Hotuba ya Rais Kikwete ya Mwisho wa mwezi Julai, 2014

Unajua Siasa ni Mbinu - hawa CCM wameshaka nakubaliana. They are not there to discuss the KATIBA for the interest of TANZANIANS ila to endelea kukaa na kula tuu. They know very well kwamba wasipo weka KATIBA vizuri --- wengi wao wataishia jela tutawafunga kwa dhambi zao. OPEN BIG YOUR EYES. THESE GUYS ARE CLEVER AND THEY KNOW WHAT THEY ARE DOING AND UP TO.
Yani wewe unaandika tuu kama mtu aliyechanganyikiwa! Hebu jadili yaliyomo kwenye hotuba ya Rais!
 
Rais mbona kaongea vizuri tu na kasema kuna mazungumzo ambayo yanasimamamiwa na Samwel Sitta, wanaweza kujadiliana na kuyamaliza au ulitaka rais hawafokee CCM kwenye hotuba yake.
Tatizo lenu mnadhani watanzania wote wanamawazo ya ki CCM ambayo yamejaa uwongo na unafiki! poleni sana. Someni alama za nyakati basi.
 
Katika mambo ntakayokumbuka kwa JK ni kushindwa kuzungumza kama Rais. Mara zote anaegemea upande mmoja.sijui ni ukosefu wa maarifa au udhaifu binafsi.kuhusu katiba alianzisha bila kuwa sera yake so ni vema akubaliane na wenye sera Hiyo.ni afadhali afanye mauaji ya kimbari kuliko kutotimiza hamu ya watanzania aliyoiamsha.

My president bwana hapo kamaliza ati kesho huyo anakwea zake pia USA.
 
Mkuu leo Jk kawapa somo UKawa na hawa wanaponzwa na Lissu maana ana wadanganya na kwa hotuba hakika wata susa kabisa maana Rais kajenga hoja vizuri sana!

Na alicho nifurahisha ni kutukumbusha kuwa UKAWA wamekuwa kama popo maana wakati wanatoka kwenye bunge la Katiba walisema wametoka sababu ya matusi,kejeli na ubaguzi lakini hili la Rasimu ya wananchi kutojadiliwa hawakulisema Lakini walivyotoka Wamebadilika na kuongeza madai!

Ni wazi wananchi wameona jinsi kikundi cha UKAWA kisivyo na tofauti na vikundi vya vurugu na ni vyema serikali kupiga maarufuku hichi kikundi!
kwa ukawa kuongozwa na watu walioshindwa kwenye ngazi ya familia usitegemee kuwa watakuwa na hoja nzuri. Mbatia hana Mke, Lipumba naye hana mke, Mbowe naye anamalizia mambo yake Dubai. Watu wa aina hii ni vigumu kuwa na mwelekeo mzuri. Wanaleta usanii hata kwenye mambo ya msingi
 
Ni jambo la kusikitisha. Halafu anajikanganya sana.

Kwa mfano, anasema alikutana na tume mara nyingi lakini mazungumzo hayakuwa ya kina. Hivi unaweza kukutana na akina Warioba, Salim, Augustino Ramadhani kucheza drafti tu au bao kwa jina la tume.

Pili, anasema hata walipomtaka atoe maoni, alisita ili kutoingilia tume na mchakato.
Halafu kuna aya anasema, yeye kama raia ana ruhusu ya kutoa maoni yake.

Tazama Rais alivyokosa uelekeo. Hawezi kuwa Rais akapewa nafasi ya kuzungumza na kukataa. Kisha, Rais huyo huyo aliyepewa nafasi hiyo akaenda kuzungumza katika BMK tena akimtanguliza Warioba.

Hapa maana yake ni kuwa hakutoa maoni, kisha katoa maoni mahali pake.
Mh Rais, BMK si mahali pa kutoa maoni. Ni sehemu ya kujadili rasimu aliyoisani yeye.

Rais anasema alitoa maelezo elekezi na hana tatizo na serikali tatu.
Kwanini Rais anaongopa mchana.

Katika hotuba kuna sehemu kasema ''SERIKALI TATU ZISUBIRI MWAKANI NIKIONDOKA'' Sasa anaposema hana tatizo ana maana gani wakati ameshasema kuna tatizo lisubiri aondoke?

Rais anasema alitoa maoni elekezi kama Rais. Amesahau alitisha nchi kupinduliwa na jeshi. Hivi hayo ni maoni au ni vitisho?

Na mwisho, Rais haoni tatizo la ubaguzi uliokuwa unazungumzwa na CCM.
Hakuona tatizo la LUKUVI kwenda kanisani kuhudbiri katiba.

Inawezekana LUkuvi naye alikuwa anatoa maoni yake.
Lakini basi Rais haoni hata tatizo la kutafsiri sheria?

Kinachoonekana katika hotuba hii ni rais kujivua Uraia na kuongea kama mwenyekiti wa CCM. Amewakana na kuwasuta akina Warioba, amezidi kuwadhalilisha UKAWA n.k.

Ameendelea kusisitiza kuwa akidi inatosha na bunge litaendelea. Well, waandike katiba yao ya CCM. Siku yatakapotokea yale ya Kenya, atakapopata habari za michirizi ya damu ya wanadamu pengine atatambua kosa.

Katiba wanayoandika CCM itakuwa halali kisheria, lakini itakosa uhalali wa kisiasa na kidemokrasia na kuwa kama yai viza.

Asichokiona Rais wetu ni hatari ya usalama na gharama. Hivi CCM wakindika katiba na ikakosa 2/3 Rais haoni atakuwa ameliingiza taifa katika hasara nyingine.

Nadhani suala la kinga kwa makosa kama haya liangaliwe upya.

Kikwete, Katiba ni maridhiano, kama hilo hulitambui endelea kuchochea kuni na mafuta. Mkapa alijaribu hadi leo mzimu inamwandama.

Nawe pia una FFU n.k. unaweza kuwatumia, hata hivyo Moi, Kaunda na wengine sasa hivi ni raia tu. Urais una mwisho, na si mwisho wa maisha.



Hapo kwenye red. Hilo alilisitiza sana ktk hotuba yake ya ufunguzi wa BMK. Sasa bila hao UKAWA ktk BMK, kuna maridhiano? Anajichanganya jamaa huyu!!!!!
 
lini wewe jk alikufurahisha? Wewe si akina slaa
Sasa hoja iko wapi hapo? Sijaona ulipothibitisha umhimu au sababu za sisi kufurahishwa na huyo rais, sana sana tunaona chuki zako za kitoto dhidi ya Slaa! halafu bado unathubutu kujiita msomi! Kunahitilafu kubwa kwenye mfumo wetu wa Elimu.
 
Halafu tena anajifanya hana habari kwamba huyo Pinda wake alikuwa anahonga, anatoa vitisho kwaWabunge wa CCM na wajumbe wengine kushikilia msimamo wa CCM. Haoni kabisa kama hii katiba itapatikana kwa hongo?
 
Nilichokiona kwenye hii inayoitwa hotuba ni malalamiko tu na sijaona sehemu zimejibiwa hoja na madai ya msingi ya UKAWA, Ikiwa huyo anayeitwa nahodha analalamika na masarahange wanalalamika ni nani atakivuusha chombo salama

Ndiyo walewale wanaopenda kupindisha ukweli. Mbona hotuba umetoa majibu ya kile kilicholalamikiwa na ukawa. Ina maana hata hii hujaisoma
Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Ibara ya 33 (8) inasema: Nanukuu: “Wakati wa mjadala, Mjumbe yoyote anaweza kutoa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko yaliyomo katika Sura za Rasimu ya Katiba zinazojadiliwa kwa utaratibu ufuatao: (a) Ikiwa ni marekebisho, maboresho au mabadiliko yanayobadilisha jambo la msingi, au yanayobadilisha maudhui ya Ibara, mapendekezo ya marekebisho yatapelekwa kwa maandishi kwa Katibu siku moja kabla ya mjadala wa Ibara husika. (b) Ikiwa ni marekebisho madogo, ambayo hayabadili msingi au maana, mapendekezo ya marekebisho yatawasilishwa na mjumbe wakati wa mjadala baada ya kupata ruhusa ya Mwenyekiti”.
Kanuni hii ilipotungwa, Wajumbe wote wa Bunge Maalumu pamoja na wale ambao baadae walisusia vikao vya Bunge walikuwepo Bungeni na walishiriki kuipitisha. Tena basi, baadhi yao walikuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni iliyopendekeza Kanuni hizo. Unapowaona watu wale wale sasa wanakuwa vinara wa kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba, unajiuliza maswali mengi kuhusu watu hao bila ya kupata majibu yaliyo sahihi na kutosheleza akili na ufahamu wetu.

Ndugu Wananchi,
Unaposoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge Maalumu, hii ni dhahiri kwamba wote walikuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mamlaka ya Bunge Maalumu ya kujadili Rasimu iliyoandaliwa na Tume na kutunga Katiba inayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.

UKAWA waje hapa jamvini na watuambie hii kanuni wakati inapitishwa wao walikuwa wapi? au hawakushiriki kuipitisha? Tundu Lisu (Mwanansheria) siku hiyo alikuwa baa kama kawaida yake ndo maana kipengele hiki kilipita? Hawana points za msingi mbali ya umbumbumbu na uvivu wa kufikiri unaowasumbua. Watanzania siyo wa kupelekwa kwa ajili ya maslahi ya watu wachache.UKAWA badilikeni kifikra.
 
Wewe unafanya nini? Unatoa maoni, unalalamika, unagomba? Mmemsema sana president, hotuba yake iko sawa ksbisa, subirini atoke madarakani muigawe nchi vipande vipande kama huyo rais ajae atakuwa juha kama mnavyofikiria
Hivi thatha unajua unachokisema kweli? Kwamba maoni ya wanachi si lolote si chochote; kwamba wananchi wakitaka wasubiri atoke madarakani ndipo maoni yao yaweze kuthaminiwa! What is wrong with you people? Katika nchi zenye mwamko tamko kama hilo lingemsababishia matatizo makubwa ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwa uhaini.


 
Last edited by a moderator:
Na kwa nini alingojea Warioba awasilishe RASIMU YA PILI (ya serikali tatu tena) ndiyo akachaguwa wale 201 kwa kuwachomeka wengi wa chama chake! halafu anataka eti 'uwingi' uheshimiwe! 'Uwingi' wa kupikwa kimakusudi?
 
Kwanini haamini kuwa hutoba yake kwenye BMK (aliyoita maoni yake) iliinfluence mwenendo was majadiliano wakati mwanzo alipotakiwa na tume atoe maoni aliamini hivyo?

Kweli. leo nimemini Tanzania inaweza kuongozwa na yeyote
 
Jamani Mungu atudhibu kwa uongo yetu; mbona kiini macho ? Mapolisi eti wameshika mke na mume wanaohusika na hurubuaji mabomb ??? Wanafikiria kuwa wa Tanzania wa sasa ni wajinga sana kuwarubuni na uongo. Mbona tunajua hizo mbinu zao CCM na Mapolisi
 
Kubwa alilozungumzia ni Bunge la Katiba linaloanza tena wiki ijayo.

Ni ndefu sana naangalia namna ya kuwaletea kwa muhtasari au kuleta yote kama ilivyo

HINTS ZA HOTUBA
- Bunge la katiba linajadili RASIMU YA TUME na sio vinginevyo. Wanaosema Bunge halijadili rasimu ya Tume ya Warioba ni Wazushi.

- Sheria inaeleza kuwa Tume inapaswa kuandaa RASIMU ya KATIBA na Bunge la katiba linapaswa kuandika KATIBA INAYOPENDEKEZWA. Kwahiyo Bunge linafanya kazi yake kikamilifu.

- Huwezi kutunga Katiba inayopendekezwa bila kufanya Mabadiliko. Bunge la Katiba lazima lifanye mabadiliko na linaruhusiwa kisheria ili kutekeleza jukumu lake la kutunga katiba inayopendekezwa.

- UKAWA hawana sababu ya msingi ya kutoka au kususia Bunge

- Bunge litaendelea na theluthi mbili ndio itaamua hatma ya Katiba inayopendekezwa na kisha wananchi wataamua kupitia kura ya maoni


sikumsikia kusema kwamba alisema zikipitishwa serikali tatu jeshi litapindua nchi
 
Halafu tena anajifanya hana habari kwamba huyo Pinda wake alikuwa anahonga, anatoa vitisho kwaWabunge wa CCM na wajumbe wengine kushikilia msimamo wa CCM. Haoni kabisa kama hii katiba itapatikana kwa hongo?

Anaamini watu wake wameshawahonga wale wajumbe wa Zanzibar (wasakatonge) na kwamba quorum ya 2/3 itapatikana tu. Anacheza kamari kubwa na amani ya nchi huyu mjamaa. Ana uhakika gani ng'ombe baada ya kumpeleka ziwani atayanywa maji?

Huyu jamaa kila siku zake za urais zinapokaribia, ndipo anazidi kuwa kama dikteta vile! God bless Tanzania!
 
Back
Top Bottom