Hizi ni dalili kuwa Rais Magufuli ana mapungufu ya uongozi?

January Makamba na mwigulu walipiga billion 1.7 wakati kampeni ikiendelea huku wakiwa na tuhuma zingine kibao zikiwemo za mwigulu kuchukua pesa za Escrow kwenye Gunia na kupokea 10% toka kwa wazabuni wote waliokuwa wakiidai Serikali pesa nyingi.

Mungu isaidie Tanzania
 
Kikwete kawashauri mmushambulie yeye na mmuache Magufuli afanye kazi. nyie vipi hamuelewi? ebo!

Rais Magufuli - mapungufu ya uongozi

Sijaridhika wala kukubaliana na utumbuaji wa majipu wa huyu Mheshimiwa Magufuli, ambaye ni Rais wa Jamhuri yetu ya Muungano.

Jambo la kwanza alilonikosesha nisimwamini kwa asilimia kubwa niusanii namna alivyokwepesha kashfa ya watu binafsi waliojimilikisha UDA na kuikosesha serikali mapato kwa kukwepa kodi. Suala la UDA limefukiwafukiwa hadi sasa linaonekana kutopewa uzito stahiki.

Uteuzi wa baraza la mawaziri umedhihirisha hana jipya zaidi ya kuwanyanyapalia dagaa huku wahusika wakuu wa kashfa bandarini, Escrow na TRA waliokuwa mawaziri na makatibu wakuu wa serikali ya Kikwete akiwatunukia uwaziri tena na kuendelea Ukatibu Mkuu licha ya kashfa nzito zilizoibuliwa na bunge hadi kuachia ngazi.

Kushindwa kushughulikia mgogoro wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar dalili tosha Rais Magufuli kadiri ya msimamo wa CCM hana ubavu kwa chama chake, bali kukipigia magoti tu. Hana nguvu alina nayo kikatiba ila kutii matakwa ya chama chake.

Dhahiri alichoanza Rais Magufuli ni nguvu za soda, hatimaye yatakayojilia ni kukata tamaa na kuendelea na mazoea bora liende muhula uishe.
 
Khaa!! Sasa yakianza kutumbuliwa majipu ambayo bado hayajaiva sawsawa sijui itakuwaje humu :mvutaji:
 
hata mwenyezi mungu alifanya kazi kwa siku saba na ndio ana nguvu zote sembuse binadamu. Hebu mwacheni afanye kazi yake. Sisi watu wa kawaida tunafurahia sana poleni zenu msubiri tu zamu yenu!!!! Na kama unaamini ni nguvu ya soda basi wewe endelea tu kuisoma namba!

hili jukwaa lingetumika kwa nia ya uchambuzi lingevutia wengi. Bahati mbaya uchangiaji wa hoja nyingi unajaa ushabiki wa vyama na itikadi!.
 
Magufuli piga kazi,Ukizisikiliza hoja za hawa jamaa walioshindwa utapoteza muda wako bure.Mwanzo walisema hawautambui ushindi wako,ajabu sasa wanataka kukupangia baraza la mawaziri!!
 
Magufuli piga kazi,Ukizisikiliza hoja za hawa jamaa walioshindwa utapoteza muda wako bure.Mwanzo walisema hawautambui ushindi wako,ajabu sasa wanataka kukupangia baraza la mawaziri!!

Jibu hoja zilizoanikwa kwenye mada.
 
matatizo yatatuliwe maoema kabla hayajawa mazito zaidi

Utumbuaji wa majipu umeisha? Sijaona tena safari za kushtukiza za Mheshimiwa Magufuli, sijaona tena utumbuaji wa majipu zaidi ya lile la bandarini, kisha alipogusia jipu la UDA imeelekea kasi imepungua ghafla, nini tutegemee zaidi?
 
Humu jamvini kuna watu ukisoma post zao unspata kiungulia kabisaa eti watu wanamchagulia rais mtu wa kumteua kuwa waziri hiki ni kituko live u comedian mwingine shidaaa
 
Watu sasa hivi wanazungumzia uteuzi wa mwenye kashfa ya escrow! Wakati wanamteua kinara wa kashfa ya Richmond kugombea urais walitumia ujasiri wa mwendawazimu kutuaminisha kuwa huyu ndo alikuwa msafi. Kimsingi nyie walalamishi hamna credibility yoyote ya kumlaumu JPM kwenye baraza lake. JPM anatumia best intelligence he has. Tusubiri utendaji neo tufungue midomo.
 
Mkuu, Mzee wa msoga tulimpa mud a Na tuliona alichokifanya kwa uchumi wa nchi, ukisha umwa na nyoka hata ujani utakushtua. Kwa mbwembwe za mheshimiwa Magufuli alizo-anza nazo tulitegemea angekuja na timu mpya kabisa, lakini kaingia na wale wale walioachwa na awamu iliyopita na walio mpigia kampeni.

