Hongera kwa Cameraman wa TBC1, JWTZ ila pole sana kwa huyu Mlinzi Mlalavi wa Rais JPM kutoka PSU

Huyu Jamaa nina muda mrefu sana sijamuona hapa JF na nakumbuka Mada kama hizi huwa anajitahidi mno Kuzichangia na hata hii naamini sasa hivi angekuwa anaichangia mno. Asante Kiongozi kwa Kumtaja hapa kwani nilikuwa nimeshamsahau.
He he he Genta bana
 
😅😅😅 Fungua thread zake,mpangilio,muandiko,mtiririko na maneno meengiii uliyotumia kwenye uzi huu ndvyo alivyo Man GENTER isitoshe anapenda sana mambo ya kiintelijensia,kifupi mnafanana muandiko hadi sauti ingawa najua ndio wewe.😁

Hapo katika Kufanana nae hadi Sauti nahitaji Ufafanuzi wako kidogo Kiongozi kwani kumbe hapa tunavyokuwa tunaandika hivi pia huwa tunaongea na kusikilizana kwa Sauti au? Nasubiria jibu lako Kiongozi.
 
Hata Mimi Kiongozi nasubiri akirudi aseme alikumbwa na nini na kwanini amepotea hivi hapa Jukwaani isivyo kawaida. Ni Mmoja wa Members ambao nilianza Kuwakubali hata kabla sijajiunga rasmi hapa.
unazuga tu si ndiyo?

nimependa ulivyokuja kivingina, vilevi'fonts vinavyoumiza macho umeviacha huko...

pia yale matusi na kejeri umeacha huko. pongezi kwa mods tafadhali!
 
umeandika pointi ila umaandika kama nsha.Maneno mengi point chache.umerudiarudia points kiasi sasa unaelekea kuwa mkuda

Madhali Kiini cha Hoja yangu Kuu umeshakielewa basi sioni tatizo lolote lile sana sana tu nikushukuru kwa Kuufungua huu Uzi na hadi Kuchukua muda wako Kuusoma wote na Kuuchangia kama hivi.
 
Kwa mara ya Kwanza kabisa nitoe pongezi zangu za dhati kabisa kwa Cameraman wa TBC1 hasa aliyekuwepo zamu leo huko Chato Geita kwa Kitendo chake cha Kuonyesha Uweledi wake na kutofanya Kazi yake Kinafiki ambapo kila mara alikuwa akiuonyesha Udhaifu wa Mmoja wa Walinzi wa Rais JPM ambaye ni Mlalavi ( Mpenda Kusinzia / Mpono ) sana awapo eneo la Tukio.

Pili nizidi Kutoa pongezi zangu kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) hasa kwa Kuzalisha Wapiganaji ( Wanajeshi ) ambao kiukweli wamekuwa wameiva hasa na kweli Kimedani ambapo mfano wake amekuwa ni huyu Mpambe wa Rais ( ADC ) ambaye Kiukweli tokea awe hapo baada ya Kuchukua nafasi ya aliyekuwepo sijawahi Kuona akifanya Makosa ya Kiulinzi na Kiusalama kama ambavyo amekuwa akiyafanya Mmoja wa Walinzi wa Rais JPM anayetokea PSU.

Tatu na mwisho kabisa nitoe pole zangu kubwa kwa Kikosi cha Ulinzi wa Rais PSU chini ya Idara ya Usalama wa Taifa nchini ( TISS ) hasa kwa kuzidi Kuendelea Kulilea tatizo la Kimsingi kabisa na la Kiusalama la huyu Mmoja wa Walinzi wa Rais JPM ambaye ni Mlalavi ( Mpenda Kusinzia hovyo ) awapo Kazini hali ambayo Kiusalama sidhani kama ina Afya bali ni mwendelezo wa Udhaifu.

Kama kawaida huyu Mlinzi Mlalavi wa Rais JPM na leo tena amerudia Udhaifu wake ule ule wa Kulala na tokea nianze Kumuona akipenda Kusinzia nadhani hii ya leo kule Chato Geita atakuwa amevunja Rekodi kwani alikuwa akisinzia kwa Intervals japo namsifu kwa kuwa Mjanja kwani kila akisinzia tu na akishtuka utamuona anajifanya yupo attentive kisha anazuga kidogo kwa Kumuangalia Bosi wake kisha anaendelea tu na Ulalavi ( Upono ) wake.

Uzi huu wala hauna nia ya Kumuharibia hicho Kibarua chake na natambua fika kuwa Kiutendaji yupo vizuri tena sana tu na ndiyo maana PSU wakaamua kumpa hilo Jukumu zito la kuwa Mmoja wa Walinzi wa karibu sana wa Rais JPM ila nadhani huyu Mlinzi atakuwa na matatizo ambayo labda Mimi, Wewe na Yule hatujui hivyo basi Wahusika waliangalie hili kwa haraka na walitatue kwani kwa Kitendo chake cha kila mara Kuonekana akisinzia hovyo tena mbele ya Camera huku Watanzania wote wakiwa wamempa dhamana ya Kiulinzi ya Rais wao kiukweli inatia mno shaka.

Najua kuna wale wenye Viherehere, Visebusebu na Viroho Papa watakuja mbio hapa na kudhani kuwa labda nimekurupuka tu au nimebuni haya Madai hivyo basi kabla hamjapoteza muda wenu rejeeni Footage ya TBC1 leo huko Chato Geita hasa kuanzia pale Yule Kijana wa Kisukuma alipokuwa akitumbuiza ambapo ilikuwa ni Saa 6 na dakika 5 ambapo huyu Mlinzi alianza Kulala Saa 6 na dakika 13 akaja Kushtuka na Kuzuga Saa 6 na dakika 17 kisha akaendelea tena na huo Utaratibu wake ambapo Saa 6 na dakika 19 hadi na dakika 21 wakati Wanakwaya wa Kwaya ya AIC Mganza wakiimba kwa Hisia alisinzia tena na nadhani kuna Wakubwa zake walimshtua kwani kuna muda alionekana ameshtuka hivi na kama anapokea Maelekezo fulani kupitia Mawasiliano yao ya Siri na tangia hapo Umakini wake ukarejea.

Kinachonishangaza zaidi ni kwamba huyu Mlinzi Mlalavi ( Mpono ) wa Rais JPM hakuanza utaratibu wake huu wa Kupenda Kusinzia leo, jana wala juzi bali ndiyo umekuwa utaratibu wake lakini nashangaa Wahusika ( Wenye Mamlaka ) wala hawashtushwi nalo. Hii siyo Sifa kwa Kikosi cha Ulinzi wa Rais na utaratibu huu wa huyu Mlinzi ni kama vile anadhakidhalilisha hicho Kikosi cha PSU ambacho hajiwahi kuwa na Sifa hii mbaya tokea Awamu zote kuanzia ile ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, Mzee Kikwete ila haya Maajabu tumeanza kuyaona Awamu hii.

Kama kwa huu Uzi wangu An Eagle nitabatizwa kwa Kuitwa Mchochezi au Msaliti au Wakala wa Mabeberu au siyo Mzalendo sitojali na pengine nitawashukuru pia ila nadhani huu Uzi wangu unaweza ukawa na Msaada na Suluhisho kwa hili tatizo kwani naamini kuwa Kiusalama hiki si Kitendo kizuri na pengine kama wakitokea Watu wenye nia mbaya na Rais wetu basi wanaweza Kuutumia huo Udhaifu wa huyo Mlinzi wa hatimaye wakafanya yao na Historia mpya Kutengenezwa Tanzania kitu ambacho sipendi kije kutokea na wala sikiombei kitokee.

PSU liangalieni hili Kiumakini na mlifanyie Kazi kwani linachafua sana Taswira yenu kama Kikosi chenye Dhamana kubwa ya Ulinzi wa Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Magufuli. Sitaki kuwapangieni nini cha Kufanya kwani hata uwezo huo sina na ukizingatia Mimi ni Mtu wa kawaida tena mno ila najiuliza na mpaka sasa nashangaa yupo wapi kule Mlinzi mwenye Kutoka Zanzibar ambaye nasikia hivi sasa ni RSO sijui DSO huko Mkoani Kilimanjaro. Ukimuangalia Kimedani Umakini wa Kiutendaji wa Yule Jamaa ( huyo Mzanzibari ) ana uwezo mkubwa sana kuliko huyu Mlalavi ( Mpono ) na huwa anakuwa hana Sifa wala Mashauzi bali muda wote alikuwa akijua Majukumu yake na Itifaki ilikuwa imempendeza na aliifanya vyema kabisa Kazi yake.

Yangu ni hayo tu.
Mpono = pono
Mlalavi = ni yule anae lala vibaya kitandani.

Umetumia muda mrefu na maneno mengi sana (mengi yanjirudia rudia) kuelezea kitu ambacho ungekielezea kwa ufasaha kwa kutumia mistari isiyozidi mitano.

Jifunz kuwa "conservative" kwenye kuandika kwako na usipende kutumia maneno/misamiati usiyoifahamu.
 
Unategeka!?unadhani amesinzia. Kajaribu uone show yake.
 
