Hoja nzito kwanini CCM ni wakupewa likizo

Kahabi

New Member
Jan 26, 2012
4
1
Ndugu zangu wana JF ni vyema tuwekane sawa kwa jambo hiil ambalo sote kama WaTanzania yatupasa kulichukua kwa uzito wa aina yake na kisha kila mmoja kwa nafasi yake ama yeye mwenyewe kuchua hatua au kuelimisha jamii inayo tuzunguka.nimezingatia makundi totofauti totofauti katika jamii, kwa mana kwamba hatuwezi kupata habari sawa sote. Wapo ambao wako pembezoni mwa nchi ambao kwao taarifa za vyombo vya habari hawapati. Lakini hatuwez tukasema tuwaache wasipate. Wapo pia wanaopata habari mbalimbali lakini hawajitambui walipo ambao kwao kila kitu wanajua kiko SUPER.kundi jingine ni la watu ambao hawataki kutafuta kujua nini kinafannyika na Serikali yao.

Ndungu zangu wapenda maendeleo ya Taifa letu,wazalendo wa kweli wa nchi yetu, wenye uchungu na rasilimali za Taifa makundi haya ya watu yote ni ya mhimu kwetu na kwa mkutadha wa Taifa letu.kuna philosophy isemayo, ‘’OPPRESSED IS THE MOST IMPORTANT WEAPON OF THE OPPRESSORS’’ ndiyo mana nasema sote kwa unyonge wetu tuelimishane juu ya nini tufanye kawawajibisha watawala bila kuchoka na bila kuona kuwa kundi fulani halitufai na mwisho wa siku wote tusimame na kuanguka pamoja kuelezea hisia zetu kwenye mambo ambayo tunaona watala wetu wamepuyanga na hivyo tuwape muda wa kutafakari kwa gharama ya kuwapa nafasi hizo wenye kujali wanyonge.

Natilia mkazo kwa kariba ya kutosha nafasi yetu kuamua nani anatufaa na nani wasiotufaa,hili ni swala mhimu sana tukitambua hilo hakuna atakaye tutisha na fedha zake za mikataba mibovu na wizi wa mamilioni ya fedha za jasho letu wenyewe. WanaJF wenzangu nafasi yetu kwenye kisanduku cha kula ndo njia pekee ya kuonyeshs nguvu zetu kwa mapapa wakubwa baharini,walafi,wanaoishi kama wako peponi kwa gharama ya maisha ya mama,dada,shangazi zetu ambao hufa kwa kukosa huduma bora hospitalini.ndugu zetu vijijini wanalazimika kukesha njiani wakihangaikia maji.

Nasema haya kwa uchungu mkubwa.CCM kinacho shika dola mpaka sasa wanaendelea kujipambanua katika jamii ya WaTanzania kuwa wamemudu kuhudumia jamii ya watu wake kitu ambacho sicho sasahi kwa sababu zifuatazo;

1: Wameshindwa kutimiza ahadi zao ndani ya ilani yao ya uchaguzi,kwa mfano maisha bora kwa kila Mtanzania.kwa ufupi hakuna dalili ya dhati ya kutekeleza maazimio ama sera hiyo,matokeo yake WaTanzania wanazidi kupata hali mbaya ya maisha kuliko ilivyo wahi kushuhudiwa.kupanda kusikotarajiwa kwa nishati ya dezeli na petrol kufanya mfumuko wa bei ya vifaa vya ujenzi na kusababisha wananchi maskini kushindwa kumudu bei hiyo hivyo kuongezeka kwa watu wanaolala kwenye nyumba za tembe na nyasi, pia mfumko wa nauli za magari na bidhaa mhimu kwa matumizi ya kila siku kwa mfano sukari,vyakula na vingine vya aina hiyo.Sasa hapa sijui tuchague kutokula na kutosafari.

2: CCM na serikali yake wameshindwa kudhibiti ongezeko kubwa la tabaka la kipato katika jamii ya WaTanzania kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kinachofanyika ni serikali kuabudu tabaka la wenye nacho na kuacha kuhudumia wasio nacho. Nachelea kutumia theory ya Darwins SURVNG FOR THE FITTEST inayo toa mazingira halisi ya Tanzania ilipofikia.Darwins anatazama jinsi maisha ya wanyama porini yalivyo, kuwa simba anaishi kwa gharama ya maisha ya swala mnyonge na wanyama wengine humwogopa sana.Ambapo hata kama kuna mnyama mwingine akamwonea huruma swala akitabishwa na simba basi hatothubutu kutoa msaada mana mbabe wake yuko pale .Basi wanyama wengine watabaki kumshuhudia swala tena kwa umbali wa kutosha ili wasidhuriki.

Tazama kundi la hawa tunaowaita vigogo kisha pima mwenyewe.Bila shaka utaafiki kuwa kundi hili ndilo linalo sujudiwa.Ni ukweli usio pingika kuwa si mkuu wa nchi wala wasaidizi wake, mawaziri wala waandamizi wanawaogopa na kuwapigia magoti vigogo hao. Viongozi wa nchi wameiacha nchi mikononi mwa vigogo wachache wanaojiamlia nini wafanya huku maskini wanyonge mithili ya akina swala wakionja uchungu wa shubiri. Kitendo cha walio jilimbikizia mali za wanyonge kupindukia kuendelea kulitafuna Taifa kwa gharama za maisha ya wanyonge ndio umekuwa msingi wa wanyang’anyi hawa kuishi.

WanaJF tumashuhuda wote kuwa trillions za pesa zetu zinateketea na wanyang’anyi na wala hakuna kiongozi anaye chukua hatua.Kwa mfano mamilioni mangapi ya pesa yalipotea kwenye mkataba tete wa kufua umeme na kampuni ya Richmond.Kampuni ambayo ilikuwa ikilipwa milioni 100 kwa siku.Je zile billion 133 za madeni ya akanti ya nje EPA ni hela kidogo?. Je bilioni ngapi ziliteketea TICTS. Je billion ngapi zimeteketea na KAGODA agricultural.Kwa mifano michache hiyo tujaribu kuangalia nani walifunga mikataba ile upande wa wamiliki na upande wa Serikali.

Bila shaka utaniambia kuwa ni kundi hili la walafi wakubwa wa fedha(VIGOGO) na viongozi wetu wenye kuimba nyimbo za kuwasifu mabwana hawa hatakama wanajua athali za mikataba ile.Mkataba wa Richmond na TANESCO na hatimaye DOWANS ni taswira ya vigogo jinsi wanavyo abudiwa na kupigiwa magoti kuanzia mkuu wa nchi mwenyewe,mawaziri,na maafisa wandamizi.

Walijua dalili za ubovu wa DOWANS jinsi ambavyo ingeweza kuwa mzigo mkubwa kwa walipa kodi.Lakini DOWANS ilipata tenda ile kwanini?. Ndg zangu tunajuzana, aliyekuwa nyuma ya pazia la dirisha hilo ni Bwn ROSTAM AZIZI ambaye wote tunaweredi wa kutosha ni mtu wa aina gani, nguvu yake ya kifedha inagharimu Taifa kiasi gani.Sasa narejea kusema watu hawa wanafanya kila liwezekanalo kusafisha hazina na rasilimali za Taifa kwa gharama ya wanyonge.

NINI KIFANYIKE

Ndugu zangu wapenda maendeleo ya Taifa letu,sote kwa umoja wetu tuunganishe nguvu zetu kila mmoja kwa nafasi yake tuelimishane ,tupashane habari, tujitambue kuwa nchi hii ni yetu sote na kuwa ongezeko la umaskini si makusudi ya MUNGU la. Tumejaliwa kuwa na rasilimali nyigi mno ambazo sote ni mali yetu, kwa minajili hiyo tukisimama na tuseme imetosha hakika itatosha na tutashuhudia mabadiliko makubwa juu ya maisha ya jamii yetu. Rais KAGAME wa majirani zetu Rwanda mwishoni mwa mwaka jana alisema right angekuwa anaongoza nchi yenye utajiri wa rasilimali nyingi kama Tanzania angetoa huduma bure kwa watu wake na wasifanye kazi yoyote.

