Watu wengi wana dhana potofu kuwa wafanyabiashara ni vilaza, wahuni, watu wasiojitambua, hawajui sheria wala kujieleza. Kinyume na dhana hii potofu wafanyabiashara mmeonesha weledi mkubwa (professionalism) kwa jinsi mlivyowasilisha na kudai ufumbuzi wa kero zenu mbele ya serikali.
Mmekuwa wazi na kueleza kero zenu mbele ya waziri mkuu bila woga wowote na bila kumumunya maneno na kuonesha kuwa nyie ni kada muhimu sana na yenye nguvu katika jamii yetu.
Nimevutiwa sana kwa jinsi mlivyoonesha kutoridhishwa kwenu na utendaji mbovu wa waziri wa fedha Mwigulu Nchemba na waziri wa viwanda na biashara Ashatu Kijazi na hamkusita kuwasema mbele ya waziri mkuu bila kupepesa macho!
Mmeonesha ushirikiano mkubwa na jinsi ya kudai haki na mazingira mazuri makazini. Watanzania hususani wafanyakazi katika sekta mbalimbali tunapaswa kuiga weledi na ujasiri huu kudai maslahi yetu.
Watanzania tutambue kuwa kero zetu hazitashughulikiwa bila kuunganisha nguvu zetu na kudai mabadiliko kama walivyofanya wafanyabiashara.
Hongereni wafanyabiashara kwa kuonesha njia!