Hapo katika Kufanana nae hadi Sauti nahitaji Ufafanuzi wako kidogo Kiongozi kwani kumbe hapa tunavyokuwa tunaandika hivi pia huwa tunaongea na kusikilizana kwa Sauti au? Nasubiria jibu lako Kiongozi.
Ukisoma una assume na sauti ya mtoa mada😁😁😁,yan kama unasoma habar iliyoandikwa na george maratu lazma usome kwa sauti yake
 
unazuga tu si ndiyo?

nimependa ulivyokuja kivingina, vilevi'fonts vinavyoumiza macho umeviacha huko...

pia yale matusi na kejeri umeacha huko. pongezi kwa mods tafadhali!

Samahani Kiongozi huu Ujumbe wako umeuwasilisha Kwangu Kimakosa au labda umeamua tu Kumsema huyo sijui Gentamissini Wenu kupitia huu Uzi wangu? Samahani hivi hapo Jina lake nimeliandika sawasawa au labda nimelikosea Kiongozi?
 
Japo sijamuona ila naamini ni yule cheusi kauzu aliyetoka nae toka enzi za kampeni ambaye siku hizi kanenepa hivi,mana nishamuona Mara nyingi akisinzia
 
Siyo Siri kwa jinsi mnavyomtaja taja huyu Jamaa mmenilazimisha nami sasa nianze Kumfuatilia ili nione alikuwa akipendelea Kuandika nini hapa kwani inaonyesha alikuwa na Mvuto wake wa Kipekee kabisa na ndiyo maana naona Watu wanaacha Kujadili lililopo mezani ( Jukwaani ) ambalo linahitaji Mjadala mpana na mrefu na wao wamekalia Kumjadili Yeye tu huyo Gentamycine. Ni lazima tu atakuwa na Nyota Kali mno hadi anazungumzwa na kufuatiliwa na Members hapa. Na sijui amepotelea wapi!
ha ha ha dah
 
Huyu Jamaa nina muda mrefu sana sijamuona hapa JF na nakumbuka Mada kama hizi huwa anajitahidi mno Kuzichangia na hata hii naamini sasa hivi angekuwa anaichangia mno. Asante Kiongozi kwa Kumtaja hapa kwani nilikuwa nimeshamsahau.
Huwa wanasema ni wewe ila umefungua akaunti nyingine
 
Mpono = pono
Mlalavi = ni yule anae lala vibaya kitandani.

Umetumia muda mrefu na maneno mengi sana (mengi yanjirudia rudia) kuelezea kitu ambacho ungekielezea kwa ufasaha kwa kutumia mistari isiyozidi mitano.

Jifunz kuwa "conservative" kwenye kuandika kwako na usipende kutumia maneno/misamiati usiyoifahamu.

Afrika Kusini na Ujerumani wanatafuta sana Walimu ( Wakufunzi ) wa Lugha ya Kiswahili je umeshapeleka tayari Maombi yako au Wewe Kiswahili chako ni cha kuja tu hapa Jukwaani na Kukosoa Wenzako kana kwamba unakijua mno wakati yawezekana na Wewe ukawa ni Mngendembwe ( Mshamba ) tu vile vile?
 
Samahani Kiongozi huu Ujumbe wako umeuwasilisha Kwangu Kimakosa au labda umeamua tu Kumsema huyo sijui Gentamissini Wenu kupitia huu Uzi wangu? Samahani hivi hapo Jina lake nimeliandika sawasawa au labda nimelikosea Kiongozi?
najua una lifeban kule na niwapongeze mods kwa kazi nzuri waliyofanya!

mimi ulinisabashi ban ya wiki, wewe umeliwa maisha safi sana!
 
Huwa napenda sana na hadi Kushukuru nikiona Watu ( Members ) Makini na very Intelligent kama Wewe wanajitokeza Kuchangia Mada zangu ambazo kuna muda mwingine huwa zinahitaji Akili kubwa na pana Kuzielewa lakini ukiwa Duduna ( Pumbavu ) kamwe hutozielewa na kunielewa pia.

Narudia tena Kusisitiza kama Watu wa PSU chini ya TISS wataendelea Kunyamaza juu ya Mapungufu ya huyu Mlinzi wa Rais JPM Mlalavi ( Mpono ) huku wakiziba Masikio yao kwa Kuweka Pamba kwa jinsi ambavyo kila mara tumekuwa tukiwatahadharisha hapa basi nami sasa nitaanza Kuamini kuwa kuna shida Kubwa Kuanzia hapo PSU Kwenyewe hadi TISS kwa Ujumla ya Utendaji wa Watendaji wake.
Ndugu yangu, kuna mambo ya kuletea mzaha lakini sio issues za kiusalama hasa kwa kiongozi muhimu. Hatujakua leo tunayafahamu sana haya, bora wewe umekua wa pili kulisemea hili baada ya Gentamycin. Wapo wanasoma humu na watafanyia kazi, sisi kazi yetu kusaidia kutoa taarifa. Ni jambo jema na la kizalendo umesikaka
 
Back
Top Bottom