Hotuba ya Rais Magufuli kwenye maonesho ya SADC na Shauku yake Kutengeneza mabilionea Tanzania

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,467
2,861
Moja ya vitu vya msingi katika hotuba ya kufungua maonesho ya viwanda wiki hii Mhe. Rais JPM ame-spearhead kukuza uchumi wa Afrika Tanzania ikiwemo kupitia viwanda. Aidha majuma machache yaliyopita JPM alijinasibu amekusudia kutengeneza mabilionea wapya zaiidi ya 100 hapa nchini. Hili linawezekana hasa kama kuna mikakati itafanyika. Huko mbele ntafafanua.

JPM alidadavua kwa kina ni namna gani Afrika (Tanzania ikiwemo) tunauza mazao ghafi kama vile pamba, cocoa, kahawa, korosho, katani, chai n.k. Baada ya mazao ghafi ambayo sisi wenyewe tunazalisha kwa nguvu zetu na mashambani kwetu kwenda Ulaya, Asia na Marekani sisi hao hao tunanunua finished products kwa fedha nyingi za kigeni. Tanzania na nchi nyingi za Afrika zinajiendesha kwa Balance of Trade Deficit badala ya Balance of Trade Surplus.

Tuna wajibu kusimama na JPM maana uwepo wa viwanda Tanzania; wafaidika wa uwepo wa viwanda ni Watanzania kwa namna mbalimbali ikiwamo;

Watanzania kupata kazi (ajira viwandani),
Viwanda vitakuza sekta ya huduma ikiwamo logistics kusafirisha raw materials and finished products toka viwandani

Sekta ya kibenki kukua kwa kuongeza wateja wanaoweka akiba na wafanyakazi kukopa ili kujenga makazi bora ya kuishi au kununua usafiri au kukopa machinery na kuwekeza pia kwenye small industry kama machinery za kusaga na kusindika unga;

Sekta ya bima ya Afya kupanuka

Sekta ya pesheni kupata wateja zaidi

Sekta ya huduma za kisheria kupata wateja kupitia mikataba mbalimbali kuandaliwa
Tax base ya TRA kuongezeka (hii ikiendana na kuongeza fursa za ajira TRA)
Kupunguza imports ya vile tuna bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani
Kuongeza exports za products za viwanda ambavyo mimi na wewe tuna platform ya kuvijenga kama tuna fedha za kuwekeza.

Kukua kwa sekta ya umma (ikiwemo kutoa ajira) kwa taasisi za huduma kama TBS ambazo zinahusika kudhibiti/kuimarisha ubora

Ongezeko la mishahara ya wafanyakazi wa umma kwa kuwa TRA itakuwa na makusanyo makubwa zaidi na hivyo uwezekano wa ongezeko la mishahara kuwepo.

The list goes on...

Mwl. JK Nyerere baba wa Taifa aliacha viwanda vya nguo, viwanda vya Ngozi, viwanda vya kusagisha nafaka, viwanda vya kuchakata katani na kutoa magunia, viwanda vya zana za kilimo, viwanda vya sukari, viwanda vya zana za kilimo (ikiwamo kuzalisha mbegu na Mbolea). Leo tuna import mpaka mbegu za nyanya.

Mwl. Nyerere alifanya. Mwisho wa siku viwanda vikiwepo na vikatoa fursa ya kukua uchumi wa sekta ya umma na sekta binafsi.

Leo Tanzania ikishinda kwa uwekezaji, sisi sote kwa namna moja au nyingine tunafaidika.

JPM go go go. Tujenge viwanda, watu wafanye biashara, mauzo ya bidhaa za ndani yaongeze mzunguko wa fedha, vijana wengi wapate ajira na tuone viwanda viki-akisi na kukuza uchumi wa Watanzaniawengi wafikie maisha ya kipato cha kati (middle class earning countries)

India miaka ya mwisho ya 1960 iliamua kuanza na kilimo kama mkakati wa kujikomboa na food imports. Kwa miaka 3 waliondokana na kuwa tegemezi kwa chakula kuanza ku-exports.