Bila shaka KAGAME ni mwumini wa Philosophy isemayo GOOD GOVERNANCE IS THE PARAMOUNT TOOL OF SUCCESS. Kazi kwetu sasa kuchambua chuya ni ipi na mchele ni upi WAPI HUKO? 2015. KWENYE NINI? Kisanduku cha kura.

WanaJF sipati kigugumizi kutamka kuwa CCM haistahili kupewa ridhaa ya kuongoza nchi tena kwa sababu kuu zifuatazo;

I) Ikiwa wameshindwa hata kutekeleza maadhimio ya vikao vya kamati za juu kabisa vya maumzi vilivyowataka wanachama wake kuachia ngazi nafasi za uongozi za chama hicho walio husishwa na kashifa ya ufisadi wa mabilioni ya pesa.Sababu ilikuwa ni kukirejeshea chama heshima na kuaminika kwa wapiga kura wake. WanaJF CCM imeshindwa japo haieleweki kama magamba hayo ni magumu sana kiasi cha kutovulika. Watuhumiwa wote kwanza ndio wanatesa ndani ya nyumba.

Kama hayo maamuzi magumu waliyoyaita ya kuwavua nyadhifa waliokosa maadili na kukiuka miiko ya uongozi yameshindikana Je wataweza kufanya maamzi magumu ya kulitoa Taifa katika hali mbaya ya maisha inayowakabili WaTanzania?Kwa mfano nchi iko katika kiwango cha juu mno cha UFISADI, nchi iko kwenye wimbi la viongozi kukosa uzalendo,nchi imo kwenye hali mbaya sana ya uchumi usiokuwa imara,lakini piia nchi imezongwa na mawimbi makubwa ya bahari mithili yale ya NUNGWI ya pepo za kusi yaliyoikumba MV ISLANDERS viongozi kujilimbikizia mali.

Hiyo ni mifano michache ambayo kimsingi inahitaji maamzi magumu kuliko hata hayo ambayo CCM wameshindwa kufanya kwa wanachama wao.Eti kamati kuu imeshindwa sasa wanaadhimia maamzi yafanywe na ngazi za chini. Hawa ndio wanawataka WaTanzania wawape fursa ya kuongoza tena.Tutazameni, tumakinikeni. Kuna hatari ya maamzi ya nchi kwa mstakabali wa Taifa kuambiwa yanafanywa na wenyeviti wa vitongoji ua wajumbe wa mitaa. Lakini ndg zangu WanaJF bado wanatwaminisha kuwa wanaweza.Labda niulize hawa jamaa wanaweza kwa yapi?.

II) Sababu nyingine ni kuwa CCM ni wanafiki kuendelea kuhubiri siasa za ujamaa ilihali wao hao hao wanacheza kibepari .Kwa mfano njia zote kuu za uchumi zinamilikiwa na makampuni ya kigeni huku wazawa au Serikali wakibaki kuimba ndiyo mzee kwa mataifa ya magharibi.Tuangalie pia ardhi jinsi gani inavyomilikishwa kwa FOREIGN COMPANIES hakika ikiwa mwendo utakuwa ndio huu,siku si nyingi tutakuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu wenyewe.

Pia tusisahau kuwa azimio la Arusha Ia 1967 ambalo lilisheheni miiko ya uongozi bora.Kwa mfano kiongozi wa chama na Serikali kutoruhusiwa kuwa na hisa katika kampuni yoyote iwe nje au ndani ya nchi,kiongozi kutoruhusiwa kuwa na mishahara zaidi ya mmoja,kiongzi kutambua kuwa kupokea hela yoyote ni matokeo ya jasho lake (kazi), Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya nchi yetu kwa kuondoshea umaskini; ujinga na maradhi.WanaJF maazimio haya yalizikwa na azimio la Zanzibar la 1992.Je hawa wanatumikia sera ipi kama si kupoteza dira huku. Bado wanatutumainisha kuwa wanafaa.Yatosha kusema hivi, nguvu yetu wanyonge ni kubwa.TOGETHER WE CAN .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom