Prisoner 46664
JF-Expert Member
- Dec 18, 2010
- 1,948
- 1,237
kwa mujibu wa katiba ya yetu ya mwaka 77, ili mtanzania agombee ubunge, anapaswa kuwa na umri usiopungua miaka 22. ruhusa huu umefanya bunge letu liwe na wabunge wengi vijana. ni jambo zuri! tatizo langu liko kwenye mwenendo na tabia ya vijana kwa ujumla. wabunge wengi vijana akina zitto, kafulila, mnyika, sugu. mkosamali, mdee, magige, bulaya.... nk..... hawajaoa au kuolewa. pana umuhimu kwao kuoa au kuolewa
NDOA HUJENGA AKILI NA NA HULETA HESHIMA
nasisitiza wakaoe au wakaolewe kwa sababu uwezo wa kufanya hivyo wanao. ndoa humfanya mtu ajiheshimu na pia aheshmike. jamii humuona alieoa kama mtu aliekamilika.
UJANA UNAWASUMBUA WABUNGE VIJANA
umri wa mtu aghalabu kuathiri upeo wake wa kufikiri na kujieleza. kitendo cha mnyika kumtukana mh Rais bungeni na kumuita dhaifu ni kinyume cha kanuni za bunge na ni kinyume na desturi zetu watanzania. la kushangaza alichokua anazungumzia hakimhusu Rais moja kwa moja! kusema hadharani bungeni kuwa "rais kikwete ni dhaifu" ni kauli ya kumdhalilisha mh rais. mnyika licha ya kuwa na shahada ya chuo kikuu, damu ya ujana inamsumbua. aliombwa na naibu spika kufuta kauli yake lakini akakaidi kufanya hivyo! mchango ambao angeutoa kuwawakilisha wana ubungo kuhusu bajeti hakuweza kuutoa baada ya kutolewa nje ya ukumbi wa bunge na naibu spika ndugai
NINI KIFANYIKE?
kwa nia njema nashauri katika maoni ya katiba mpya, tupendekeze umri wa mbunge uanze miaka 30. umri huu mtu anakuwa keshapitia mikiki mingi ya maisha. anajua la kusema kama mtu mzima aliekamilika. naomba kuwasilisha!!!!!!
livingstone lusinde kibajaji ameoa,ana watoto(wala sio mtoto) na ana miaka zaidi ya 30..kwa maana hii,kwa vipimo vyako vya busara..huna hoja.
Halafu watanzania mtaacha lini uoga??lini hasa??rais mmemchagua wenyewe,kama amekuwa dhaifu asiambiwe jamani??kwani amekuwa nani?mfalme?yesu?mohammad?au malaika?Nadhani kama tumempa kazi na ameshindwa kuifanya kwa mkono hodari..yeye ni DHAIFU!