HOJA BINAFSI YA KUMUENGUA Lady doctor kwenye shindano la MISS CHIT CHAT..

Status
Not open for further replies.

Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,482
9,517
Ndugu waungwana wana chit chat salaam..

Naleta hoja hii mbele yenu ili tujadili na kufikia hitimisho la hiki kinachoendelea kwani ni dhahiri kuwa kuna kila dalili za mchezo mchafu unaofanywa aidha kwa dhahiri ama kificho ili kumfanya Lady doctor achukue taji hili kiupendeleo.

Awali ya yote ningependa kuwakumbusha japo kwa kifupi tu historia ya shindano hili hasa kwa wale wageni nalo.
Shindano hili lilikuwa likiendeshwa na ndugu Lundenga Ruhazwe JR ambapo katika kipindi chote alikuwa smart kwa kutojitanabaisha na mgombea yeyote.. Hii ilikuwa inajenga taswira ya kidemokrasia kwa wagombea na wapambe wake hivyo hata mgombea yeyote alipita kidemokrasia bila kuibua malalamiko...

TOFAUTI ILIYOPO SASA.

Katika shindano hili muandaaji na mratibu mkuu wa shindano hili ndugu Arushaone kwa uwazi kabisa pasi na kificho amejinatanabisha na mgombea mmoja ambae ni Lady doctor hadi kufikia hatua ya kumpigia kampeni za waziwazi kuwa ndiye anayetaka atwae taji hilo.. Katika mazingira haya unajengeka wasiwasi mkubwa endapo wagombea wengine watatendewa haki hasa shansarie ambaye ameonekana kuwa mwiba mkali kwa Lady doctor tangu hatua za awali za fainali hizi. Ni dhahiri kuwa Arushaone akiwa kama mratibu mkuu na muandaaji wa shindano yuko radhi kuhujumu shindano hili ili ashinde Lady doctor ambae ana maslahi nae binafsi kitu ambacho hakikubaliki KATIKA JAMII YETU YA KIDEMOKRASIA NA INAYOPENDA MABADILIKO YA KWELI.

WITO

Tulikatae jambo hili kwa kupinga kile anachofanya Arushaone dhidi ya wagombea wengine. TUCHAGUE KUWA UPANDE WA DEMOKRASIA NA USHINDANI HURU NA WA HAKI.

NAWASILISHA.
Baba V
Mwenyekiti wa mahusiano na ndoa Chit chat ©2012.
 
Last edited by a moderator:
Lady doctor all the way,
Hizo personal conflicts hata zisiharibu polls.:beer::thumbup::beer:
 
Hivj kuna muongozo wowote wa kuendesha shindano hili? Kama upo je ni kifungu gani kimekiukwa ili tuweze kujadili jambo lako

Mkuu sio kila jambo ni lazima liandikwe.. mengine yanahitaji tu busara ya kawaida kuyang'amua.. ndio maana kuna unwritten constitution pia... tuangalie katika yale yaliyoainishwa.. je ni halali kile anachokifanya muandaaji wa shindano..!!?
 
Nimeona sehemu pia yeye kama muandaaji anatoa sh.10,000/=
Afu ndiyo rais wa shindano!!

Lakini Arushaone hebu kumbuka kipindi mchakato unaanza we mwenyewe kuna kauli nzuri sana ulizitoa zakutoshiriki katika kampeni!!

Shindano uandae wewe! Mshindi umtafute wewe..
Mbona majanga???
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sio kila jambo ni lazima liandikwe.. mengine yanahitaji tu busara ya kawaida kuyang'amua.. ndio maana kuna unwritten constitution pia... tuangalie katika yale yaliyoainishwa.. je ni halali kile anachokifanya muandaaji wa shindano..!!?

Huu mchakato ulifaa upingwe kwenye hatua za mwanzo na sio kukaa hadi mwisho then ndio yanaletwa malalamiko
 
Huu mchakato ulifaa upingwe kwenye hatua za mwanzo na sio kukaa hadi mwisho then ndio yanaletwa malalamiko

Mkuu unaanza kupinga jambo pale unapoanza kuona linaenda ndivyo sivyo. Awali hatukudhani kama Arushaone angekengeuka na kutenda kama hivi. Tumeanza kumpigia kelele baada ya kuona anaharibu..
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom