HIZO KAULI ZAO: Tulilaan, Tukapinga na Kuunga mkono na kupongeza Jitihada za Kuwashitaki - TUKABEZWA

Ndugu yangu,

Wasamehe tu bure na zidi kuwaelimisha ni upofu tu si kosa lao, waombee Mola awape ufahamu na akili ya kufikiria na kung'amua mambo katika mazingira yanayowazunguka. Unajua nyote mnaweza kuona jambo moja na kusikia sauti ile ile lakini ni namna gani kila mmoja akili yake inaweza kutafasiri kisahihi alichokiona na kukisikia ni tofauti.Wako wengi ambao mpaka wanyeshewe mvua ndo hutambua kuwa mawingu waliyoona ndo ilikuwa ishara ila baada ya hapo huwa wanafunzi makini zaidi.

Shehe ponda amefufua watu,watu walewale waliokuwa wanashangilia askari kupiga mabomu na kuua raia kwenye mikutano ya kisiasa usiku mzima wa jana nimesoma post zao wakiwalaani polisi.Namuachia Mungu watu hao atajua atakavyowalipa.
 
Hapana umejichanganya mwenyewe...!! CDM ni Chama cha kisiasa, mimi ni Mtanzania wa kuzaliwa mwenye asili ya Tanganyika (Tanzania Bara). Nisaidie kujua umechanganyikiwa wapi nione jinsi ya kukusaidia, kukwamua akili zilizokwama na kuzijenga katika misingi isiyomchanganya mtu ndo tamaa iliyoko moyoni mwangu. Hoja kuu ni KUPINGA NA KULAANI UDHALIMU NA TABIA YA SERIKALI/DOLA KUENDELEA KUTEKELEZA MAUAJI YA RAIA KWA RISASI NCHINI MWETU. KARIBU!

We CDM nini mbona kama unanichanganya?
 
Unajua haya mambo yalivyo...mpaka siku atakufa nape au mwigulu ndo watu wataamka...ipo siku tu wewe subiri...
 
Nilisema na nitaendelea kusema watu wali "under estimate" uzito wa kauli ya Pinda, hakuweka mipaka, tulioipinga tukaonekana wajinga, leo ndo kuna watu wanafumbua macho... Ponda's matter is a turning point huh..!!!?
 
Bado wapo mashabiki wanaotetea polisi na serikali kwa uchafu huu na uhuni aliofanyiwa Mzee Ponda.

Pinda, Mwigulu, Lukuvi etc watakuwa wanachekelea kama walivyofurahia damu iliyomwagika Arusha. Kwao damu kumwagika ni ushindi kwa ccm.
 
J.W. Mawlicela, Mwigulu, Nape na Pinda bila shaka watajitokeza na kuilaani CDM kama mtuhumiwa namba moja.

Lakini hapa Nape humwoni kwenye hili, ila kesho unaweza kusikia ameibukia kwenye magazeti ya Jamhuri na habari leo akiitaka Serikali kuchunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika.
 
Mnijuze jamani yale maandamano ya watu wa pwani kupinga haki za binadamu kumshitaki Pinda yamefikia wapi!
 
Inauma sana..mimi ni mkirsto lakini ili la shehe ponda limenitoa machozi sana
Roho inauma sio kwa sababu ya dini iliyopo peke yake ni kwa sabbu ww ni MZALENDO na ndo huo tumefundishwa kipindi tuko shule

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
...nilisema..."wakisha tupiga Chadema tukaisha watawageukia na nyinyi wa Lumumba kwani mtu akishaonja nyama ya binadamu hawezi kuacha kuila"(mkacheka na kukebei kadri mlivyoweza)...sasa nyie vikaragosi wa Lumumba nawaambieni tena "tieni maji"...jana ilikuwa,Ally Zona,Ulimboka,Mwangosi,Kibanda,wanaArusha(Chadema),wanaMtwara na leo ni Sheikh Ponda,je kesho nani atafuatia?...TAFAKALI...
 
WATAFAKARI...!! Labda watakusikia leo, sijui wamefanywaje akilini kiasi kwamba hata ukiwaambia saa hizi ni nne asubuhi watabisha na kukwambia ni usiku wa manane. Hawa jamaa nilishashindwa kuwaelewa, wana nini kinachowapofusha hivyo!! SIELEWI

...nilisema..."wakisha tupiga Chadema tukaisha watawageukia na nyinyi wa Lumumba kwani mtu akishaonja nyama ya binadamu hawezi kuacha kuila"(mkacheka na kukebei kadri mlivyoweza)...sasa nyie vikaragosi wa Lumumba nawaambieni tena "tieni maji"...jana ilikuwa,Ally Zona,Ulimboka,Mwangosi,Kibanda,wanaArusha(Chadema),wanaMtwara na leo ni Sheikh Ponda,je kesho nani atafuatia?...TAFAKALI...
 
Shehe ponda amefufua watu,watu walewale waliokuwa wanashangilia askari kupiga mabomu na kuua raia kwenye mikutano ya kisiasa usiku mzima wa jana nimesoma post zao wakiwalaani polisi.Namuachia Mungu watu hao atajua atakavyowalipa.
Watanzania tunatafuta kitu kinachotugawa.
Na CCM imefanikiwa kwa hilo kwa kiasi fulani...
Ila mda si mmrefu watajikuta silaha wanazotumia kutugawa ndo hizo tutazigeuza silaha za kutuunganisha.
 
Back
Top Bottom