Magufuli amemteua Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, huyu nae tunaweza kujenga hoja kuwa uteuzi wake umetokana na kumpigia kampeni?

Mimi naamini kina Mwigulu, Muhongo n.k. wameteuliwa kwasababu wana uwezo haijalishi kwamba wamepigia kampeni.

Ni suala la kuwapa muda tu, tuone watafanya nini... Tujifunze kuweka akiba ya maneno tusijekuumbuka baadae. Wakati Majaliwa alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu kuna watu walibeza... Muangalie leo anavyofanya mambo makubwa!

At Makumbusho.
 
Ukawa wako kwenye harakati kubwa san warudi kwenye chart bahatimbaya kila wanachobuni hakuna anayejishughulisha nao jpm amebamba kila kona.
 
Sasa kama ya Kikwete ndio manyumbu waogope kuitaji?
wanafiki sana nyie...

Nyumbu ni ccm ambao Nchi ina miaka 54 bila maendeleo wapo tu wamekariri Akili za Nape kuwa ipo siku mungu atafanya miujiza Tanzania itakuwa kama German.
 
Rais Magufuli - mapungufu ya uongozi

Sijaridhika wala kukubaliana na utumbuaji wa majipu wa huyu Mheshimiwa Magufuli, ambaye ni Rais wa Jamhuri yetu ya Muungano.

Jambo la kwanza alilonikosesha nisimwamini kwa asilimia kubwa niusanii namna alivyokwepesha kashfa ya watu binafsi waliojimilikisha UDA na kuikosesha serikali mapato kwa kukwepa kodi. Suala la UDA limefukiwafukiwa hadi sasa linaonekana kutopewa uzito stahiki.

Uteuzi wa baraza la mawaziri umedhihirisha hana jipya zaidi ya kuwanyanyapalia dagaa huku wahusika wakuu wa kashfa bandarini, Escrow na TRA waliokuwa mawaziri na makatibu wakuu wa serikali ya Kikwete akiwatunukia uwaziri tena na kuendelea Ukatibu Mkuu licha ya kashfa nzito zilizoibuliwa na bunge hadi kuachia ngazi.

Kushindwa kushughulikia mgogoro wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar dalili tosha Rais Magufuli kadiri ya msimamo wa CCM hana ubavu kwa chama chake, bali kukipigia magoti tu. Hana nguvu alina nayo kikatiba ila kutii matakwa ya chama chake.

Dhahiri alichoanza Rais Magufuli ni nguvu za soda, hatimaye yatakayojilia ni kukata tamaa na kuendelea na mazoea bora liende muhula uishe.

Huo ni utoto mmbo yote hayo huwezi kushughulikia siku 30
 
Watu sasa hivi wanazungumzia uteuzi wa mwenye kashfa ya escrow! Wakati wanamteua kinara wa kashfa ya Richmond kugombea urais walitumia ujasiri wa mwendawazimu kutuaminisha kuwa huyu ndo alikuwa msafi. Kimsingi nyie walalamishi hamna credibility yoyote ya kumlaumu JPM kwenye baraza lake. JPM anatumia best intelligence he has. Tusubiri utendaji neo tufungue midomo.
Richmond ni ya Kikwete na hata escrow ni yake pia hao wengine wamenunua kivuko kibovu mabehewa mabovu mikataba mibovu ya Gesi kutafuna pesa za chenji ya rada na bunge la katiba nk , Nchi hakuna msafi hata majaliwa mwenyewe ni Ndugu yake kikwete hata uteuzi wake umetokana na mkono wake
 
Wapiga

Sasa kama Richmond ni ya JK mbona mnaogopa kuitaja, mnalalamikia ESCROW tu..
Nyie watu ni wanafiki na walaghai, heshima ndogo ya uaminifu mliyopewa na wa Tz mnaitumia vibaya, saivi mnaonekana mpo sawa na CCM tu, wote wapigaji.
KATAA KUWA NYUMBU
 
Hii ni tabia yetu binadamu kumhukumu mtu kwa kosa moja na kufuta mazuri yake yote. Tumeanzia baraza la mawaziri na majibu wakati wa maswali ya waandishi. Hii inaonesha wengi wetu hatumfaham huyu jamaa. Mimi nafuatilia sana utendaji wake. Jamaa yuko vizuri na tusubiri mtaniambia kama hatawagusa hata mnaodhani hawataguswa. Jamaa hana tabia ya kuchoka nawaambia mtaniambia. Tushukuru tumempata rais wa wanyonge. Hata hivo akiwagusa viongozi wa ukawa msianze kusema analipiza kisasi. Jamaa nina uhakika 100% kwa 100% kuwa jamaa huwa anapita humu pia. Aliyependekeza kuangaliwa upya sheria ya manunuzi ataniunga mkono maana hili limetekelezwa. JF ni jukwaa la mawazo yetu wanyonge. Long live Jamii Forum.
 
Back
Top Bottom