Hospitali ya Benjamin Mkapa kuanza rasmi upasuaji wa kupunguza unene

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1576303237992.png

BAADA ya kupata mafanikio ya majaribio ya kupunguza unene, Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imetangaza rasmi kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa kupunguza uzito kwa watu wenye unene uliopitiliza. Pia mwanzoni mwa mwezi ujao, wagonjwa sita watafanyiwa upasuaji wa kupandikiza figo kwenye hospitali hiyo.

Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Kessy Shija alipokuwa akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa na hospitali hiyo katika kipindi cha miaka minne ndani ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli wakati wa ziara ya timu ya maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake.

Akizungumzia mafanikio hayo, Dk Shija alisema hospitali imefanikiwa kuwa na vifaa tiba vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu ikiwamo CT-Scan, MRI, na maabara maalumu ya kisasa ya uchunguzi na matibabu ya moyo ambayo ilianza Februari mwaka 2019. “Tangu huduma hii ya maabara ianze Februari 2019, na hadi Juni mwaka huu tayari wagonjwa 41 walihudumiwa.” Alisema huduma za kibingwa zinazotolewa hospitalini zimesaidia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi ambapo hadi Juni 2019, wagonjwa saba walipandikizwa figo.

Dk Shija alisema kati ya Januari 6-7 mwakani, hospitali hiyo inatarajia kupandikiza figo wagonjwa sita na taratibu zote za upandikizaji figo kwa wagonjwa hao zimekamilika. Aidha, Dk Shija alisema hospitali hiyo ilianzisha huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa ambao figo hazifanyi kazi na mpaka sasa wamehudumia mara 2,974 kwa wagonjwa 86. Kwa upande wa matibabu ya saratani, Dk Shija alisema hospitali imefanikiwa kuanzisha huduma ya matibabu hayo.
 
Back
Top Bottom