Natamani pamoja na mengi tutakayofanya, Tanzania tupunguze imports ya samaki za uzani wa tani laki 4. (Kuna Mtanzania ana mradi wa kuzalisha tani 120,000 kwa mwaka kwa kutumia worldclass technology toka ughaibuni) TADB au TIB wangekuwa wana jicho la uwekezaji kwa kasi ya JPM ndani ya miezi 9 Watanzania wangejenga uwezo na baadae uwekezaji kama huu ungegusa wengine kwa upanuaji wa biashara.

Nina shauku ya kuona tunapunguza imports ya maziwa kwa zaidi ya bil 150/mwaka.

Hayo machache niliyoyadodosa, yakiendelea kufanyika nje, tafsiri yake tunatoa ajira kwa wenzetu wazalishe na kutuuzia sisi wakati tuna platform ya kuzalisha.

Hakuna rocket sayansi. Ni utashi wa uongozi ambao JPM ashauonesha. Ni wakati mzuri wasaidizi wake nao wawe na kasi kwenye maamuzi yenye tija na kupunguza michakato ambayo huchukua muda na kuna wakati tuna-miss target. Time is always key hasa kwenye uwekezaji ukijumuisha uanzishwaji wa viwanda.

Kwenye kujenga uchumi wetu; Watanzania sote tuko vitani kugombea fedha yetu isipotee kwa imports ambazo tunaweza kuzalisha, ila pia kugombea kupata forex kwa kuzalisha kwa viwango na ubora unaokidhi soko la nje pia. Vitani policies haziamui kila kitu. Ila strategy ni key factor kushinda vita ikiwamo vita vya uchumi. Strategy hubadilika tokana na wakati na soko lipi bidhaa inaingia kuzalishwa au technology ipi inatumika.

Mkoloni wa Tanganyika tulimtoa kwa Mwl. Nyerere ku-present case UN. Dunia akatuelewa mkoloni mwingereza akatoka 1961. Mkoloni Mwingireza huyo huyo kumtoa Zimbabwe na kumtoa Kaburu Namibia na “Bondeni” hapo ilibidi mtutu wa bunduki utumike. Na ndipo SADCC ya kwanza kunzishwa na makao makuu yakawa Gaborone Botwasana. Mwl. JK Nyerere aliona Botswani ipo eneo la kimkakati na ilikuwa ni nchi huru tayari. Botswana imepakana kwa kaskazini Zimbabwe na imepakana na South Arica kwa kusini.
Yet kambi za mafunzo ya kijeshi zikawa Morogoro, Kongwa na Mbeya. Vijana wakakuwa trained hapa, wanatua Botwasana enzi za Sir. Khama, wanaingia kupigana na mkoloni. Mkoloni yuleyule ila strategy hazikiwa zinafanana. Huu ulikuwa mkakati mahsusi na kabambe.

Nirudi kwenye mada ya kufanya kweli na kutoboa kiuchumi ili kutengeneza mabilionea wa Kitanzania. Nilikuwa nasoma desa moja linaonesha katika uchumi 100 mkubwa duniani 51 ni uchumi wa makampuni na 49 ni uchumi wa nchi (if you take into acount of the 100 largest economies of the world 51 are corporations and 49 are countries)

Uchumi wa Walmart ni mkubwa kuliko nchi ya Poland na Ugiriki. Uchumi wa Mitsubish ni mkubwa kuliko Indonesia. Uchumi wa GM Motors ni mkubwa kuliko Denmark. Mtafiti ambae kaandika taarifa hizi ambae pia ni kachero wa masuala ya kiuchumi kaingia ndani akionesha bajeti ya kijasusi wa kampuni ya GM Motors (Competitive Intelligence tool) ni kubwa kuliko bajeti ya kijasusi ya Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa.

Dhana mahsusi ambayo ni msingi wa kuondoka nayo kwenye desa hilo, sio kila kitu kinaweza kutegemea tender za wazi, michakato ya wazi hasa kwenye uwekezaji wa viwanda vya kimkakati… ni kwamba tutachelewa kufika, au jamaa (competitors) wakijua hapa tunatoboa ni rahisi ku-divert agenda ya kukuza uchumi wetu au kutuwahi kuingiza mzigo sokoni maana kila kitu kiko wazi.

Nakubaliana na michakato ya wazi ya mambo mengi ya uwekezaji, ila jamaa wanachofanya katika mambo ya biashara za kimkakati; 20% yanakuwa hayatangazwi wanataka kufanya nini. Jamaa wanajipanga, wanafanya homework mara wanaibuka na wanafanya kweli. Mzigo unaingia sokoni wanapiga hela kupitia mauzo ya bidhaa ndani na nje ya nchi zao. Wanajenga viwanda, wanatoa ajira wanakuza tax base ya nchi zao. Wanakuza brand na market share sokoni.

Watanzania; Kahawa, Pamba, Chai, Korosho, Cocoa, Katani haya ni mazao ya kimkakati. Ripple effect yake ni kubwa mno. Ni vema akili za kila wanaofikiri kwa "picha kubwa" zikatafutwa bila kutegemea ma-prof na ma-dokta pekee ya vyuo vyetu. Kuna brains za Watanzania wenye creative, innovative na futuristic DNA. Tukiwatafuta na kuwatumia tuta-maximize value chain Agro-processing, tutakuwa na agro-industries, tutatumia technology na eventually tutauza finished products kwa soko la ndani (tupunguze imports) ziada kuuza soko la nje (kuongeza exports). Hata ndege yetu ikienda China, India na UK inaondoka na mzigo wenye ubora na viwango made ni Tz.

Uchumi wa Tanzania unaweza kukua bila shaka. Watanzania tukiamua tunaweza. Na tuamue sasa.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu msaidie JPM atimize shauku yake ya kutengeneza mabilionea wapya. Nami nashawishika watapatikana kwa hakika.
 
Mchawi ni yeye mwenyewe hajui njia ya kufika huko anadhani ubabe ndo utaleta viwanda kumbe kuna kitu kinaitwa diplomasia .aonyeshe na kuishi katika diplomasia atafanikiwa
 
Kuna swali liliulizwa, kama tulikuwa na viwanda vingi ni kwann maisha ya kipindi hicho yalikuwa na changamoto sana mpaka kufikia foleni madukani kupata bidhaa? Ni viwanda havikuwa na matokeo chanya kwenye uchumi, ni ujamaa Au mambo yalikuwa sawa sema vile vita vya UG vikaaribu?
 
Hao mabillionea 100 inawezekana kabisa si hawa wasukuma wenzake anaowapa vitengo kila siku.
Nadhani sio sawa kuwabagua wasukuma wachache walio kwenye sehemu ya utawala wa JPM kwani wana haki sawia na Watanzania wengine kwenye kutekeleza majukumu ya kuhakisha ifikapo 2025 Tanzania inakuwa middle class earning country. So far serikalini kwenye wakuu wa Idara, Mawaziri na wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya kuna uwakilishi wa kila kabila.

Kubwa kuliko yote, ni vema tukawa objective kwani maaduni zetu ni umasikini, ujinga na maradhi. Tukijikita kwenye kuwadhibiti hawa kwa kuongeza thamani ya mazao ya kilimo kwa viwanda, kahawa Kilimanjaro inatakuwa isiendelee kuuzwa kama kahawa ghafi
Kahawa na chai ua nyanda za juu inatakiwa isiuzwe kama kahawa ghafi.
Pamba ya kanda ya ziwa isiuzwe kama ghafi.

Viwanda vitaongeza ajira na ukwasi katika jamii ya Watanzania na kila mtu wa pende yoyote ya nchi atafaidika katika mnyororo wa thamani wa kuongeza thamani, kudhibiti ubora, kusafarisha ndani na nje ya nchi na kupata tija kwa shughuli za uzalishaji tunazofanya.
 
Tatizo la watanzania wengi wanapenda sana" kutengenezewa" siyo "kujitengenezea" kwa haraka haraka viwanda vilivyokuwapo apo nyuma enzi za Mwl vilizalisha bidhaa zilizokosa ubora na kushindwa na washindani wao ktk ulingo wa soko, kutoka na ushindani wa technologia, mwisho tukashindwa kutengeneza vyetu kwa ubora zaidi, tukaanza kutengenezewa na kuhuziwa kutoka nje, tukaisha kabisa na akili ikalala viwanda vikafa.
Apa insue ni kuwekeza kwwnye technologia za kisasa tuendane na wakati
 
Zilonga mbali zitendwa mbali, mtaji milioni 100, kodi 2bilion!! Hapo unapata mabilionea kwa kuwapa hela si kwa ubunifu na kufanya biashara!!
 
Tatizo la watanzania wengi wanapenda sana" kutengenezewa" siyo "kujitengenezea" kwa haraka haraka viwanda vilivyokuwapo apo nyuma enzi za Mwl vilizalisha bidhaa zilizokosa ubora na kushindwa na washindani wao ktk ulingo wa soko, kutoka na ushindani wa technologia, mwisho tukashindwa kutengeneza vyetu kwa ubora zaidi, tukaanza kutengenezewa na kuhuziwa kutoka nje, tukaisha kabisa na akili ikalala viwanda vikafa.
Apa insue ni kuwekeza kwwnye technologia za kisasa tuendane na wakati
Ndugu yangu;
Maziwa ya kusindika kwenye kiwango cha UHT (Ultra-high temperature processing) yalikuwa na Ubora na kiwanda cha Utegi mkoani Mara kilikuwa cha kwanza chenye kiwango hicho kilikuwepo miaka ya 80. Mwl Nyerere aliwekkwa lengo la kuongeza tija na thamani kwa maziwa kwa wafugaji. Kulitokea tatizo la kupewa watu wasio na vision kwa kutengeneza product diversification.
Kiwanda cha maziwa ya ASAS cha sasa ilikuwa mali ya Umma.
Kulikuwa na kiwanda cha maziwa Arusha wasiojali wakauza Kenya. Tulipeleka ajira na ongezeko la thamani ambalo lingefanywa ndani.
Kulikuwa na General tire kuchakata mpita, wasiojali wakauza Kenya. (Tulipeleka ajira na ongezeko la thamani ambalo lingefanywa ndani)
Tulikuwa na viwanda vya Ngozi Moro na Mwanza-Tanaries. Vikauzwa na machine waliouziwa wanajua walipeleka wapi (Tulipeleka ajira na ongezeko la thamani ambalo lingefanywa ndani)

On serious notice tulikosa wazalendo wa kujenga uchumi wetu kwa faida jumuishi.

Na hapa ndipo natoa rai wa wakubwa wenye uzalendo wa kweli, kuna haja ya kuwa na jicho la exploration ya kizazi kipya cha Watanzania wenye kiu ya kuwa game changers. Na moja ya jukumu jipya la hao new Tz investors iwe ni kuandaa succession plan inayotekelezeka ya kuwaachia kizazi kijacho mfumo imara wa uwekezaji wenye ubia kati ya umma na sekta binafsi ya Kitanzania.

Chungulia economic Intelligence strategy ya Japan na Ufaransa hapa unaweza kupata taswira wenzetu wanafikiri kwa jicho lipi na tokea hapo tukaja kwa pamoja ili tuamua nasi tuje na model gani

Hawa hapa chini ni Wajepo

1565680108270.png


Hawa hapa chini ni Wafaransa

1565680199365.png


Ukicheki model zao za kukuza uchumi unaweza kuwa na picha ni namna gani jamaa wako serious kujenga uchumi wao. Mipango ya miaka 10, 20, 30....
Tunayo kazi ya kufanya na wakati ni sasa kufanya kwa pamoja kutengeneza mabilionea Zaidi ya 100 kwa kujenga uchumi jumuishi na endelevu kupitia sekta ya viwanda na biashara
 
Back
Top Bottom