Hotuba ya Rais Kikwete ya Mwisho wa mwezi Julai, 2014

mm ccm ila rais kwa hili unastahiki lawama sana, kwani ulipokutana na tume huko kabla ya rasmi kuisaini hawakukupa mda wa kutoa maoni yako ?
 
Kifungu hiki kimeniacha hoi!! Hivi kweli hajui kama ushauri wake huu ndio umeharibu Bunge la Katiba na kulivuruga? au anafanya mzaha huyu jamaa?

Siwezi kukumbuka pahala po pote ambapo Mhe Dr. Rais Jakaya Kikwete amaeishawahi kuonesha seriousness katika maana hali ya neno 'serious'! Ni mtu wa mizaha tu!!! My first reaction moyoni mwangu kwa hotuba yake ya ufunguzi wa BMK ilikuwa ni kwamba Tanzania inahitaji mujiza litokee jopo la wise men and women kufungua kesi mahakama kuu ya kusimamaisha mchakato wa Katiba Mpya. Wiki chache baadaye nilifarijika sana nilipoona wise men na women wamejitokeza kwa njia ya UKAWA. Huyu bwana anatania.
 
Nitashangaa sana siku nikiona upinzani unaacha kupinga. Wana kazi ipi zaidi ya kupinga?
 
maoni yake binafsi hakupaswa kuyatoa kwenye jukwaa rasmi la mkuu wa nchi kuzindua bunge. isitoshe, maoni yake si tayari alishatoa kwenye chama chake?
 
hahahahaa rais bora kwa nani? Kijigazeti cha kule marekani!! Maajabu haya.

kijigazeti hicho hicho kingemzawadia ukawa mmoja tusingekunywa maji, kwa ni rais wetu mpendwa imekuwa nongwa, acha kucheka kicheko cha wivu wa kijinga
 
siwezi kukumbuka pahala po pote ambapo mhe dr. Rais jakaya kikwete amaeishawahi kuonesha seriousness katika maana hali ya neno 'serious'! Ni mtu wa mizaha tu!!! My first reaction moyoni mwangu kwa hotuba yake ya ufunguzi wa bmk ilikuwa ni kwamba tanzania inahitaji mujiza litokee jopo la wise men and women kufungua kesi mahakama kuu ya kusimamaisha mchakato wa katiba mpya. Wiki chache baadaye nilifarijika sana nilipoona wise men na women wamejitokeza kwa njia ya ukawa. Huyu bwana anatania.
alionesha seriousness alipowakaribisha ukawa ikulu kupiga juice
 
Mwana Mpotevu,

..naona Raisi akaamua kufumba macho na kuziba masikio.

..hivi tuseme Raisi ameridhika na mwenendo wa wana CCM ndani ya bunge maalum la Katiba?
Ni jambo la kusikitisha. Halafu anajikanganya sana.

Kwa mfano, anasema alikutana na tume mara nyingi lakini mazungumzo hayakuwa ya kina. Hivi unaweza kukutana na akina Warioba, Salim, Augustino Ramadhani kucheza drafti tu au bao kwa jina la tume.

Pili, anasema hata walipomtaka atoe maoni, alisita ili kutoingilia tume na mchakato.
Halafu kuna aya anasema, yeye kama raia ana ruhusu ya kutoa maoni yake.

Tazama Rais alivyokosa uelekeo. Hawezi kuwa Rais akapewa nafasi ya kuzungumza na kukataa. Kisha, Rais huyo huyo aliyepewa nafasi hiyo akaenda kuzungumza katika BMK tena akimtanguliza Warioba.

Hapa maana yake ni kuwa hakutoa maoni, kisha katoa maoni mahali pake.
Mh Rais, BMK si mahali pa kutoa maoni. Ni sehemu ya kujadili rasimu aliyoisani yeye.

Rais anasema alitoa maelezo elekezi na hana tatizo na serikali tatu.
Kwanini Rais anaongopa mchana.

Katika hotuba kuna sehemu kasema ''SERIKALI TATU ZISUBIRI MWAKANI NIKIONDOKA'' Sasa anaposema hana tatizo ana maana gani wakati ameshasema kuna tatizo lisubiri aondoke?

Rais anasema alitoa maoni elekezi kama Rais. Amesahau alitisha nchi kupinduliwa na jeshi. Hivi hayo ni maoni au ni vitisho?

Na mwisho, Rais haoni tatizo la ubaguzi uliokuwa unazungumzwa na CCM.
Hakuona tatizo la LUKUVI kwenda kanisani kuhudbiri katiba.

Inawezekana LUkuvi naye alikuwa anatoa maoni yake.
Lakini basi Rais haoni hata tatizo la kutafsiri sheria?

Kinachoonekana katika hotuba hii ni rais kujivua Uraia na kuongea kama mwenyekiti wa CCM. Amewakana na kuwasuta akina Warioba, amezidi kuwadhalilisha UKAWA n.k.

Ameendelea kusisitiza kuwa akidi inatosha na bunge litaendelea. Well, waandike katiba yao ya CCM. Siku yatakapotokea yale ya Kenya, atakapopata habari za michirizi ya damu ya wanadamu pengine atatambua kosa.

Katiba wanayoandika CCM itakuwa halali kisheria, lakini itakosa uhalali wa kisiasa na kidemokrasia na kuwa kama yai viza.

Asichokiona Rais wetu ni hatari ya usalama na gharama. Hivi CCM wakindika katiba na ikakosa 2/3 Rais haoni atakuwa ameliingiza taifa katika hasara nyingine.

Nadhani suala la kinga kwa makosa kama haya liangaliwe upya.

Kikwete, Katiba ni maridhiano, kama hilo hulitambui endelea kuchochea kuni na mafuta. Mkapa alijaribu hadi leo mzimu inamwandama.

Nawe pia una FFU n.k. unaweza kuwatumia, hata hivyo Moi, Kaunda na wengine sasa hivi ni raia tu. Urais una mwisho, na si mwisho wa maisha.


 
Kifungu hiki kimeniacha hoi!! Hivi kweli hajui kama ushauri wake huu ndio umeharibu Bunge la Katiba na kulivuruga? au anafanya mzaha huyu jamaa?

Ulikuwa hujui kuwa kikwete ni mtu wa mizaha? ndo mana hajui kwanini tz ni maskini
 
maoni yake binafsi hakupaswa kuyatoa kwenye jukwaa rasmi la mkuu wa nchi kuzindua bunge. isitoshe, maoni yake si tayari alishatoa kwenye chama chake?
kwani unadhani hata asingetoa maoni yake ccm wangeuka mkono serikali tatu?.

Ni visingizio tu.
 
Back
Top Bottom