IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
Habari zanu wanajamvi,
Kwanza niwashukuru wanajamvi wote wanapost habari zinazoonyesha wazi kukerwa kwao na vitendo vya rushwa.
kwa siku za karibuni malalamiko dhidi ya vitendo vya rushwa yameongezeka maradufu. Mfano mkubwa ni malalamiko yamkambi mbalimbali za uchaguzi ndani ya CCM, malalamiko ambayo hata Rais Kikwete mwenyewe ameyatoa katika majukwaa. Vile vile, wakongwe wa CCM pia wamesikika wakilalama kuhusu rushwa. Wabunge pia wamehusishwa na rushwa ambayo kamati maalumu iliyoundwa ilikamilisha ripoti yake wakati ambao mbunge mmoja ana kashfa ya matairi ya TANESCO.
Ni muda mrefu sasa TAKUKURU imekuwa kimya dhidi ya vitendo vya rushwa ambavyo hata Rais mwenyewe anaviona na kuvifahamauSwali kubwa ni kama Rais mwenyewe anaoushahidi wa vitendo vya Rushwa...je TAKUKURu wanafanya nini?
Hivyo basi napendekeza TAKUKURU ivunjwe. Tume hii inatumia fedha nyingi za walipa kodi kuwalipa wafanyakazi ambao hawafanyi lolote. Pia, kuna tetesi kuwa Wafanyakazi wa TAKUKURU ni wapokea rushwa kupindukia. Tunaishi nao mtaani na wanapata maendeleo ya harakaharaka mno ambayo inasadikiwa ni kutokana na malipo ya fadhila za kuzima harakati za kuwafichua watoa rushwa.
Napenda kuwaomba wanasheria waliomo humu jamvini kuangalia jinsi gani yaweza kutengenezwa motion ya kuivunja TAKUKURU.