Hongela Chadema kwa kunielewa Kuh:Kutoziamini mahakama

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Hii imenipa moyo kwamba sasa Chadema imeanza kuelewa siasa ,kwani siasa sio vita ni mbinu na mikakati iliyokomaa kimipango,hili la kutoelekea mahakamani ni mwanzo wa kuonyesha kutokuwa na imani na mahakama zetu hapa Tanzania.

"...........Mala ambaye ni Diwani wa Kimandolu, alisema baada ya kukaa na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, wameona hakuna sababu ya kufanya hivyo kwani wanachojua wao ni kwamba nafasi ya Meya wa Jiji hilo bado iko wazi kwani kikao kilichomchagua Meya ni batili.Alisema hawataenda mahakamani kwani wamebaini kuwa wakifanya hivyo watakuwa wamejimaliza.
“Uzoefu unaonyesha kuwa kukimbilia mahakamani sio tija kwani kesi inaweza kupigwa danadana hata zaidi ya miaka mitano. Sisi bado tuna hatua nyingi tunazoweza kuzichukua kudai haki yetu, hatuna wasiwasi kwani tunaamini kuwa tunatetea haki ya wananchi walio wengi,” alisema Mala.
Kuhusu msimamo wao wa kumtambua ama kutomtambua Meya aliyechaguliwa, alisema sio tu kuwa hawamtambu Meya huyo, Gaudence Lymo, bali hawautambui hata mkutano wa Baraza la Madiwani uliomchagua kwani ulikuwa wa upande wa chama kimoja cha CCM..."
 
bali hawautambui hata mkutano wa Baraza la Madiwani uliomchagua kwani ulikuwa wa upande wa chama kimoja cha CCM..."

mkuu na tlp walikuwepo! sema idadi ya wajumbe haikutimia!
 
mkuu.... mwiba anatatizo la ulimi..... na hii inasababishwa na kuliwa dendi mara kwa mara
Tatizo umeharibika ukubwani yaani hujui hata unaandika kitu gani !!! mwiba
 
Hii imenipa moyo kwamba sasa Chadema imeanza kuelewa siasa ,kwani siasa sio vita ni mbinu na mikakati iliyokomaa kimipango,hili la kutoelekea mahakamani ni mwanzo wa kuonyesha kutokuwa na imani na mahakama zetu hapa Tanzania.

"...........Mala ambaye ni Diwani wa Kimandolu, alisema baada ya kukaa na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, wameona hakuna sababu ya kufanya hivyo kwani wanachojua wao ni kwamba nafasi ya Meya wa Jiji hilo bado iko wazi kwani kikao kilichomchagua Meya ni batili.Alisema hawataenda mahakamani kwani wamebaini kuwa wakifanya hivyo watakuwa wamejimaliza.
“Uzoefu unaonyesha kuwa kukimbilia mahakamani sio tija kwani kesi inaweza kupigwa danadana hata zaidi ya miaka mitano. Sisi bado tuna hatua nyingi tunazoweza kuzichukua kudai haki yetu, hatuna wasiwasi kwani tunaamini kuwa tunatetea haki ya wananchi walio wengi,” alisema Mala.
Kuhusu msimamo wao wa kumtambua ama kutomtambua Meya aliyechaguliwa, alisema sio tu kuwa hawamtambu Meya huyo, Gaudence Lymo, bali hawautambui hata mkutano wa Baraza la Madiwani uliomchagua kwani ulikuwa wa upande wa chama kimoja cha CCM..."

Kumbe wanafiki mko wengi sana Tanzania?? Hebu pitia haya mawazo yako hayo hapo chini uliowahi tuyatoa hapo 2010 juu hicho chama chako ukipendacho cha CHADEMA hapo mwaka jana.

CHADEMA kwisha kazi, Kikwete keshawapatia kwa tume yake ya JANJA YA NYANI na mkiingia tu laini kwenye hili basi tayari mtakua choo cha kike na wala hamtoweza kujiondoa humo tena.

Ikiwa Chadema imeshindwa na ustaarabu bora Msajili akifute Chama hiki,chama ambacho kinashindwa kujidhibiti na kuwezaa kufuata mkondo wa kisiasa,kwa nini hawaiangalii CUF wapi imetoka na wapi ipo ,hii leo !!

Mimi nawashauri Chadema wasitishe kuingia kwenye Bunge mara moja,nawahakikishia serikali itabadili muelekeo ,ni lazima itabadili muelekeo na vile vile lile lengo la kutomtambua Kikwete kama Raisi halali au alieshinda kihalali, hapo hapana ubishi ni lazima CCM na serikali yake ikae sawa na ni njia moja ya kidemokrasia kabisa.

Lakini kuwarubuni wananchi wakati mnaingia bungeni na kula na kusaza ,hili halikubaliki kabisa kisha kutaka kuwaburuza wananchi kwenda kuchezea maji ya washawasha ,nyie wabunge mnakuwa tandize na majokofu ya jumba la bunge,huo utakuwa utapeli kushinda wa mafisadi,amueni moja tuwafahamu.
 
Mwiba una shida ya r na l kama mimi! lol unaimanisha HONGERA

Tatizo hili lipo kubwa sana kwa upande wa wasukuma vilevile.

Cha muhimu ni kuwaelewa tu walikuwa wanamaanisha nini. Wakurya mkoani Mara ndo acha kabisa utavunjika mbafu.
 
hivi itakuwaje ukiitishwa mkutano wa baraza la madiwani? unaweza kuendelea ikiwa hawa wa chadema hawati hudhuria? kwa maana ya idadi ya watu wanao hitajika kwa kikao kufanyika.
 
Back
Top Bottom