#COVID19 Hospitali ya Bugando yakumbwa na upungufu wa mitungi ya Oksijeni kwa Wagonjwa wa Kupumua

hospitali marehemu mama yangu alilazwa walikuwa wanatumia VENTILATOR za umeme!sio cylinder!...
Mkuu ukiona mtu anafanya joke na UVIKO-19 ujue haujampitia au haujapitia familia yake. Ebu aende ICU akaone wagonjwa wenye UVIKO-19 wanapumuaje, alafu aje hapa aseme ni mafua tu. Hii kitu isikie tu mkuu kwa mbali. Usiombe ikutokee au itokee wazizi wako alafu uambiwe yuko kwenye ventilator.
 
Habari wadau.

Hali naona imeanza kuwa mbaya kwa upande wetu Tanzania ,nasikia huko Bugando washaanza kukumbwa na upungufu wa mitungi ya oxygen...
Subiri kwanza tujenge sanamu la malaika mkuu,

JamiiForums-620675953.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe hiyo hela ni ndogo sana kwa serikali. Ni hela ya chai na mikate kwa siku moja tu.

Acha kuiaibisha serikali na kuitukana.

Afu unaonekana una mawazo ya kimasikini masikini sana wewe!

Sio kila kitu ni madawati tu. Hata kumuenzi na kumuheshimisha Rais Magufuli ni jambo pia, tena la muhimu.

Kwanza hako kahela kadogo mnoooo ukilinganisha na mambo ambayo Magufuli amelitendea Taifa hili.

Nyinyi majizi mnaogopa hata sanamu ya aliyekufa?

Mwanzoni nilikuwa nafahamu kwamba nyinyi majizi na wauza unga mnamuogopa Magufuli kutokana na namna alivyowaadabisha, kumbe hata sanamu yake mnaiogopa pia?
Wewe jamaa ni mjinga sana. Kabla hujaandika jaribu kufikiria kidogo na sio kuandika kwa ushabiki tu. Serikali ina hela imetoa wapi? Hiyo ni hela yetu wananchi na ni lazima ituhudumie kwanza kabla ya kwenda kujenga masanamu yasiyo na maana yoyote. Wananchi wanakufa kwa kukosa oxygen na wana hela zao wamekabidhi watu kuzitunza na kutumia kwa ajili yao lakini wao wanakwenda kujenga sanamu. Sanamu yenyewe ya mtu aliyeacha historia mbaya katika jamii. Ujenzi wa sanamu ni matumizi mabaya ya hela ya wananchi. Amka!!!!!
 
Kitaeleweka TU,
Kikubwa imani yako, ukiwa na hofu utakufaa mapema.

Shughuri ziendelee,
Kama tulisavaivu kipindi inaanza, na tutasavaivu pia hata kipindi hiki.

Tusitiane Hofu,
Nna imani Mungu atatutia Nguvu.

Inshallah
Kweli kabisa... Tusitishane
 
Tunajenga kwanza sanamu ya aliegundua vitunguu swaumu na malimau kama dawa ya Corona,mitungi ni mambo ya baadae sana.
 
Ni upumbavu mtupu
Ichi ndicho niliwai kusema kwenye post yangu ya nyuma apo watu waka anza kunitukane eti Mimi mjinga
But my bro’s this true wanatumia vyombo vya abari kupeleka hofu kwa watu
Sijuwi Italy wame kufa watu 3000 kwa siku uongo mtupu akuna kweli

Ivi ninyi na akili yenu kabisa you hamuwezi fanya uchunguzi juu ya ugonjwa huu?

Maana some day nilifanya and majibu yangu yalikuwa positive niliambiwa kaa karantine siku 14 cha ajabu nilikaa kilicho ni shangaza kwa izo siku 14 sikutumia Dawa wala nini siku niliyo rudi hospital nika ambiwa nime pona COVID-19

Na so mimi tu marafiki zangu wengi wamesha wai pimwa iyi covid wana ambiwa wana covid wanakaa ndani siku 14 bila kutumia Dawa yeyote alafu wakirudi wana ambiwa wana pona
Mmmmm fanyeni uchunguzi huu sio ugonjwa


Jaribu kufikiria tu

Kipindi madascar walitengeneza Dawa
Uko afrika walizibitisha kabisa ina ponya
Kwanini who walikataa Dawa ile ? Na wakati hawakufanya uchunguzi wowote ?


Kuna Docter wa ufaransa alisema eti kuna vidonge vinaponya covid walikataa

Leo wame tuletea chanjo zao tuna lazimishwa kuchanja

Dah jamani watu fanyeni uchunguzi sio kuwekana hofu bure tu

Kuna vitu wanavyo taka awa wapumbavu kama sio pesa ndo wanazo zitafuta basi ita kuwa vitu vingine
Na madhara ya vitu ivyo itaonekana in the future
Hata mashehe gerezani waliugua na kupona kwa kutumia azuma. Dawa inayotibu kisonono.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Habari wadau.

Hali naona imeanza kuwa mbaya kwa upande wetu Tanzania ,nasikia huko Bugando washaanza kukumbwa na upungufu wa mitungi ya oxygen.

Kipindi hiki lockdown haikwepweki bila shaka. Mpaka sasa Bugando Hospital wanaupungufu wa mitungi 500 ya oxygen.

Huku mtaani kwetu Buza sioni kabisa taadhali zikifuatwa ,Mungu atunusuru kwa kweli.

Chanzo: ITV Habari 06/07/2021.
View attachment 1844061
Hivi serikali inasubilia nini ku impose strict measures ikiwemo lazima ya barakoa,marufuku ya mikusanyiko isiyo ya lazima na kwenye mastendi kuzuia milundikano,lazima ya maji tiririka kama kipindi kile unaingia?

Kutumia tuu soft language ya kwamba watu wachukue tahadhari haisaidii na hata shule kwa sasa zipigwe ban kabla Hali ya India haijatufika..

Ikiwezekana lockdown ifanyike kwenye mkoa huo
 
Nilimsikia Rais akisema kuna pesa zaidi ya US dollar 400ml. kwaajili ya Corona, hizo pesa zielekezwe huko kununua mitungi ya oxygen kwa hospitali za serikali.

Lakini pia, tahadhari dhidi ya Corona ni vyema ziendelee kuchukuliwa kwa kila mmoja wetu kukumbushwa ana jukumu la kumlinda mwingine kwa kuanzia na kujilinda yeye binafsi.
Kukumbushana bila bakola watu hawaelewi
 
We mtu wa ajabu hiyo ripoti inasema kuchukua tahadhari na kujiandaa kuwa na mitungi ya oxygen.
Ulichoandika ni kana kwamba wagonjwa ni wengi mpaka oxygen imekosekana.Watu Kama wewe ni hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom