Hotuba ya Magufuli na Sekta ya Elimu

Sudysoko

JF-Expert Member
Aug 19, 2015
449
180
Hotuba ya Magufuli

Katika Sekta ya ELIMU:

"Tutatekeleza Sera ya Mfumo mpya wa Elimu unaotaka Elimu ya msingi iishie kidato cha Nne na iwe BURE. Itahakikisha Tatizo la Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya juu linashughulikiwa kikamilifu na kuondoa usumbufu ambao ambao Wanafunzi wamekuwa wakiupata ikiwa ni pamoja na kupata fedha kwa wakati ili muda wao wautumie kwa kusoma na sio migomo.

Aidha kwa kushirikiana na mifuko ya pensheni na Sekta Binafsi tutajenga hosteli za kutosha ili kuwaondoa wanafunzi adha ya malazi.Kuhusu masilahi ya Walimu, napenda mfahamu kuwa mimi pia ni mwalimu,hakuna mgombea anayezijua adha zenu kama mimi. Matatizo mliyonayo hata mimi nilipata, nayajua.

SITAWAANGUSHA; Mnatufundishia Wataalamu katika Sekta mbalimbali,nitawapa kipaumbele. Lazima tuboreshe masilahi yenu, tutatekeleza kikamiifu Muundo mpya wa Walimu na kuimarisha Tume ya Utumishi wa Walimu.

Mazingira ya kazi yataboreshwa.Ujenzi wa nyumba za walimu utatoa kipaumbele katika shule za vijijini." JP Magufuli.

Mchague MAGUFULI kwa maendeleo ya Tanzania.

#HapaKaziTu
 
Mimi nitampa kura Magufulh kwa imani niliyo nayo juu yake. Utendaji wake uliotukuka ktk kila wizara aliyopewa.

Nachagua MTU , sichagui CHAMA, CCM IMEOZA.
Kwa imani niliyonayo juu yaka JPM ninahakika ana uwezo mkubwa kupunguza uozo ndani ya CCM.

Lowassa hafai kupewa nchi hii kwa vyovyote vile.
 
'Mimi ni Mwalim nayajua matatizo ya walim' hata afsa elim wangu ni mwalim na anatambua matatizo yangu......
 
'Hakuna Mtoto wa Masikini atakayekosa elim eti kwa sababu hana mkopo' haya maneno kuna mtu aliyaongea miaka kadhaa nyuma,vijana kibao wanalialia na mikopo
 
Hivi wanasiasa wanatuchukuliaje ss walimu! Au wanatuona ss tuna ubongo wa kuku? (Yaan wasahaulifu), maana nashangaa tangia miaka ya 1995 campeni za vyama vingi ilipoanza , ccm walikuwa wanabeba hiyo ajenda ya walimu hadi Leo na hawajafanikiwa, je hawaoni kama wanatudhalilisha ss walimu huko majukwaani? Bora watupotezee tu coz na ss tumeshawapotezea
 
Anajua matatizo yapi ya walimu aliyoyaishi huyu mwizi? Ualimu alifanya mwaka mmoja tu, hivyo asitake kutidanganya hapa! Hivi hii ajenda ya walimu ni lini ilikosekana kwenye ilani za ccm? Ni lipi walilokifanya tangia hapo? Hebu watupishe huko!!
 
Mimi nitampa kura Magufulh kwa imani niliyo nayo juu yake. Utendaji wake uliotukuka ktk kila wizara aliyopewa.

Nachagua MTU , sichagui CHAMA, CCM IMEOZA.
Kwa imani niliyonayo juu yaka JPM ninahakika ana uwezo mkubwa kupunguza uozo ndani ya CCM.

Lowassa hafai kupewa nchi hii kwa vyovyote vile.
Nakuunga mkono 1000% mtu wangu usemalo hata mm latoka rohoni kwa CHAGUO hilo la mungu na LUKUVI Mungu amjalie MAGUFULI awe Wazir wake mkuu. CCM CHAKAVU CDM CHAMA LKN RAIS MAGUFULI NA LOWASA FISI NO MORE
 
Anajua matatizo yapi ya walimu aliyoyaishi huyu mwizi? Ualimu alifanya mwaka mmoja tu, hivyo asitake kutidanganya hapa! Hivi hii ajenda ya walimu ni lini ilikosekana kwenye ilani za ccm? Ni lipi walilokifanya tangia hapo? Hebu watupishe huko!!

Tatizo la Magufuli anatumia nguvu nyingi na akili kidogo.Ni mikakati gani alio nayo in hand bila kuonyesha ankara ya fedha,hiyo fedha ya kuwalipa kwanza viporo vyao vya siku nyingi,kuwalipa mishahara stahiki,kuboresha marupurupu yao nyumba n.k atazichota wapi?
Anasema Elimu itakuwa bure,hakuna cha bure,hizo ngonjera za TANU kusaka uhuru tuliambiwa tutawekewa rami mpaka chooni.be serious magufuli usitoe ahadi za Rocket science.
 
Hivi mbona atuambii kwa mini hazina wamesema hakuna mwalimu anayeidai serikali huku kiuhalisia walimu wengi bado wanadai mapunjo ya mishahara yao.
 
Mifuko hii ipo hoi baada ya kufirisiwa na serikali ya CCM kwa kukopa bila kulipa. Sasa anataka kuizika kabisaaaaaa
 
baada ya uchaguzi kukamilika na hatimaye kumchagua dr magufuli kuwa rais mteule. sasa nawapa fursa walimu popote pale walipo waanze kupendekeza rangi ya laptop wazipendazo. kumbuka hiyo ni ahadi ya rais mteule kuwa kila mwalimu atanunuliwa laptop mpyaaa.
 
Mimi nataka Mac
 
Amerithi madeni kibao ya walimu aanzie hapo .Hicho ndicho kipimo changu cha kwanzo cha uwezo wake kiutendaji.-malimbikizo ya mishahara,fedha za uhamisho,likizo,masomo,nk.Nyingi hazilipwi kutokana na ubabe wa waliopewa majukumu ya kusimamia maeneo hayo kutokujali na pia kupuuza walimu.je magufuri atawaweza?
 
Hotuba ya Magufuli

Mchague MAGUFULI kwa maendeleo ya Tanzania.

[HASHTAG]#HapaKaziTu[/HASHTAG]
ahahaha
Mimi nitampa kura Magufulh kwa imani niliyo nayo juu yake. Utendaji wake uliotukuka ktk kila wizara aliyopewa.

Nachagua MTU , sichagui CHAMA, CCM IMEOZA.
Kwa imani niliyonayo juu yaka JPM ninahakika ana uwezo mkubwa kupunguza uozo ndani ya CCM.

Lowassa hafai kupewa nchi hii kwa vyovyote vile.
Eti?ahahaha
'Mimi ni Mwalim nayajua matatizo ya walim' hata afsa elim wangu ni mwalim na anatambua matatizo yangu......
kumbe?ahahaha
'Hakuna Mtoto wa Masikini atakayekosa elim eti kwa sababu hana mkopo' haya maneno kuna mtu aliyaongea miaka kadhaa nyuma,vijana kibao wanalialia na mikopo
apia kwa jina la Mungu!
 
Back
Top Bottom