikifikiri katika muono huo kamwe hatutapata katiba ambayo ndio mstakabali wa taifa lote na sio mstakali wa Chadema wala wa ccm tu.
Dhana kwamba Katiba mpya itamuondolea Rais Madaraka, Si kweli, bali Katiba Mpya itapunguza madaraka ya rais ya sasa na kumwekea misingi imara ya kuongoza nchi kama rais kuliko ilivyo sasa anavyoongoza kama mfalme. Katiba ya sasa inasema, Katika kutekeleza madaraka yake, Rais hatasikiliza wala hatashauriwa na mtu yoyote au kikundi chochote,
Katiba mpya itaweka sawa eneo hilo na kutomfanya Rais kuwa Mungu-Mtu.
Ni wajibu wetu vijana nchi nzima bila kujali chama ama itikadi, kuongoza vuguvugu hili kuhakikisha mchakato wa katiba mpya unaanzia kwenye Rasimu ya Jaji Warioba.
Asanteni sana vijana wenzangu!
Na Yericko Nyerere