Shamrashamra za kumpokea aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Urughu, ndugu Simon Tyosela, katika viwanja Ulemo jimbo la Iramba Magharibi. Kiongozi huyo aliambatana na wanachama wengine wa Chadema ambao walipokelewa na Katibu wa NEC uchumi na fedha ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi Mhe. Mwigulu Nchemba.